Naombeni msimamo wenu kwenye suala hili!

jamiif

JF-Expert Member
Joined
Apr 30, 2012
Posts
2,413
Reaction score
995
Habarini za leo ndugu zangu!

Jamani kuna suala hili nimekuwa nikijiuliza bila kupata usahihi au ubaya wake. Kwenye ndoa, eti ni lazima au sio lazima kumuonesha mwenzako kipato chako unachoingiza ili mpange wote matumizi yake?

Mimi binafsi niko wazi kwa mume wangu na huwa tunaoneshana vipato vyetu kwa ajili ya kupangilia matumizi.

Sasa kuna mama mmoja nilikutana naye ktk kitchen pati moja, akatoa mada kuwa ni marufuku mume kujua kipato cha mkewe kwa kuwa yeye ndiye mkuu wa familia basi anatakiwa kuprovide kwa ajili ya matumizi ya nyumbani na sio wewe km mke...hapo nikabaki kushangaa!

Na ktk scenario nyingine nikiwa kibaruani huku kuna kaka mmoja alishawahi kulalamika kuwa anamshangaa mkewe amemfungulia duka la vipodozi huko kariakoo na anafanya vzr tu kibiashara lakini kutwa ni kumbana mumewe ahudumie kila kitu huku yeye (mke) kipato chake hakiweki wazi na wala yeye mume mtu hajui mkewe anapeleka au anatumia vipi pesa zake.

Huu ni mkanganyiko kwangu! je ndugu zangu, hili mnalitazama vipi?

Karibuni tusaidiane kufumbuana macho na kuwekana sawa.
 
hata mie nalijua hilo, na ninailinda sana familia yangu tofauti na ulivyofikiria...sijatoa uzi huu kupata ushauri, NO! ni mada tu km mada nyingine ijadiliwe ili mtu aamue kufuata lipi kutokana na maisha yake as kila mtu hapa ana akili timamu!
^^
Si kila mafundisho yanafaa kujenga..linda familia yako.
Walimu wengi watakupa division five ya ndoa.
^^
 
hata mie nalijua hilo, na ninailinda sana familia yangu tofauti na ulivyofikiria...sijatoa uzi huu kupata ushauri, NO! ni mada tu km mada nyingine ijadiliwe ili mtu aamue kufuata lipi kutokana na maisha yake as kila mtu hapa ana akili timamu!

^^
Hata mimi nilikuelewa labda tu nimekosea kuchangia kwa kutumia nafsi..
La msingi ni kuwa kuna taratibu za ndoa fulani ukizileta kwenye ndoa nyingine hazijengi.
^^
 
ok, ila mpaka hapo hujesema kwa upande wako unalionaje hili suala...hujachangia tukajua unavyoona wewe ni aje...

Ndio maana niliamua kuoa Mchaga, baada ya mavuno kila kitu kinawekwa mezani...kinarudishwa tena kwenye investments.

Wale wenye mikono ya birika waache waendelee kuwa na mikono ya birika...
 
Si vyema kufichana vipato.....

Zote ziwekwe mezani zipangiwe matumizi na zitakazobaki either zihifadhiwe au zizungushwe kwenye miradi (kama ipo)
 
hata mie naona kuweka wazi vipato vyetu ni jambo jema kwa kweli kwani hurahisisha upangiliaji na maamuzi kuhusu matumizi na mipango yenu...
 
Hakuna formula kwenye ndoa. Wanaume wengine hawataki kabisa kusaidiwa chochote. Na wengine wanahitaji msaada ili ndoa iendelee. Cha maana hapa ni mtu binafsi kutenda sawasawa na ndoa yake inavyokwenda ili mradi wote mnakuwa wazi na mnafurahia maamuzi yenu. kwa mfano wewe jamiif unachangia na una amani kwenye ndoa yako endelea na usibadili. Ambaye hachangii na mumewe hamshauri anakwenda kuyaongelea ofisini ni tatizo la mume.
 
Last edited by a moderator:
ok, ila mpaka hapo hujesema kwa upande wako unalionaje hili suala...hujachangia tukajua unavyoona wewe ni aje...

^^
Naamini katika umoja wa mke na mume.
Kinyume chake kwangu ni ubinafsi.
^^
 
Ndio maana niliamua kuoa Mchaga, baada ya mavuno kila kitu kinawekwa mezani...kinarudishwa tena kwenye investments.

Wale wenye mikono ya birika waache waendelee kuwa na mikono ya birika...

Kaka hujambo? miss u sana. Ulioa kwa sababu ni Mchaga au ulimpenda na ikatokea kwamba ni mchaga?
 
sijaoa lakini kauli ya huyo mama ya kuficha kipato asijue mumeo ni ya "KIUFOOSARO" zaidi,what next ishu kama hizo zinaishiaga "KI MUSHILIZATION",
roho mbaya,u primitive wa baadhi ya wanawake(everything a man should provide) ni umbumbumbu!!na ni moja ya factor ya family instability-KIAFRIKA ZAIDI
 
well said mkuu hata mimi nilimshangaa sana, ila nikaona ok labda ndoa yake inahitaji hivyo na jinsi anavyoishi na mumewe ila kiukweli sikupenda...ndoa nijuavyo mimi ni kusaidiana pia.
sijaoa lakini kauli ya huyo mama ya kuficha kipato asijue mumeo ni ya "KIUFOOSARO" zaidi,what next ishu kama hizo zinaishiaga "KI MUSHILIZATION",
roho mbaya,u primitive wa baadhi ya wanawake(everything a man should provide) ni umbumbumbu!!na ni moja ya factor ya family instability-KIAFRIKA ZAIDI
 
Kaka hujambo? miss u sana. Ulioa kwa sababu ni Mchaga au ulimpenda na ikatokea kwamba ni mchaga?

Sijambo, habari ya masiku mengi?

Upendo hushinda yote, lakini matamanio ya moyo ni mwanzo wa furaha...

Nilitamani kuoa Mchaga na bahati nzuri nikapata Mchaga...

Unapotaka kuingia vitani ni lazima ujue unaenda kupambana na nani...

Pia ni lazima ukague silaha zako zote na ufanisi wake kwa ukubwa wa vita iliyopo...

Ndoa kwa upande mwingine ni vita haswa kama ukiweka mapenzi kando...

Usipokuwa makini ndoa inaweza kuwa chanzo cha umasikini au hata kupoteza kabisa muelekeo...

Hivyo awali ya yote inakupasa kuchagua mwenzi ambaye ataendana na vipaumbele karibia vyote...
 
jamiif kwanza niseme hujambo??
Binafsi nadhani 'mafundisho' mengi ya siku hzi kuhusu ndoa yako misguided
Jamii nyingi zinamfanya mwanamke kuwa tegemezi na hii hulka anakuwa nayo
Hataki kuchangia chochote kwenye ndoa simply she's a woman..
Tufike wakati vipato vijulikane vyote kwenye familia..
 
Last edited by a moderator:
sijambo ndg yangu! kiukweli hatya mimi sikupenda fundisho hilo maana inakuwa km vile unaolewa ili upone kimaisha kwa kumkamua mwenzako tu ambayo si kitu kizuri kama kweli unampenda mwenzako...upo sahihi sana ni kweli mafundisho mengi siku hizi ni kuvuruga badala ya kujenga..

Maisha ya NDOA ni kushirikiana..
Na kama mama una kipato kiweke wazi kijulikane..
Mambo haya ndo yanaleta shida sana..baadaye

sijambo ndg yangu! kiukweli hatya mimi sikupenda fundisho hilo maana inakuwa km vile unaolewa ili upone kimaisha kwa kumkamua mwenzako tu ambayo si kitu kizuri kama kweli unampenda mwenzako...upo sahihi sana ni kweli mafundisho mengi siku hizi ni kuvuruga badala ya kujenga..
 
Sijambo, habari ya masiku mengi?

Upendo hushinda yote, lakini matamanio ya moyo ni mwanzo wa furaha...

Nilitamani kuoa Mchaga na bahati nzuri nikapata Mchaga...

Unapotaka kuingia vitani ni lazima ujue unaenda kupambana na nani...

Pia ni lazima ukague silaha zako zote na ufanisi wake kwa ukubwa wa vita iliyopo...

Ndoa kwa upande mwingine ni vita haswa kama ukiweka mapenzi kando...

Usipokuwa makini ndoa inaweza kuwa chanzo cha umasikini au hata kupoteza kabisa muelekeo...

Hivyo awali ya yote inakupasa kuchagua mwenzi ambaye ataendana na vipaumbele karibia vyote...

Mie mzima kabisa Kaka! Kumbe ndoa ni kuingia vitani ... bila shaka hukusahau kuvaa helmet kichwani na gobore mkononi kuikinga roho yako isitolewe kwa sababu ya mali mlizochuma! Kila la kheri Kaka!
 
Back
Top Bottom