Naombeni kufafanuliwa Tofauti ya Jaji na Wakili

UVIKO

JF-Expert Member
Jun 14, 2021
285
500
1. Mwanasheria ni mtu yeyote mwenye taaluma ya sheria. Inaweza kuwa cheti, diploma, degree n.k

2. Wakili ni mwanasheria mwenye cheti/leseni inayomruhusu kumuwakilishi mtu mahakani na kuandaa document za kisheria. Kwa sasa ili uwe wakili ni lazima baada ya kupata degree ya sheria upite lawschool, yaani shule ya sheria kwa vitendo.

3. Jaji ni cheo cha kuteuliwa na raisi. Ila kuteuliwa kwake lazima awe na uzoefu wa kufanya kazi za kisheria (wakili/hakimu n.k)kuanzia miaka 10 na kuendelea.
Naomba nichomekee kidogo ,,hivi cross Examination ina umhimu katika ushahidi mkuu
 
Bechede

JF-Expert Member
May 3, 2020
330
1,000
Naomba nichomekee kidogo ,,hivi cross Examination ina umhimu katika ushahidi mkuu
Inasaidia kupima ushahidi unaotolewa kama unaukweli ndani yake ama ni wa kutilia shaka. Mfano:
Shahidi anatoa ushahidi kwamba alimshuhudia mtuhumiwa akitenda kosa mida ya usiku.

Kwenye cross atabanwa maswali ya kimitego ili kupima ushahidi wake kama unakweli. Labda "Ulimshuhudia mtuhumiwa usiku akitenda kosa, Je uliwezaje kumuona wakati ni usiku na giza ni kali?"
 
Asanteh
 
UVIKO

JF-Expert Member
Jun 14, 2021
285
500
Mkuu pia wakili ni mtumishi wa mahakama
Mmmmhh,wakili anawezaje kuwa mtumishi wa Mahakama mkuuu, Kwa uelewa wangu lakini ,mfano mwanafunzi si mtumishi wa shule anakwenda kupata huduma hivyo Kwa wakili nae anaenda kupewa huduma but jaji ni mtumishi wa Mahakama,,, wataaalamu WA haya Mambo watatusaidia
 
chapangombe

Senior Member
Sep 28, 2014
197
250
Mmmmhh,wakili anawezaje kuwa mtumishi wa Mahakama mkuuu, Kwa uelewa wangu lakini ,mfano mwanafunzi si mtumishi wa shule anakwenda kupata huduma hivyo Kwa wakili nae anaenda kupewa huduma but jaji ni mtumishi wa Mahakama,,, wataaalamu WA haya Mambo watatusaidia
Mkuu wakili ni mtumishi wa mahakama fatilia vzr
 
kifinga

JF-Expert Member
Dec 5, 2011
5,058
2,000
... swali zuri! Hakuna chuo kinachofundisha ujaji kama ambavyo hakuna vyuo vinavyofundisha uprofesa. Kama ambavyo uprofesa ni promotion based on one's outstanding performance na kwa majaji ni hivyo hivyo; based on outstanding performance katika ngazi za chini either mahakamani au katika tasnia ya sheria.

Changamoto inakuja kwa shitholes; badala ya vigezo kuzingatiwa wote mnapigwa na butwaa hata fulani naye kawa jaji siku hizi! In short, huo ndio utaratibu.
nimecheka sana
 
Munambefu

JF-Expert Member
Jun 24, 2012
1,975
2,000
Mawakili ni sawa na wachezaji wa mpira na jaji ni refa.Ukielewa mfano huu utanishukuru bila shuruti.
Naomba nikupinge mkuu hii analogy yako sio sahihi.
Kila judge ni mwanasheria, kila wakili ni mwanasheria
Kwa upande wa pili kila refa anajua sheria za mpira lakini sio kila mchezaji anajua sheria za mpira. Vile vile kila mchezaji anajua kuchezea mpira lakini sio kila refa anaweza kuchezea mpira.
Ndio kusema hawana ground moja ya msingi wanapokutana.

Kwa upande wa jaji na wakili wanakutana kwenye ground ya kuwa wanasheria wote, hivyo unaweza kusema kila judge anaweza kuwa wakili ikimpendeza, na kila wakili anaweza kuwa jaji ikiwa anasifa ya umri kazini na ikimpendeza mamlaka ya uteuzi.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom