Naombeni ushauri kwa huyu mwanamke

kibovu

JF-Expert Member
Apr 17, 2017
701
753
Ndugu zangu nimekuwa ndugu yenu nikiishi na mwanamke geto huku wote tukiwa ni wanafunzi wa vyuo tofauti hapa dsm but Mimi nimekuja kimasomo tukaanzisha mahusiano taaluma yangu ni mwalimu

Ndugu zangu nimeishi na binti huyu Geto moja namhudumia kila kitu ispokuwa ada tu. Mbali na ualimu mimi ni mfanyabiashara kipato changu kwa mwez sio chini ya milioni moja.

Ndugu zangu juz Dada yake aliugua huko mkuranga akapata taarifa akaniambia tukiwa geto naenda mkuranga nikamuambia mpe Pole shem akasema sawa akaniomba nauli nikampa elfu kumi akaondoka.

Siku za nyuma nilimpa laki moja kwa ajili ya Emergency yoyote sio matumiz ya nyumbani.

Amerudi nikamuuuliza naomba ile laki niliyokupa ananiambia imetumika kwa dada yake imebaki elfu50 nikamuambia mbona unapewa majukum makubwa ilihali ww mwanafunz na ikumbukwe kuwa dada yake huyo kaolewa na jamaaa akanijibu kwa hiyo umechukia pesa yako kutumika huko nikamjubu ww ni mwanafunz hupaswi kupewa majukum makubwa akanijibu nimetumia kwa matumiz yangu mwenyewe ww kwani huna matumiz? Nikamuambia Kwanzia Leo emergency money ntazishika mwenyewe na of course Nilikuwa nataka zikifika laki5 nimpeleke Zanzibar tukaenjoy kwa sababu matumiz kila kitu nakamilisha kuanzia lotion, spray, nk. Kwa hiyo kuna pesa huwa napata kwenye biashara nikiona mapato mazr Kias nampa hata laki 2 au3 ashike lakini nimekuwa nakuta zimepungua.

Jana amerudi toka mkuranga amekuta vyombo vichafu kama alivoviacha ameanza kunigombeza umeshindwa kuosha vyombo kuanzia leo ntakuwa sipiki nimemjibu kuwa majukum ya kaz za ndani ni ya mwanamke akaniambia ww hujanilipia Mahalia sisitahili kukupa huduma zote. Akawa kachukia nakusema hatanipikia chakula na wadau nimeishi na huyu binti miez sita nikimhudumia kila kitu kanifulia nguo zangu mara mbili tu.
Tulipoamka asubuhi baada yakunipa ile elfu hamsini nikampa elfu kumi akaicha kitadani tukaondoka kwenda kupanda daladala

Naomba ushauri juu ya hili je ananifaa huyu binti kuwa mie?
 
Wewe ndo mbaya, huyo binti umempa hela za emergency, sasa kama imegence imetokea akatumia mbona umalalamika?

Na kweli hujamtolea mahari wala nn, unataka akufanyie nn? Nawe kweli mtu kasafiri anakuta vyombo vichafu, halafu unamjibu kwa jeuri hivyo, we ulitaka yy afanyaje? Jiweke na wewe kwenye nafasi yake bas uone anavyopata taabu.
 
kwenda huko , yani wewe umgonge mtoto wa watu, umpikilishe kwenye jiko lako la kuinama plate moja, akufulie afanye usafi na bado unalalamika kutumia hela yako ya emergency ,... kama unataka kumfaidi kaoe huko ,,.. yani nadhani mimi ungekuwa umeshaandika thread ukiunganisha nikitabu cha page 300, we soma kwanza jijenge halafu oa acha hayo mambo wacha akugombeze kabisa na kukutoboa hayo macho
 
Mkuuuuu kweli mwanaume wako apike aoshe vyombo ww upo na mnaishi geto 1that's stupid
 
Wewe ndo mbaya, huyo binti umempa hela za emergency, sasa kama imegence imetokea akatumia mbona umalalamika?

Na kweli hujamtolea mahari wala nn, unataka akufanyie nn? Nawe kweli mtu kasafiri anakuta vyombo vichafu, halafu unamjibu kwa jeuri hivyo, we ulitaka yy afanyaje? Jiweke na wewe kwenye nafasi yake bas uone anavyopata taabu.
Na yeye mwanamke kama anajua hajatolewa mahari pale anafanya nini?Anagharamiwa kila kitu,kasoro ada...kazi ndio hataki?.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom