Naombeni msaada wa kumuelewa huyu binti

Naombeni msaada wa kumuelewa huyu binti

NIMEONA

JF-Expert Member
Joined
Aug 4, 2019
Posts
3,854
Reaction score
5,714
Habari zenu wadau na poleni kwa kuwavamia asubuhi km hii. ni member mpya lkn ni mdau wa miaka mingi humu natembelea si chini ya mara tano kwa siku na kwa miaka mingi.

kwenye mada!
kuna binti nilibahatika kuwa kwenye mahusiano nae (nimemzidi 15 yrs--msishangae. Yeye ni 20 lkn kalikuwa na ujasiri wa kuniface). Baada ya mwezi mmoja akawa anforce ndoa. Kwakuwa ni kama vile sikuwa nimejiandaa vizuri (kiakili) kwa hilo nikamwambia nitamjibu kuhusu hilo. Ikawa kila ikipita wiki anaulizia suala hilo hilo nami jibu langu likabaki vilevile. baada ya miezi mitatu mahusiano kati yetu yakakatika. Akaja kunitafuta tena baada ya miezi miwili na namba mpya huku akiniambia kuwa yuko Dar, tukawa tunachati. Kama kawa, nikajisikia kumwita lkn safari hii akawa anapiga sana chenga flani hivi. wakati huohuo, kwa upande wangu, fikra za kufanya kweli kindoa zikawa zinanijia kwa kasi sasa maana niliona inawezekana ndo nimeletewa huyu. Nilipojaribu kumgusia hilo akawa nalo hafunguki sawasawa. Mara nataka, mara sitaki. nikaazimia kumpotezea, ajabu nikashangaa taratibu safari hii moyo unagoma (haya mapenzi acha tu).

Siku zikapita huku hali ya kuchati ikiendelea kati yetu kwa miezi mitatu mfululizo huku hatujaonana. mwezi wa sita nikapata safari ya kwenda Dar na nikamtaarifu kuwa nitakuwa huko nae akasema tutaonana tu. Mungu si Athumani, siku mbili kabla sijaenda nilikutana na mwanakijiji mwenzie na ktk stori za hapa na pale nikamtosea habari za huyo binti km anamjua au la. jibu alilonipa ndilo lilipelekea hadi kufikia kuandika hii thread. aliniambia kuwa huyo binti kwa sasa ni mchumba wa mtu na kwamba mwezi wa sita wanafunga ndoa. nilimchukulia kawaida sana huyu binti na hata hakuwa akisumbua akili sana, lkn baada ya habari hiyo tu sijui kimetokea kitu gani.....yaani ameniganda akilini na moyoni mpaka najihurumia maana nakosa raha, amani na wakati mwingine najitukana mimi mwnyw kwa uzembe nilioufanya pale mwanzo (jamani, love her when you have her).

sikumwambia kabla yule binti niliamua nione km nitamwona huko basi atanieleza hukohuko. tarehe ya kusafiri ilifika na ni kweli yule binti alikuja buguruni nilikofikia....kimuonekano ni kweli alionekena amechorwa flani hv mikononi na simu yake hakuja nayo. tukaongea na kufanya yetu huku namcheki tu nikisubiri muda nimpasulie. ajabu ni kuwa alikuwa anachunguza mpaka simu yangu. nikamwacha tu. baadae nikaamua tu nimueleze yote na kumlaumu kuwa alichofanya sio chema kwa usalama wangu, wake na mustakabali wa maisha yangu mimi maana kuna nilioamua kuwapotezea kwa kumuamini yeye. alilia sana na kukiri kuwa hizo taarifa ni kweli na aliamua hvyo baada ya kuona kuwa sina uelekeo wowote wa kumuoa na kwmb hakuniambia kwa vile aliona km atakuwa amenikashfu lkn kwakuwa nimegundua mwenyewe bs hana pa kutokea.iliniudhi lkn hakukuwa na namna, tukaaagana.usiku tukaongea mpaka ikafikia akaniambia km vp irudishwe mahali ili arudi kwangu, baadae, ht kabla sijajibu(na sikuona mantiki) akaliondoa wazo. sikumshawishi aongee hivyo ht kidogo. nilichokuja kugundua baadae ni kuwa bwana'ake ana umri karibia na wangu lkn ye ni tajiri sana....milionea kwn ana uwekezaji wa kutosha kbs wa mashamba na biashara mbalimbali ktk miji mbalimbali ikiwemo morogoro, lindi n.k. kiufupi yuko vizuri kwelikweli.....na huyo binti anaenda kuwa mke wa 3, kwan wawili wapo tayari. jana, naambiwa mmoja ameshaachwa kwa ajili ya kumpisha huyu binti.....anaolewa mwezi huu kwani ule wa sita ilighailishwa.

cha ajabu (hatari), huyu binti mawasiliano na mimi mpaka sasa hayajakata, nami najikuta siyakati pia....kila nikimshauri tuache ananipa moyo nisiwe na wasiwasi. nina akili na busara zangu na najua si jema, lkn ht sielewi imekuaje mpaka sasa imekuwa hv. isitoshe, mi nawaogopa sana watu wenye fedha.kila siku lazima tuwasiliane mpaka usiku wa manae mpaka najiuliza kulikoni huko au ndo hali itabadilika baada ya kuolewa? nina mpenzi mpya ambaye najaribu kumuandaa awe mchumba maana huyu si wangu tena, namhurumia mno maana simuwazii kbs akili yote imehamia kwa huyu binti ni namna gn nimemkosa. wa sasa kiukweli ni mzuri kuliko huyo binti.

nilenda bagamoyo hv karibuni, nikamuomba tuonane lkn ilishindikana.....kuna sababu kadhaa alizitoa nami kwakuwa ni mwizi tu nikaamua kuzipokea ht km zina walakini.

kuna maswali kadhaa najiuliza mnaweza kunisaidia;
1. kwanini alinificha kuwa ana mchumba?
2. kwanini haachi kuwasiliana nami wakati huohuo haonekani kufanya jitihada za dhati kuonana?
3. jana kaniomba 20k anasema kuna mambo anataka kuyafanya (nahisi ni maandalizi ya harusi, probably, uandaaji wa kadi). nilipomtania kuwa naona ni maandalizi ya ndoa, amekataa katakata mpaka nashangaa tatizo ni nini. pia, anapata hela yoyote anayohitaji kutoka kwa mumewe, kwanini aniombe mimi wakati kwa sasa sina maana yoyote ile kwake (ht kuonana ni hiyo mara moja tu basi kwa mwaka huu)?
4. km hanipendi kwanini ananitafuta na hataki uache kuwasiliana?
5. km ananipenda kwanini ananipiga chenga wakati mwingine?yupoje huyu?


Ameniambia tarehe 15 mwezi huu kuna kitu anataka kuniambia, nahisi itakuwa ni kuhusu kuolewa kwake na namna gani napaswa kupotea....bila shaka. natamani kupotea kabisa kabla sijasikia the worst tarehe hiyo!!!!

ushauri tafadhali
 
Subiri kwanza, umsikilize hiyo tarehe 15 atakueleza jambo gani. Lakini ni vyema ukajiandaa kisaikolojia mkuu wake za watu wanaua. Usishangae akakwambia ana kiumbe chako.
 
Mi sijaona sababu ya maswali yako wala kumuwazia huyo binti.
a) Umeshasema una mchumba mzuri kuliko yeye na ulishasema binti alikupotezea baada ya wewe kuzingua mwanzoni. Do you really want to miss another girl???? Uje ufungue uzi mwingine mrefu hivi??? Give us a break - pambana na mchumba mpya.

b) Unajua wazi kutokana na stori nyingi sana kuwa Nothing good is going to happen when you have an affair with another mans wife! Especially when he is loaded. Unasubiri nini hapo????
 
Haihitaji elimu hata ya cheti kumuelewa hapo unasubiri nini kuachana nae?
 
Kuna watu wengine huwa wanakua umri tu....we jamaa ni mtoto na ni mpuuzi kuliko huyo mtoto wako,nakushauri tu jizoeze kutembea na vilainishi maana ushajitoa akili kung'ang'ania mtoto ambaye hata uelekeo wa maisha yake haujui.
 
Mi sijaona sababu ya maswali yako wala kumuwazia huyo binti.
a) Umeshasema una mchumba mzuri kuliko yeye na ulishasema binti alikupotezea baada ya wewe kuzingua mwanzoni. Do you really want to miss another girl???? Uje ufungue uzi mwingine mrefu hivi??? Give us a break - pambana na mchumba mpya.

b) Unajua wazi kutokana na stori nyingi sana kuwa Nothing good is going to happen when you have an affair with another mans wife! Especially when he is loaded. Unasubiri nini hapo????
Hata Mimi nimewaza hvyo mkuu.
Na kingine pia Cha kuongezea Ni kwamba huyo binti inaonekana alikuwa na haraka ya ndoa kwa hyo alivyoona jamaa haeleweki akatafuta mtu mwingine mbadala.
Kwa maana nyingine tunasema binti akili yake ya maisha ilitangulia mbele zaidi ya jamaa.
Hizo situations zilinikuta sana miaka ya nyuma lkn mwisho wa siku nikaja kuoa mke niliyepangiwa na mungu.
 
Iyo 20k ni yakazi gani we MPE tu, kikubwwa mwache aolewe we utakua unapiga pesa tu
 
Back
Top Bottom