Kwa upande wa mama yangu tumezaliwa wawili tu yaani mimi na huyu mdogo wangu ila mama na mzee walishatangulia mbele za haki [mama kafariki nikiwa na miaka mi3 na mzee nikiwa na miaka 13 ]
huyu mdogo wangu Yeye yupo nyumbani anakaa na mama mkubwa ( step mother )
Sasa mimi ni Juzi tu nimemaliza chuo kwa mbinde sana mana nmejitegemea kila kitu miaka yote mitatu mpaka namaliza, sikuwa na wakumwelekezea shida zangu zozote ingawa kwa upande wa Baba tupo watoto 16 na sisi ndio wa mwisho na hawa ndugu zetu wote kila mtu ni mambo safi kweli ( kweli kutoa ni moyo 🥲)
Sasa huyu mdogo wangu kanitumia Hii meseji nimepatwa na stress sana wakati ni Juzi tu nmeongea na huyu mama mkubwa wangu tukakubaliana kuwa atampeleka mdogo wangu chuo ila ntakua nampa back up kwa vitu vidogo vidogo kama matumizi ya apa na pale.
Mimi saiv ndo nmeanza biashara bado hata sijafikia ile level ambayo nimejiwekea malengo nifikie lakini nakumbana na majukumu mazito kama haya.
Binafsi apa nilkua napambana nipate hela niingie Law school mwezi July lakini izo dalili naona kabisa zikififia🥲
Kinachoniuma ni mdogo wangu af ni mtoto wa kike na tumezaliwa wawili tu, Naombeni ushauri nifanye nini ili nijue namjibu vp huyu mdogo wangu in a positive way [emoji120]
View attachment 2469632
Pole mkuu na changamoto za Maisha
Sijui umri wako ila naimani unaweza kupambana na changamoto Kwanza kwa sababu ni Mwanaume lakini pia kwa sababu ni Msomi
Uanaume utakufanya upambane kadri unavoweza bila kukata tamaa na bila kijari aina ya kazi na Elimu yako itakusaidia kubadirisha changamoto kuwa fursa
Huo ni mzigo wako kwa sasa na ata ulaumu ndugu ni kazi bure maana haitabadirisha chochote, me pia ni muhanga wa njia ambayo anataka kupita mdogo wako
Mimi pia alienisaidia ni Sister wangu tu na sio Mzee wala ndugu wa Mzee japokuwa walikuwa wapo njema kiuchumi, kuna siku unakuta nimefukuzwa shule Ada, inabidi nirudi home kutoa taarifa kisha sister anaingia ndani anajifungia analia sana
Kuna muda hadi nikawa najichanganya kitaa kusaka deal ili angalau nipate chochote cha kuongezea nguvu ila akijua anamaindi sana, hakutaka kabisa niwe mtu tofauti na yule ambae alikuwa katika Akili yake
Alikuwa anapenda me nisome ili nisije kuwa sawa na vijana wengine ambao wapo pale mtaani ila alikuwa na changamoto ya kipato na bado haikumkatisha tamaa bali ilimkomaza kiakili na kujua ni namna gani apambane kuongeza kipato ili kukidhi mahitaji
Bora yako una deal na mtu mzima ambae anajielewa na unaweza kumweka chini na kumpa ukweli wa mambo ulivo,ukamwambia ni jinsi gani unajinyima ili yeye awe sehemu Fulani, me sister wangu amenichukua nikiwa na darasa la 4 hadi university
Sasa wewe unamzidi Sister wangu vitu vikubwa vitatu, Kwanza Jinsia lakini pia Elimu na mwisho kabisa una njia rasmi ya kukuingizia kipato chako halali ata kama ni ndogo ila utaongeza kulingana na Elimu yako
Hivo we anzia hapo hapo ulipo usidhani kuna siku utaamka na hiyo hela unayolia kuwa huna, Anza Kwa kumfanyia maombi katika vyuo vizuri, mengine yatajulikana huko huko mbele ya safari
Kama ana ufaulu mzuri anaweza kupata Government support na ukajikuta umepunguza sana mzigo ila hilo usiliweke sana kichwani, we jiandae tu kulipa Ada na uzuri Ada zinalipwa kwa awamu hivo kama kweli umeamua ni ngumu kushindwa kabisa
Nyongeza, me pia sipendi sana kuchat na mtu ambae anaandika kama huyo mdogo wako, na waga sijibu SMS ya mwandiko huo unless otherwise nimeambiwa habari ya Ugonjwa
All the best