Naombeni msimamo wenu kwenye suala hili!

Naombeni msimamo wenu kwenye suala hili!

Mie mzima kabisa Kaka! Kumbe ndoa ni kuingia vitani ... bila shaka hukusahau kuvaa helmet kichwani na gobore mkononi kuikinga roho yako isitolewe kwa sababu ya mali mlizochuma! Kila la kheri Kaka!


Hahahah...ndoa hujumuish kuwajibika, nidhamu n.k ndio maana nimeshahabisha na vita....

Sikuwa na maana tofauti na hiyo hata ukafikiria mbali kuwa kuna habari za kutoana roho...

Amen kwa heri uliyonitakia...natumai nawe mambo mswano sasa eenh :becky:
 
labda mulete salary slip kama ni kuongea tu sidhan kama kuna atayesema ukweli!!! ila kwa wanawake wa kiafrica hasa wa kwetu hapa bongo thats the biggest mistake unayoweza fanya kama mwanaume kumwambia mkeo unachopata na hili tatizo linatokana na ukweli kwamba africa tuna extended family so kila cku mtakua mnagombana mbona husaidii ndugu zake!!!
 
Aisee, hayo ni mafundisho gani?

Mimi nifahamuvyo from my parents' experience ni kuwa wote wanafahamu kipato cha mwenzako. Nimeogopa sana mafundisho hayo aisee.

Mimi nadhani imekuwa precipitated na maisha ya siku hizi wanaume kutokuwa responsible and all that. Watu kuwa selfish.

Wakati nakuwa sikuwahi kusikia wazazi wangu wakiongelea kitu, "pesa yako" "pesa yangu" "chako" "changu" na yafananayo na hayo!
 
dada hakuna siri na haipaswi kuwepo siri yoyote kwa wanandoa coz wanajenga nyumba moja kwann wagombanie fito?
na hapo wanawake ndipo wanapokosea kuwa tegemezi kwa kila kitu ndo maana huwa wananyanyaswa kila kukicha ila km we ukaleta 1 na ye kaleta 1 vikawa viwili nadhani ndipo kuwe na ht haja ya kusema haki sawa kwa wote pale itakapobidi.
 
Habarini za leo ndugu zangu!

Jamani kuna suala hili nimekuwa nikijiuliza bila kupata usahihi au ubaya wake. Kwenye ndoa, eti ni lazima au sio lazima kumuonesha mwenzako kipato chako unachoingiza ili mpange wote matumizi yake?

Mimi binafsi niko wazi kwa mume wangu na huwa tunaoneshana vipato vyetu kwa ajili ya kupangilia matumizi.

Sasa kuna mama mmoja nilikutana naye ktk kitchen pati moja, akatoa mada kuwa ni marufuku mume kujua kipato cha mkewe kwa kuwa yeye ndiye mkuu wa familia basi anatakiwa kuprovide kwa ajili ya matumizi ya nyumbani na sio wewe km mke...hapo nikabaki kushangaa!

Na ktk scenario nyingine nikiwa kibaruani huku kuna kaka mmoja alishawahi kulalamika kuwa anamshangaa mkewe amemfungulia duka la vipodozi huko kariakoo na anafanya vzr tu kibiashara lakini kutwa ni kumbana mumewe ahudumie kila kitu huku yeye (mke) kipato chake hakiweki wazi na wala yeye mume mtu hajui mkewe anapeleka au anatumia vipi pesa zake.

Huu ni mkanganyiko kwangu! je ndugu zangu, hili mnalitazama vipi?

Karibuni tusaidiane kufumbuana macho na kuwekana sawa.

Kwenye mafundisho ya ndoa tulifundishwa kwamba, kipato cha mume na mke ni kipato cha familia. Mnakichanganya pamoja, mnapanga mipango ya pamoja. Ni dhambi kubwa kumficha mwenzi wako kipato chako. Maana hiyo haina tofauti na kutokuwa mwaminifu kwenye ndoa yako.

Watu wengi ambao wamepata maendeleo ya haraka wakiwa wanandoa wamekuwa hawafichani vipato vyao. Kipato kikiwa cha familia ni rahisi kupanga vipaumbele vyenu.
 
ni ukweli ndg yangu!!!
Kwenye mafundisho ya ndoa tulifundishwa kwamba, kipato cha mume na mke ni kipato cha familia. Mnakichanganya pamoja, mnapanga mipango ya pamoja. Ni dhambi kubwa kumficha mwenzi wako kipato chako. Maana hiyo haina tofauti na kutokuwa mwaminifu kwenye ndoa yako.

Watu wengi ambao wamepata maendeleo ya haraka wakiwa wanandoa wamekuwa hawafichani vipato vyao. Kipato kikiwa cha familia ni rahisi kupanga vipaumbele vyenu.
 
Mimi nilifundishwa hivi na wazazi wangu mwanaume lazima amhudumie mke wake kwa kila kitu, asiombe msada kwa mke wake ni aibu.

Hao wanao saidiwa na wake zao, sijaona kama wamefanikiwa zaidi ya kuambulia masimango.

Nawashukuru sana wazazi wangu kwa kunipa mwanga, kama wewe ni mwanaume bakia kuwa mwanaume, mwanaume haombi msada.
 
" Sharing is Caring " ...Lakini wataalamu wengine husema :- Mpende kama nduguyo, Na muhesabiane kama Mmehasimiana !!
 
^^
Si kila mafundisho yanafaa kujenga..linda familia yako.
Walimu wengi watakupa division five ya ndoa.
^^

ndo maana nakupendagaa kakaangu mwe!!



mafundisho gani ya kijinga hivyo.
kweli za kuambiwa changanya na zako
 
hii kweli changamoto..ndio mshaamua kuish pamoja (pengne mkawa hvyo hadi kufa) wewe unajtolea kila kitu mwenzio anafcha, sijui anamfchia kwanini na kwaajili ya nan. Mwanamke hvyo kudumu kwa ndoa yake kunamashaka as hata kisaikolojia anajiandaa (hata kabla ya mtafaruku wowote) kuish kivyake.
 
Back
Top Bottom