Naombeni ushauri kuhusu huyu mdogo wangu

Kwa upande wa mama yangu tumezaliwa wawili tu yaani mimi na huyu mdogo wangu ila mama na mzee walishatangulia mbele za haki [mama kafariki nikiwa na miaka mi3 na mzee nikiwa na miaka 13 ]

huyu mdogo wangu Yeye yupo nyumbani anakaa na mama mkubwa ( step mother )

Sasa mimi ni Juzi tu nimemaliza chuo kwa mbinde sana mana nmejitegemea kila kitu miaka yote mitatu mpaka namaliza, sikuwa na wakumwelekezea shida zangu zozote ingawa kwa upande wa Baba tupo watoto 16 na sisi ndio wa mwisho na hawa ndugu zetu wote kila mtu ni mambo safi kweli ( kweli kutoa ni moyo 🥲)

Sasa huyu mdogo wangu kanitumia Hii meseji nimepatwa na stress sana wakati ni Juzi tu nmeongea na huyu mama mkubwa wangu tukakubaliana kuwa atampeleka mdogo wangu chuo ila ntakua nampa back up kwa vitu vidogo vidogo kama matumizi ya apa na pale.

Mimi saiv ndo nmeanza biashara bado hata sijafikia ile level ambayo nimejiwekea malengo nifikie lakini nakumbana na majukumu mazito kama haya.

Binafsi apa nilkua napambana nipate hela niingie Law school mwezi July lakini izo dalili naona kabisa zikififia🥲

Kinachoniuma ni mdogo wangu af ni mtoto wa kike na tumezaliwa wawili tu, Naombeni ushauri nifanye nini ili nijue namjibu vp huyu mdogo wangu in a positive way

View attachment 2469632
Mpambanie mdogo wako sana asome chuo alafu acha kumind mambo madogomadogo unamfanya dogo ashindwe kukushirikisha mambo mengi zaidi hizo sms zako za kummind hapo juu sio nzuri..
Mpende sana mdogo wako wa kike anaweza kuja kukufaa siku moja hutaamini ila amin...
 
Hata kama tumeumbiwa shida mimi bado mdogo jamani kubebeshwa hili jukumu ni msalaba mzito.

Biashara ikue, Niingie Law school July plus makandokando mengine na mdogo wangu tena jamani, tena Chuo wakati Bi Mkubwa anao uwezo wa kusomesha.!!

Whyyyyyyyyyyyyy me

Ishu ikigoma usilazimishe sana mkuu.
Anza kumfundisha biashara aujue ulimwengu jinsi unavyokwenda kisha mambo ya kusoma chuo ataenda siku zijazo mambo yakishakaa sawa.
Mambo siku hizi yamebadilika unaweza kuwa na vyeti vya chuo na maisha yakagoma kwenda so ni vizuri kumuandaa awe multipurpose asikariri njia moja ya kutokea

Sent from my SM-C7000 using JamiiForums mobile app
 
Mpambanie mdogo wako sana asome chuo alafu acha kumind mambo madogomadogo unamfanya dogo ashindwe kukushirikisha mambo mengi zaidi hizo sms zako za kummind hapo juu sio nzuri..
Mpende sana mdogo wako wa kike anaweza kuja kukufaa siku moja hutaamini ila amin...
Mimi na mdogo wangu tunapendana sana mkuu ila mi sio mtu wa kuendekeza upuuzi, nakuchana on the spot maana ana mwandiko wa kitoto sana ila kila nikimwambia haelewi.

Hawa watoto wa kike ukiwalea kama yai mwisho wa siku utaskia kabebeshwa mimba na jamaa hata haeleweki so kwa sasa anivumilie tu na tabia zangu mpaka atakapoweza kujitegemea mwenyewe
 
Wekeza kwenye mpango wa uhakika zaidi, ambao ni wewe mwenyewe. Dogo asubiri kwanza mpaka utakapojiweza, since ni elimu ya juu anyway.

Btw, mawasiliano yenu yanaonyesha hampo karibu, unamchukulia tu kama jukumu. Sio fresh, mkuu.
 
Ishu ikigoma usilazimishe sana mkuu.
Anza kumfundisha biashara aujue ulimwengu jinsi unavyokwenda kisha mambo ya kusoma chuo ataenda siku zijazo mambo yakishakaa sawa.
Mambo siku hizi yamebadilika unaweza kuwa na vyeti vya chuo na maisha yakagoma kwenda so ni vizuri kumuandaa awe multipurpose asikariri njia moja ya kutokea

Sent from my SM-C7000 using JamiiForums mobile app
Nakubaliana nawewe mkuu japo nilishaomba Law School nikapangiwa Intake ya July na hela tayari ipo ila bado naifanyia mizunguko kwenye biashara.

Itabidi nifuatilie kama kuna consequences zozote za mimi kutoripoti Law School Mwaka huu ili nijue nafanyeje mana apa nina stress ata uwezo wa kufikiri umepungua
 
Wekeza kwenye mpango wa uhakika zaidi, ambao ni wewe mwenyewe. Dogo asubiri kwanza mpaka utakapojiweza, since ni elimu ya juu anyway.

Btw, mawasiliano yenu yanaonyesha hampo karibu, unamchukulia tu kama jukumu. Sio fresh, mkuu.
Asante kwa ushauri mkuu.

Mimi nikiri linapokuja suala la mawasiliano kwa njia ya simu ni changamoto, sio kwa mdogo wangu tu bali kwa watu wote sababu ya ubize.
Mdogo wangu huwa nina ratiba ya kumpigia simu kila ifikapo Jumamosi na Jumapili kumjulia hali, siwez kuchat nae sababu ya mwandiko wake
 
Kwa upande wa mama yangu tumezaliwa wawili tu yaani mimi na huyu mdogo wangu ila mama na mzee walishatangulia mbele za haki [mama kafariki nikiwa na miaka mi3 na mzee nikiwa na miaka 13 ]

huyu mdogo wangu Yeye yupo nyumbani anakaa na mama mkubwa ( step mother )

Sasa mimi ni Juzi tu nimemaliza chuo kwa mbinde sana mana nmejitegemea kila kitu miaka yote mitatu mpaka namaliza, sikuwa na wakumwelekezea shida zangu zozote ingawa kwa upande wa Baba tupo watoto 16 na sisi ndio wa mwisho na hawa ndugu zetu wote kila mtu ni mambo safi kweli ( kweli kutoa ni moyo 🥲)

Sasa huyu mdogo wangu kanitumia Hii meseji nimepatwa na stress sana wakati ni Juzi tu nmeongea na huyu mama mkubwa wangu tukakubaliana kuwa atampeleka mdogo wangu chuo ila ntakua nampa back up kwa vitu vidogo vidogo kama matumizi ya apa na pale.

Mimi saiv ndo nmeanza biashara bado hata sijafikia ile level ambayo nimejiwekea malengo nifikie lakini nakumbana na majukumu mazito kama haya.

Binafsi apa nilkua napambana nipate hela niingie Law school mwezi July lakini izo dalili naona kabisa zikififia🥲

Kinachoniuma ni mdogo wangu af ni mtoto wa kike na tumezaliwa wawili tu, Naombeni ushauri nifanye nini ili nijue namjibu vp huyu mdogo wangu in a positive way

View attachment 2469632
Pole ila huyo ni mdogo wako, ulitakiwa umsikilize kwanza shida yake ndio unaze msahihisha

Yaani hapo anaeza kua ametoa machozi

Pole sana na ujitahidi aende chuo.
 
Iyo ndo last option yangu chief, nikishindwa kupata njia nyingine ya yeye kwenda chuo sitosita kufanya ivyo mdogo wangu nayeye atimize ndoto zake
Duuh jitahidi uwe selfish kidogo

Kama bi mkubwa anauwezo basi kutakua labda mdogo ako na mama hawaelewani mwambie dogo ajirekebishe tabia

Nenda Law school asee
 
Mimi leo nimeamkia Hospitali mana Tangu Tarehe 2 najiskia hovyo nilzani ni hangover za pombe za sikukuu kumbe nilkua na Malaria.

Mimi mwandiko wako ndo utaniongoza nikujibu au nisikujibu.
Sipendi miandiko ya kitoto
Mi pia mtu akiandika x badala ya s sijibu msg labda apige nachukia huo utoto eti xaxa fck!!!!
 
  • Kicheko
Reactions: EEX
Nakubaliana nawewe mkuu japo nilishaomba Law School nikapangiwa Intake ya July na hela tayari ipo ila bado naifanyia mizunguko kwenye biashara.

Itabidi nifuatilie kama kuna consequences zozote za mimi kutoripoti Law School Mwaka huu ili nijue nafanyeje mana apa nina stress ata uwezo wa kufikiri umepungua
Ndio inabidi umfundishe hiyo biashara ili ukienda kusoma aiendeleze kisha ukishamaliza law school unakuja kumpokea kijiti na yeye anakwenda chuo.
Forget about Step mother,forget about step brothers wewe ni mtu mzima sasa yaani chukulia ndio umeshaanza majukumu hivyo wewe ndio kaka,wewe ndio baba,wewe ndio mjomba kwa huyo mdogo wako.
Hiyo changamoto yako ni ndogo sana maana huyo mdogo wako naye ni mtu mzima anafundishika kirahisi.
Mimi nilianza kusomesha wadogo zangu kuanzia primary level wakamaliza,sekondary baadhi wakamaliza na kuna mmoja bado anaendelea na sekondary,wengine walimaliza kwenda chuo na wengine wanahitaji kwenda chuo sasa hivi ila ninachoshukuru Mungu likitokea jambo la dharura au shughuli yeyote wananisaidia mawazo na usimamizi kwenye utekelezaji mimi natoa mchango wa kipesa.
So nina uzoefu mkubwa wa hili jambo ninalokushauri.

Sent from my SM-C7000 using JamiiForums mobile app
 
Duuh jitahidi uwe selfish kidogo

Kama bi mkubwa anauwezo basi kutakua labda mdogo ako na mama hawaelewani mwambie dogo ajirekebishe tabia

Nenda Law school asee
Bi mkubwa nimeongea nae juzi tu tena nilkuta 5 missed calls zake nikampigia tukasalimiana na nikamkumbushia kuhusu suala la mdogo wangu kwenda chuo akasema haina shida kabisa sasa leo yan sjui ata imekuaje na sielewi.

Napanga nikitoka Kwenye mishe zangu nimpigie nimsikilize anasemaje tena.
 
Pole ila huyo ni mdogo wako, ulitakiwa umsikilize kwanza shida yake ndio unaze msahihisha

Yaani hapo anaeza kua ametoa machozi

Pole sana na ujitahidi aende chuo.
Shukran sana kwa ushauri mkuu
ila suala la kumsahihisha kuhusu mwandiko anisamehe tu bure sina uvumilivu na ilo
 
Back
Top Bottom