Naombeni msaada wa kumuelewa huyu binti

Naombeni msaada wa kumuelewa huyu binti

habari zenu wadau na poleni kwa kuwavamia asubuhi km hii. ni member mpya lkn ni mdau wa miaka mingi humu.....natembelea si chini ya mara tano kwa siku na kwa miaka mingi.

kwenye mada!
kuna binti nilibahatika kuwa kwenye mahusiano nae (nimemzidi 15 yrs--msishangae. yeye ni 20 lkn kalikuwa na ujasiri wa kuniface). baada ya mwezi mmoja akawa anforce ndoa. kwakuwa ni kama vile sikuwa nimejiandaa vizuri (kiakili) kwa hilo nikamwambia nitamjibu kuhusu hilo. ikawa kila ikipita wiki anaulizia suala hilo hilo nami jibu langu likabaki vilevile. baada ya miezi mitatu mahusiano kati yetu yakakatika. akaja kunitafuta tena baada ya miezi miwili na namba mpya huku akiniambia kuwa yuko Dar, tukawa tunachati. kama kawa, nikajisikia kumwita lkn safari hii akawa anapiga sana chenga flani hivi. wakati huohuo, kwa upande wangu, fikra za kufanya kweli kindoa zikawa zinanijia kwa kasi sasa maana niliona inawezekana ndo nimeletewa huyu. nilipojaribu kumgusia hilo akawa nalo hafunguki sawasawa.....mara nataka, mara sitaki. nikaazimia kumpotezea, ajabu nikashangaa taratibu safari hii moyo unagoma (haya mapenzi acha tu).

siku zikapita huku hali ya kuchati ikiendelea kati yetu kwa miezi mitatu mfululizo huku hatujaonana. mwezi wa sita nikapata safari ya kwenda Dar na nikamtaarifu kuwa nitakuwa huko nae akasema tutaonana tu. Mungu si Athumani, siku mbili kabla sijaenda nilikutana na mwanakijiji mwenzie na ktk stori za hapa na pale nikamtosea habari za huyo binti km anamjua au la. jibu alilonipa ndilo lilipelekea hadi kufikia kuandika hii thread. aliniambia kuwa huyo binti kwa sasa ni mchumba wa mtu na kwamba mwezi wa sita wanafunga ndoa. nilimchukulia kawaida sana huyu binti na hata hakuwa akisumbua akili sana, lkn baada ya habari hiyo tu sijui kimetokea kitu gani.....yaani ameniganda akilini na moyoni mpaka najihurumia maana nakosa raha, amani na wakati mwingine najitukana mimi mwnyw kwa uzembe nilioufanya pale mwanzo (jamani, love her when you have her).

sikumwambia kabla yule binti niliamua nione km nitamwona huko basi atanieleza hukohuko. tarehe ya kusafiri ilifika na ni kweli yule binti alikuja buguruni nilikofikia....kimuonekano ni kweli alionekena amechorwa flani hv mikononi na simu yake hakuja nayo. tukaongea na kufanya yetu huku namcheki tu nikisubiri muda nimpasulie. ajabu ni kuwa alikuwa anachunguza mpaka simu yangu. nikamwacha tu. baadae nikaamua tu nimueleze yote na kumlaumu kuwa alichofanya sio chema kwa usalama wangu, wake na mustakabali wa maisha yangu mimi maana kuna nilioamua kuwapotezea kwa kumuamini yeye. alilia sana na kukiri kuwa hizo taarifa ni kweli na aliamua hvyo baada ya kuona kuwa sina uelekeo wowote wa kumuoa na kwmb hakuniambia kwa vile aliona km atakuwa amenikashfu lkn kwakuwa nimegundua mwenyewe bs hana pa kutokea.iliniudhi lkn hakukuwa na namna, tukaaagana.usiku tukaongea mpaka ikafikia akaniambia km vp irudishwe mahali ili arudi kwangu, baadae, ht kabla sijajibu(na sikuona mantiki) akaliondoa wazo. sikumshawishi aongee hivyo ht kidogo. nilichokuja kugundua baadae ni kuwa bwana'ake ana umri karibia na wangu lkn ye ni tajiri sana....milionea kwn ana uwekezaji wa kutosha kbs wa mashamba na biashara mbalimbali ktk miji mbalimbali ikiwemo morogoro, lindi n.k. kiufupi yuko vizuri kwelikweli.....na huyo binti anaenda kuwa mke wa 3, kwan wawili wapo tayari. jana, naambiwa mmoja ameshaachwa kwa ajili ya kumpisha huyu binti.....anaolewa mwezi huu kwani ule wa sita ilighailishwa.

cha ajabu (hatari), huyu binti mawasiliano na mimi mpaka sasa hayajakata, nami najikuta siyakati pia....kila nikimshauri tuache ananipa moyo nisiwe na wasiwasi. nina akili na busara zangu na najua si jema, lkn ht sielewi imekuaje mpaka sasa imekuwa hv. isitoshe, mi nawaogopa sana watu wenye fedha.kila siku lazima tuwasiliane mpaka usiku wa manae mpaka najiuliza kulikoni huko au ndo hali itabadilika baada ya kuolewa? nina mpenzi mpya ambaye najaribu kumuandaa awe mchumba maana huyu si wangu tena, namhurumia mno maana simuwazii kbs akili yote imehamia kwa huyu binti ni namna gn nimemkosa. wa sasa kiukweli ni mzuri kuliko huyo binti.

nilenda bagamoyo hv karibuni, nikamuomba tuonane lkn ilishindikana.....kuna sababu kadhaa alizitoa nami kwakuwa ni mwizi tu nikaamua kuzipokea ht km zina walakini.

kuna maswali kadhaa najiuliza mnaweza kunisaidia;
1. kwanini alinificha kuwa ana mchumba?
2. kwanini haachi kuwasiliana nami wakati huohuo haonekani kufanya jitihada za dhati kuonana?
3. jana kaniomba 20k anasema kuna mambo anataka kuyafanya (nahisi ni maandalizi ya harusi, probably, uandaaji wa kadi). nilipomtania kuwa naona ni maandalizi ya ndoa, amekataa katakata mpaka nashangaa tatizo ni nini. pia, anapata hela yoyote anayohitaji kutoka kwa mumewe, kwanini aniombe mimi wakati kwa sasa sina maana yoyote ile kwake (ht kuonana ni hiyo mara moja tu basi kwa mwaka huu)?
4. km hanipendi kwanini ananitafuta na hataki uache kuwasiliana?
5. km ananipenda kwanini ananipiga chenga wakati mwingine?yupoje huyu?


ameniambia tarehe 15 mwezi huu kuna kitu anataka kuniambia, nahisi itakuwa ni kuhusu kuolewa kwake na namna gani napaswa kupotea....bila shaka. natamani kupotea kabisa kabla sijasikia the worst tarehe hiyo!!!!

ushauri tafadhali
issue ndogo sana hii
 
kweli mtihani huu ila jaribu kuwa na maamuzi maana mtaka mengi kwa pupa? basi fikiri katika hilo
 
Mkuu ruhusu aolewe na huyo tajiri then tumia ukaribu wake na wewe kujipatia kipato cha kuanza biashara..

Maana kama amekuwa akisumbua hisia zako ,fanya na wewe kusumbua hisia zake then na wewe uje oa mchumba wako mpya
 
kama umemzidi 15yrs na yeye ana 20...ina maana una 35 yrs. Hivi mkuu, kweli huo umri ni wa kuchanganywa na mapenzi kiasi hicho mpaka unaomba ushauri???

Jitafakari bwana kuna mambo mengi ya maana ya kuomba ushauri, hilo liko ndani ya uwezo wako kuliweka sawa.
 
Bro una miaka 35 lakini akil ya mtoto wa miaka 18.

Ushaambiwa binti ana mchumba anaolewa mwezi wa 6, so achana naye maana atakuwa mke wa mtu hv karibuni. Wasichana wamejaa kibao relax utapata wa kumuoa.
 
me hapo kwenye hyo 20k tu alaf ana bwana tajir [emoji3][emoji3] wewee me sitoi kitu,,na me nasubr tareh 15 nitoe mrejesho wang hvhv bado sijaelewa kwa kwel!!
 
Pole ila kwakifupi huyo bint ukumpenda nahata kama ulimpenda basi ulimdharau kwasababu kwawakati huo alikuwa available ila kwasababu kwasasa ni unavailable ndio unahisi kumuhitaji. Kinachokusumbua kwasasa niroho ya kwanini wewe umkose naunajihisi kama mjinga fulani ila chukulia kawaida mkuu. Alikuja kukuonjesha ili ujue huo utamu ambao wewe uliuchukulia kawaida Kuna mwenzako kauchukulia umakini wahali yajuu nandiomana kaamua aoe kabisa, RELAX Mkuu
 
Pole ila kwakifupi huyo bint ukumpenda nahata kama ulimpenda basi ulimdharau kwasababu kwawakati huo alikuwa available ila kwasababu kwasasa ni unavailable ndio unahisi kumuhitaji. Kinachokusumbua kwasasa niroho ya kwanini wewe umkose naunajihisi kama mjinga fulani ila chukulia kawaida mkuu. Alikuja kukuonjesha ili ujue huo utamu ambao wewe uliuchukulia kawaida Kuna mwenzako kauchukulia umakini wahali yajuu nandiomana kaamua aoe kabisa, RELAX Mkuu
kiukweli upo sahihi kabisa mkuu.....sahihi kabisa. ahsante sn. najitahidi kuliacha.
 
Kuna watu wengine huwa wanakua umri tu....we jamaa ni mtoto na ni mpuuzi kuliko huyo mtoto wako,nakushauri tu jizoeze kutembea na vilainishi maana ushajitoa akili kung'ang'ania mtoto ambaye hata uelekeo wa maisha yake haujui.
nimeipata point yako, ingawa umeitoa kwa ukali sn. thanx
 
Mkuu,subiri hiyo tarehe 15 atakupa majibu yako yote....usisahau kumuuliza sasa
ahsante Joanah, lkn nimeamua yaishe ht kabla ya hiyo tarehe nisije kuongeza maumivu bure
 
me hapo kwenye hyo 20k tu alaf ana bwana tajir [emoji3][emoji3] wewee me sitoi kitu,,na me nasubr tareh 15 nitoe mrejesho wang hvhv bado sijaelewa kwa kwel!!
hata mi pamenishangaza sana hapo. sijui ana maana gn huyu
 
Mkuu ruhusu aolewe na huyo tajiri then tumia ukaribu wake na wewe kujipatia kipato cha kuanza biashara..

Maana kama amekuwa akisumbua hisia zako ,fanya na wewe kusumbua hisia zake then na wewe uje oa mchumba wako mpya
poa mkuu lkn kuachana nae nafikiri ni bora zaidi
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom