Naombeni msaada kurudi bongo

Naombeni msaada kurudi bongo

Aisee umenikumbusha bro mmoja alienda ugiriki lakini alivyorudi alirudi hana hata begi la nguo..nguo alizitia kwenye Rambo..

1800usd ni hela ya mboga tu ya siku chache..Ni bora uendelee kubaki huko..
 
Mkuu, pole sana ila usikate tamaa jipange na uendelee kupiga box kwa angalau miaka mingine 5 au 10.

Je umeoa na una familia?

Kama jibu ni ndio basi ongeza kazi hiyo miaka 10 kwa ajili ya pensheni yako ya uzeeni kwenye kamradi ukirudi TZ.

Pia kama una familia na nyumba haipo, basi chukua bima ya kama Euro 200000 hivi ili iwasaidie endapo utaaga dunia.

Watoto wa kiafika huko ughaibuni wakifika miaka 16 tu wanaanza kuwakoromea wazazi wao kwa kuwahoji kwamba kwanini wao ni maskini, hiyo inauma sana maana huwezi kuchapa viboko.

Kuwa wale wazazi ambao hutumia ile fedha ya watoto ya kila wiki badala ya kuwawekea akiba.

Na kama waishi kihalali huko majuu basi angalau utakuwa umewekeza kwenye mafao yao wazungu angalau kila wiki utakuwa na mshiko kidogo.

Mimi nimeishi huko kama wewe lakini nilipofika miaka 35 nikasoma alama za nyakati na sasa nashukuru Mungu namudu maisha ya pande zote.

Nilikuwa nikirudi bongo kuangalia wapi niweke kitega uchumi na imesaidia sana.

Ila hujachelewa, piga box angalau miaka 5 kama si 10 ili upate chochote kamtaji kuweka kitega uchumi ambacho ukiamua kurudi kimoja utakuwa wasimamia wewe mwenyewe.

Kuwa twarudi nyumbani mara kwa mara kunasaidia sana kupata mawazo mbadala na yale ya kupiga boksi tuu kutwa kucha.
Mkuu Samahani, hivi """Kubeba box""" ndo kufanyaje??? Nasikia sikia hili neno...ila sijajua lina maana gani?
 
Kwanza huko ulipo unafanya kazi gani ? Usikimbilie hapa Bongo Vyuma vimekaza sana ndio Slogan ya Mujini
 
Hakuna unachoweza kufanya bongo kwa hiyo 1800 kama hauna lolote.....


Na kwa maelezo ya mtoa mada anataka aishi anavyoishi ughaibuni.

Kama ni mimi ningeamua nifie hapo alipo na hata wanaonijua wqsijue kisa cha kufariki kwangu.

Huu pia ushauri mzuri
 
Hahaha...mkuu kwa hizo dola 1800 nenda upareni kapange chumba cha elfu 20 kwa mwezi then lima mboga mboga kwenye shamba ulilo nunua eka moja laki 5...Lima mboga mboga ili upate chakula ukikosa ugali utakula mboga zako. Hamna namna hata kusafiri kwenda same na Moshi inabidi uombe lifti mkuu maana ukitumia hiyo ela yako kulipa nauli za mizunguko tutakuzika mapema maana utakufa kwa pressure.
 
1800 au 18,000?? Kama ni 1800 huwezi kuishi unavyotaka
Over
 
Labda tujifunze kwenye hili,ukiondoka maintains contact na bongo,Ila simshangai ukiwa ughaibuni na una familia halafu huna kazi proffesional ni vigumu sana kusave pesa...anyway uko ughaibuni ya wapi unialike...
Tehteh...Rebeca bhana...

Jirani yako...Weekend nyingine karibu
 
Mkuu Samahani, hivi """Kubeba box""" ndo kufanyaje??? Nasikia sikia hili neno...ila sijajua lina maana gani?

Kufanya kazi za kibarua ukiwa ughaibuni kwenye mabohari viwandani, kwenye ujenzi na kwingine kwaitwa kupiga boksi.

Kwenye mabohari kama Amazon, unakuwa na ujuzi wote wa kutumia mitambo ya kisasa ya aina zote, khasa chombo cha forklift ambacho ni lazima uwe mtaalam wa "counter balance".

Kuna vyombo vingine kama scissor lift, Gennie na spider crane ambazo hutakiwa kutumia akili kuviendesha.
 
Habari wana jf.
Mimi ni mbongo ambaye nipo ughaibuni tangu 1992 na sijawahi kurudi bongo. Nilikuja huku kutafuta maisha na kusoma, lakini kutokana na gharama za maisha na gharama za elimu sikuweza kusoma. Sasa nina miaka 51 na natamani kurudi bongo. Elimu yangu ni ya form 4 ya pugu secondari 1988. Benki nina dola 1800 tuu. Jee naweza kurudi bongo na kuishi comfortably? Yaani kunywa maziwa, kulala pazuri, kutotumia madaradara kwa usafiri, kula chakula nzuri (siyo kula nafaka).
Kuna fursa gani huko kwa wazee kama mimi?
Naombeni msaada wenu
That's peanut bro,komaa tu na kuendesha madaladala huko huko.
 
Labda tujifunze kwenye hili,ukiondoka maintains contact na bongo,Ila simshangai ukiwa ughaibuni na una familia halafu huna kazi proffesional ni vigumu sana kusave pesa...anyway uko ughaibuni ya wapi unialike...😊😊😊😉😉

Becky,

Kuweka akiba kunategemea kipato cha baba na mama ingawa mama hufanya kazi kiasi kutokana na majukumu ya ulezi.

Sasa baba kama hupati angalau euro 2000 kwa mwezi hiyo ni shida kidogo.
 
Back
Top Bottom