Mimi naona huyo wa kwanza hamfai huyu binti, huyo wa pili nae naona hamfai kwa sababu:
Kwanza huyo wa pili kwa inavyoonekana amekaa na mke wake about 20 years! kwani mtoto wa kwanza ana miaka 19. Ina maana hata baada ya 20 years mke wake alishindwa kuvumilia tabia yake au kuizoea hiyo hali aliyokuwa nayo mume wake, ni ngumu kwa huyu binti kuja kuzoea hali hiyo, itafika wakati yeye pia ataona alikosea kumchagua!!
Pili huyo mume si mtanzania, huyu dada hajui vizuri mazingira ya huyu baba, hajui maisha yake ameishije, watu huwa tunajua tabia ya mtru kwa kuangalia pia marafiki zake, sasa inavyoonekana huyu dada hajui hata marafiki wa huyu baba, so ni wazi hajui tabia yake vizuri, kwa sababu amempenda ni rahisi kusema ana tabia njema kwa sasa!!!
tatu huyu dada 25 bado ni binti mdogo, akubali kwamba kuna tabia nyingine au vitu alivyotamani kufanya akiwa kama kijana hataviona kwa huyu baba, automatically mtu anapokuwa huwa kuna vitu vinabadilika, maqmbo alityokuwa akifanya kwenye late 20's siyo ndio atakayofanya kwenye late 40's.
Nne huyu baba sijui utamaduni wa kwao ulivyo, lakini anaweza ikafika wakati akamuona kama mwanae hivyo akahitaji heshima kama ambayo angeipata kwa watoto wake, ambayo si sawa, huyu atakuwa ni mke si mtoto.
BUT ALL IN ALL KAMA AMEPENDA AOLEWE, AKIPENDA HATA YAKIJA KUTOKEA HATAJUTA, SABABU ALIPENDA.