Nahitaji Msaada Kwenye Hizi Cellular Networks (4G, 3G, H+, H , E, n.k)

GenuineMan

JF-Expert Member
Jun 13, 2017
5,251
11,598
Wasaalam,

Naomba kupewa ufafanuzi (wakitaalamu) kidogo.
Nimepatwa na Changamoto kwenye matumizi yangu ya Simu hasa upande wa internet.

Siku zote huwa nikitumia internet, huwa napata kwa 4G. Vizuri tuu.

Shida imekuja siku kama tatu kufikia leo, Nikiwa niko Chumbani kwangu. Nikiwasha data Network inasoma E" (Edge) badala ya ile 4G ya siku zote..

Ila nikitoka Chumbani, mita chache tuu naanza kuipata 4G japo kwa shida kidogo.

Na kama mnavyojua kwa zama hizi "E" haina nguvu kabisa hata ya kuruhusu sms za whatsaap. Kwahiyo imekuwa changamoto.

Nimejaribu kuangalia kwenye network settings za simu, kila kitu kiko sawa, kwa ufahamu wangu.

Nimewasiliana na internet provider(Tigo), hawana msaada wowote.

Naomba msaada, kwanza nini nifanye ile hali irudi kama kawaida
na pili tatizo ni nin? kama ni network kushuka, kwanini ishuke Chumbani kwangu tuu, ila nikizunguka dirishani network ipo?

Muhimu.
Natumia smartphone
Laini ni Tigo.
Niko Mjini.
Nina bando angalau la kutosha.

Asanteni na Karibuni..
 
Huwa mkuu network inatembea vizuri kama kukiwa hakuna kitu kinaziba ziba, kama kuna jengo refu limejengwa, mti umekuwa mkubwa etc inaweza sababisha signal kudrop.

Pia simu yako inawezekana imeshuka uwezo wa kukamata mawimbi ama Antenna zimelegea.

Na tatizo Tanzania hamna Volte hivyo ukiforce 4G only simu itakua haipatikani.

Kwa kuanzia ukiwa chumbani bonyeza
Code:
 *#*#4636#*#*

Itafunguka menu nenda phone information shuka chini itakuja menu ya kuforce aina fulani ya network itumike kwako weka Lte tu bila tech nyengine uone 4g itapotea kabisa ama signal zitakua tu ndogo.
Kuirudisha kawaid eka Lte/umts/gsm auto badala ya Umts pia inaweza kuwa WCDMA
 
Asante mkuu, nilifanya kama ulivyonielekeza, Nilivyoweka LTE only, Signal hazikusoma kabisa ( no services).

Hivyo nikahitimisha uwenda, simu imeshuka uwezo wa kukamata mawimbi. Ukizingatia pia chumba ninachoishi kiko chini kidogo.

nashukuru.
 
Back
Top Bottom