Naombeni msaada juu ya tablet yangu kuingia maji

Hechinodemata

JF-Expert Member
Sep 16, 2016
1,483
3,321
Habarini za asubuhi wapendwa, kwa atakayeguswa naomba anijuze kama ana technique yoyote.

Kwa ufupi simu yangu (tecno tablet imeingia maji) inawaka na kuzima inaniumiza kichwa coz bado mpya na nimejikusanya kwa muda mrefu nikaweza kununua ili angalau na mimi niende na wakati, yeyote anajua cha kufanya simu inapoingia maji ili angalau irudi katika hali yake ya kawaida japo sio 100% naomba anipe maujanja, kila nikiwasha inawaka na kuzima,
msaada wandugu
 
Chukua mchele kama kilo moja hivi mkavu iweke tablet yako ndani ya huo mchele kwa robo saa au nusu saa kisha itoe uiangalie kama bado ina tatizo.
 
Ilitakiwa afanye mapema aweke kwa mchele kabla hajashinda siku nzima anawasha na kuizima.. sijui ka itakuwa nzima kweli
 
Nenda posta mpya, kuna jengo la IPS ghorofa la 3 kamuone mtaalamu wa mambo ya simu na tablet, laptop n.k anaitwa fundi beka. Lazima itawaka tu trust me,
N.B - hawataki vifaa feki wanatengeneza vifaa orijino tu.
 
Ndani ya lile jengo lenye ofisi za Baraza la michezo taifa? nadhani floor ya Juu kabisa
 
Habarini za asubuhi wapendwa, kwa atakayeguswa naomba anijuze kama ana technique yoyote.

Kwa ufupi simu yangu (tecno tablet imeingia maji) inawaka na kuzima inaniumiza kichwa coz bado mpya na nimejikusanya kwa muda mrefu nikaweza kununua ili angalau na mimi niende na wakati, yeyote anajua cha kufanya simu inapoingia maji ili angalau irudi katika hali yake ya kawaida japo sio 100% naomba anipe maujanja, kila nikiwasha inawaka na kuzima,
msaada wandugu
simu ikiingia maji inatakiwa uipeleke kwa fundi mapema jinsi inavyokaa na maji ama ukungu ita short haitapona tena
 
Ndani ya lile jengo lenye ofisi za Baraza la michezo taifa? nadhani floor ya Juu kabisa
Ndio mkuu,
Ni floor ya kabisa, ni fundi mzuri sana nina muelewa binafsi ameshanitengenezea vifaa vingi vilivyo haribika ila orijino ( o.g )
 
Mtafute huyu jamaa anapatikana pale mavuno house posta karibu na Jengo la IPS 0717956685.
 
asanteni wote kwa mchango wenu wa mawazo, asubuh niliiweka kwenye mchele, nimeitoa jioni hii imewaka ila kioo kinaukungu kwa ndani
 
Hakikia jamii forum ni jamii sahihi kwangu, humu kuna wataalam mbalimbali waliovaa fake ID, TABLET yangu imepona na ule ukungu wa maji unaendelea kupungua,
 
Back
Top Bottom