Naombeni kufafanuliwa Tofauti ya Jaji na Wakili

Naomba nikupinge mkuu hii analogy yako sio sahihi.
Kila judge ni mwanasheria, kila wakili ni mwanasheria
Kwa upande wa pili kila refa anajua sheria za mpira lakini sio kila mchezaji anajua sheria za mpira.
Mchezaji hawezi kuingia uwanjani bila kujua sheria za mpira.Wachezaji wote(Hapa tunaongelea professional players) huwa wanafundishwa sheria za mpira.

Mchezaji akiingia uwanjani bila kujua sheria za mpira hataweza kucheza kwa sababu ataondolewa kupitia red card ndani ya muda mfupi sana.Kwa hiyo kuwa professional player ni pamoja na kuzijua sheria za mpira kwa usahihi ili usitolewe uwanjani kizembe kupitia red card kisha team ikapata hasara.Huwezi ukawa unalipwa mabilioni ya fedha kwa wiki kisha ukawa unaingia uwanjani bila ya kujua sheria za mpira kurisk thamani yako uwanjani.
Vile vile kila mchezaji anajua kuchezea mpira lakini sio kila refa anaweza kuchezea mpira.
Ndio kusema hawana ground moja ya msingi wanapokutana.
Kujua kucheza mpira siyo kupiga chenga na kufunga magoli.Kujua kucheza mpira ni kujua sheria za mpira na ndiyo maana kama mchezaji ataingia uwanjani bila kujua sheria za mpira hatadumu uwanjani humo,ataondolewa fasta sana kupitia red card hata kama ni mpiga chenga mzuri na mfunga magoli mzuri.

Kupigwa red card ni evidence kuwa hujui kucheza mpira.Kwa msingi huo maana yake ni kwamba kila refa anajua kucheza mpira kwa sababu kucheza mpira siyo kupiga chenga wala kufunga magoli bali ni kuzijua na kutii sheria za mpira.Kwa hiyo refa na mchezaji wa mpira wana ground moja.
Kwa upande wa jaji na wakili wanakutana kwenye ground ya kuwa wanasheria wote, hivyo unaweza kusema kila judge anaweza kuwa wakili ikimpendeza, na kila wakili anaweza kuwa jaji ikiwa anasifa ya umri kazini na ikimpendeza mamlaka ya uteuzi.
Sifa ya umri kazini ni experience katika kuijua sheria na marefa wanakuwa na experience hiyo kutokana na idadi ya mechi walizochezesha na jinsi walivyojifunza kutokana na makosa yao.
 
Mi nauliza wale wenye mihuri huku mitaani ukienda na documents anapiga muhuri na kuweka sahihi wanakuwa na elimu ipi?
 
Ninachojua kila Wakili lazima awe Mwanasheria na Huyu Jaji anasoma Elimu gani ya ziada ambayo inamtofautisha na Wakili ambapo nahisi nae Jaji Sheria nayo kasomea

Natanguliza shukrani kuuliza siyo ujinga.
Wote ni wanasheria, jaji anakuwa mtumishi wa serikali mwenye cheo cha juu katika idara ya mahakama.
 
Keshokutwa atakuja kuuliza tofauti ya 'Muhandisi' na 'Mkandarasi'. Naomba mumjibu kabisa, tusisumbuwane!!!!
 
Naomba nichomekee kidogo ,,hivi cross Examination ina umhimu katika ushahidi mkuu
Mbali na kupima ukweli wa ushahidi wa upande mwingine mahakamani...Cross examination pia husaidia kuonesha kutokubaliana na yaliyosemwa na shahidi husika.

Usipofanya cross examination kwenye points muhimu basi itahesabika kuwa umekubaliana na yale aliyoyasema shahidi husika dhidi yako.
 
Mi nauliza wale wenye mihuri huku mitaani ukienda na documents anapiga muhuri na kuweka sahihi wanakuwa na elimu ipi?
Elimu ya sheria. Mawakili wana mamlaka kama mawili mbali na yale ya kiwakili...

1. Notary Public....yaani wana mamlaka kisheria ya kutengeneza nyaraka zozote za kisheria.

2. Makamishena wa viapo....yaani wana mamlaka ya kushuhudia viapo vikichukuliwa mbele yao.

Hayo mamlaka ya kuthibitisha nyaraka wanayapata kwenye sheria ya Notary public & Commissioner for Oaths.

Mbali na mawakili sheria hiyo imetaja watu wengine pia kama Majaji, mahakimu etc wanaweza kufanya shughuli za kikamishena wa viapo.
 
Ni kama tofauti ya ex Na kuzidisha....msalaba Na kujumlisha.

Kicheche waambie...
 
Jaji ni mtu mwenye busara na hekima anayepewa dhamana ya kuamua.

Wakili ni lazima awe amesoma sheria kwa kiwango cha degree na kupita pale Kaw school!

Kuwa Jaji hata cheti tu cha sheria kinatosha muhimu ni Busara na Hekima!
Hii ni kwa mujibu wa katiba ya wapi bwashee? Yani hata uwe na seifiketi ya sheria tu inatosha na unaweza kuwa jaji?
 
Elimu ya sheria. Mawakili wana mamlaka kama mawili mbali na yale ya kiwakili...

1. Notary Public....yaani wana mamlaka kisheria ya kutengeneza nyaraka zozote za kisheria.

2. Makamishena wa viapo....yaani wana mamlaka ya kushuhudia viapo vikichukuliwa mbele yao.

Hayo mamlaka ya kuthibitisha nyaraka wanayapata kwenye sheria ya Notary public & Commissioner for Oaths.

Mbali na mawakili sheria hiyo imetaja watu wengine pia kama Majaji, mahakimu etc wanaweza kufanya shughuli za kikamishena wa viapo.
Ok! Elimu ya sheria katika ngazi ipi ndio unaruhusiwa kuwa na mihuri? Cheti, Dip or Degree?
 
Back
Top Bottom