Naombeni msaada nimetapeliwa

Ilinitokeaga hii kitu mwaka 2015 sinza kumekucha,jamaa aliniuzia gx 100 alilokopea bank,bahat nzur niliwahi kwenda police mabatini baada ya kwenda TRA kubadili jina,ukumbuke hapo biashara ilifanyika bar nikapewa card ingine lkn ukiitizama ni og! Sasa cjui alitengenezea wap! Nlimsweka ndani dalali akaonesha ushirikiano,jamaa aliplan kwenda police kudai gar yake haipo af wakinilengesha naonekana mwiz,ilichukua miez 4 lakin haki yangu niliipata! Jamaa hatakaa anisahau kwa nlichomfanyia!!
 
Nimeuza na kununua magari sana, sijawahi kutapeli wala kutapeliwa! Niko Nzega narudi Dar nimeleta Coaster nimemnunulia Mteja wangu! Sijaelewa ameibiwaje!

Mwaka huu mwezi wa Tisa nilikua nauza Rav Four Killitime! Nikapokea simu kutoka kwa jamaa mmoja akijitambulisha kuwa yuko Mwanza! Ameipenda gari na kwamba anaomba kuna MTU ataniunganisha nae ili aikague wakati yeye anakuja kwa ndege!

Baada ya muda kidogo nikapata simu kutoka kwa MTU akiniambia kuwa amejulishwa kuwa nauza gari na hivyo nimpelekee pale Toroka Uje, jirani na Best bite! Akasema ataweka mafuta, nikasema sawa!

Kufika eneo husika, nikampigia simu jamaa. Akaniambia anakuja, akaniambia yuko jirani kidogo, ghafla akaja kijana mmoja hivi, yaani naongea na yule jamaa anasema yuko jirani lakini anakuja namuona kijana mwingine anakuja, amefika akafungua mlango, vipi? Akasema ndio nimekuja kuiona gari, duh! Nikastuka kidogo, kijana yuko very smart! Bahati mbaya sana sana wakati anakaribia gari kuna signal alitoa kwa MTU ambaye alikua mita kadhaa nyuma ya gari, na nilijua kwa sababu wakati anakaribia gari kwa mbele nilikua namuangalia!

Nikacheki kwenye side mirror, nikamuona kweli mtu anakuja! Kwahio nikawa standby, wakaniambia wakague nikasema poa! Tukasogea chini ya mwembe jirani na pale eneo lilikua tulivu sana! Ghafla wakaja jamaa wengine wawili wamevaa Kaunda suit, wakakagua gari wakaniambia wanataka kuitest kwa kuendesha nikasema okay!

Nikajitoa mhanga, nikamjulisha faster ndugu yangu alikua Mwenge, akaanza safari kunifuata, nikaingia kwenye gari nikashusha Laptop yangu, nikabaki pale na jamaa wawili wengine wawili wakaondoka!

Dah, baada ya muda wakarudi! Hata sikuamini, nikachukua gari nikaondoka! Ila I am sure wale jamaa hawakua Wateja! Walikua na jambo lingine.
 
Ukiona watu wamekaa baa mchana siku zakazi na maji makuubwa ambayo hayaishi huku wakiongea na simu masaa yote uwe makini Sana kama unabiashara nao. Wengi niwapigaji
Majambaz kabisa
 
Dah unabahati mkuu
 
Nimecheka mpaka wapita njia wananishangaa.
 
Usirudie ujinga huo tena.
 
Hapo ndo ulipopigiwa sasa.
Huwa mkifika Dar mnaamini watu wanaoongea lugha yenu ni wastaarab kama uliowaacha kijijini,ila ujue watu wa miji mikubwa hasa Dar,wamepinda si watu wa kuamini hata kama amepewa ukasisi!
Sidhani sababu kuna nyingine alikuwa anaongea hadi kikabila
 
Pole sana...

Sijui ulijichanganya vipi mpaka kutapeliwa, tena gari...


Cc: mahondaw
 
Ujinga alianza nao yeye.Huwezi kupost picha za watu halafu unasema wamenitapeli bila kueleza kidogo ilikuwaje.
Mimi binafsi naona ni kiki tu ya watu wa bongo muvi!

Huyu mtu hayuko serious na huenda ameanzisha hii thread ili watu wafanye mzaha tu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…