Naombeni kufafanuliwa Tofauti ya Jaji na Wakili

chapangombe

Senior Member
Sep 28, 2014
199
250
An advocate/wakili ni ofisa wa mahakama na si mtumishi wa Mahakama. Hakimu au jaji ndiyo watumishi wa mahakama ila si mawakili.
Mkuu upo sawa lkn mbona basi advocate ana duty to the court lkn kwanini aitwe officer wa mahakama? Hivi nikisema ni officer wa TANESCO ninakuwa nina maanisha nini? Logic ni kuwa hajaajiriwa na mahakama lkn bado ni muhusika katika mahakama ndio maana mahakama inamwangalia sana wakili kwenye proceeding ili aisaidie court
 
mwagito25

JF-Expert Member
Aug 11, 2013
439
250
1. Mwanasheria ni mtu yeyote mwenye taaluma ya sheria. Inaweza kuwa cheti, diploma, degree n.k

2. Wakili ni mwanasheria mwenye cheti/leseni inayomruhusu kumuwakilishi mtu mahakani na kuandaa document za kisheria. Kwa sasa ili uwe wakili ni lazima baada ya kupata degree ya sheria upite lawschool, yaani shule ya sheria kwa vitendo.

3. Jaji ni cheo cha kuteuliwa na raisi. Ila kuteuliwa kwake lazima awe na uzoefu wa kufanya kazi za kisheria (wakili/hakimu n.k)kuanzia miaka 10 na kuendelea.
Ni bahati tu kupenya kwenye mamlaka za uteuzi(Rais)
 
Tempus Fugit

JF-Expert Member
Jun 22, 2016
574
1,000
Mkuu upo sawa lkn mbona basi advocate ana duty to the court lkn kwanini aitwe officer wa mahakama? Hivi nikisema ni officer wa TANESCO ninakuwa nina maanisha nini? Logic ni kuwa hajaajiriwa na mahakama lkn bado ni muhusika katika mahakama ndio maana mahakama inamwangalia sana wakili kwenye proceeding ili aisaidie court
Wewe ulikosea kusema kuwa wakili ni mtumishi wa Mahakama...Correct wording ni afisa wa Mahakama...akiwa na duty towards the court. Wajibu kwa Mahakama.

Kwa maana ya kuisaidia mahakama ktk utekelezaji wa maamuzi ya migogoro. Yaani wakili anawajibika kuijuza mahakama juu ya kila kitu ambacho kinaweza kuisaidia mahakama itende haki. Asifiche vitu ili kupindisha haki.

Hiyo duty ya wakili kwa mahakama haimfanyi yeye kuwa mtumishi wa mahakama. Neno mtumishi maana yake mtu huyo ni mwajiriwa wa muhimili huo wa Mahakama.

Pamoja na kuwa na wajibu kwa mahakama...mawakili wana duty nyinginezo towards the Public, Profession, oneself, etc...kwa vile wakili ana wajibu kwa umma ktk kuelimisha mambo kadha wa kadha ya kisheria...hatuwezi kusema sasa kuwa wakili ni mtumishi wa umma....kama ambavyo ni misconception kusema kuwa wakili ni mtumishi wa mahakama kwa vile ana wajibu kwa mahakama.
 
Noted comred
 
mnengene

JF-Expert Member
Nov 21, 2011
2,941
2,000
Je, wakili anaweza kuwa Jaji? Afanye nini awe jaji?
jaji anateuliwa na Raisi kasom katiba JMT 109

"(7) Bila ya kuathiri masharti ya ibara ndogo ya (9) ya ibara hii, mtu aweza tu kuteuliwa kuwa Jaji wa Mahakama Kuu ikiwa ana sifa maalum, kama ilivyofafanuliwa katika ibara ndogo ya (8) ya ibara hii, na awe mtu ambaye amekuwa na mojawapo ya sifa maalum kwa muda usiopungua miaka mitano. (8) Kwa madhumuni ya ufafanuzi wa ibara ndogo ya (7), ya (9) na ya (11) ya ibara hii, "sifa maalum" maana yake ni sifa zilizotajwa katika Sheria ya Mawakili (au Sheria nyingine yoyote inayobadilisha hiyo sheria ya Mawakili au inayotumika badala yake) ambazo ni lazima mtu awe nazo mojawapo ya sifa hizo ambazo ni lazima mtu awe nazo mojawapo ya sifa hizo ili aweze kukubaliwa kuandikishwa kama Wakili Tanzania Bara. (9) Iwapo Rais atatosheka kwamba ijapokuwa mtu mwenye sifa mojawapo ya hizo sifa maalum hakuwa nayo sifa hiyo kwa muda usiopungua miaka mitano, lakini mtu huyo ana uwezo, ujuzi na kwa kila hali anafaa kukabidhiwa madaraka ya Jaji wa Mahakama Kuu na kuna sababu za kumfanya mtu huyo astahili kukabidhiwa madaraka hayo, basi Rais aweza kutangua lile sharti la kuwa na sifa maalum kwa muda usiopungua miaka mitano, na baada ya kushauriana na Tume ya Kuajiri ya Mahakama, Rais aweza kumteua mtu huyo kuwa Jaji wa Mahakama Kuu."
 
mnengene

JF-Expert Member
Nov 21, 2011
2,941
2,000
Cheo cha jaji ni cha uteuzi ambacho rais anateua. Hakuna cha kusomea zaidi ya kubahatika kupenya kwenye mamlaka za uteuzi
katiba ya JMT sura 109 inaeleza kuhusu uteuzi wa majaji

(7) Bila ya kuathiri masharti ya ibara ndogo ya (9) ya ibara hii, mtu aweza tu kuteuliwa kuwa Jaji wa Mahakama Kuu ikiwa ana sifa maalum, kama ilivyofafanuliwa katika ibara ndogo ya (8) ya ibara hii, na awe mtu ambaye amekuwa na mojawapo ya sifa maalum kwa muda usiopungua miaka mitano. (8) Kwa madhumuni ya ufafanuzi wa ibara ndogo ya (7), ya (9) na ya (11) ya ibara hii, "sifa maalum" maana yake ni sifa zilizotajwa katika Sheria ya Mawakili (au Sheria nyingine yoyote inayobadilisha hiyo sheria ya Mawakili au inayotumika badala yake) ambazo ni lazima mtu awe nazo mojawapo ya sifa hizo ambazo ni lazima mtu awe nazo mojawapo ya sifa hizo ili aweze kukubaliwa kuandikishwa kama Wakili Tanzania Bara. (9) Iwapo Rais atatosheka kwamba ijapokuwa mtu mwenye sifa mojawapo ya hizo sifa maalum hakuwa nayo sifa hiyo kwa muda usiopungua miaka mitano, lakini mtu huyo ana uwezo, ujuzi na kwa kila hali anafaa kukabidhiwa madaraka ya Jaji wa Mahakama Kuu na kuna sababu za kumfanya mtu huyo astahili kukabidhiwa madaraka hayo, basi Rais aweza kutangua lile sharti la kuwa na sifa maalum kwa muda usiopungua miaka mitano, na baada ya kushauriana na Tume ya Kuajiri ya Mahakama, Rais aweza kumteua mtu huyo kuwa Jaji wa Mahakama Kuu.
 
Behaviourist

JF-Expert Member
Apr 8, 2016
37,338
2,000
Ila refa anaweza kuwa hajawahi kucheza mpira, lakin kwa Jaji ni tofaut
Kucheza mpira ni kuzijua sheria za mpira na kuzitii sheria hizo na wala siyo kupiga chenga na kufunga magoli mengi na ndiyo maana mchezaji akiingia uwanjani bila ya kujua sheria za mpira atarudishwa bench haraka sana kupitia red card.Hii maana yake ni kwamba refa na wachezaji wote wanazijua sheria za mpira na kwa hiyo wote ni wachezaji wa mpira.
 
yello masai

JF-Expert Member
Jan 8, 2016
3,149
2,000
Je, wakili anaweza kuwa Jaji? Afanye nini awe jaji?
Mi nafikiri hana cha kufanya ili awe jaji. Akiwa wakili tu anaweza kuteuliwa kuwa jaji. Maana navyojua majaji wanateuliwa na Raisi majina yakishapendekezwa na jaji mkuu, ampabo wateuliwa wanakuwa wanasheria hasa mawakili.
Naweza pia nisiwe sahihi.
 
Nahonyo

JF-Expert Member
Dec 28, 2012
3,983
2,000
Wakili, ni mwakilishi, yaani anaefanya kazi kwa kwa niaba ya mtu mwingine.
Mfano Umeshishitakiwa ama umeshitaki, yeye husimama kukutetea au kuwa upande wa mashitaka kukusemea badala ya wewe.

Jaji, ni mhukumu, wa daraja la juu, na hufanya kazi kwenye ngazi ya mahakama ya kitaifa/kimataifa.
 
Dabil

JF-Expert Member
Sep 30, 2021
2,355
2,000
Kwa maoni mengi inaonekana majaji wengi ni vilaza kuliko mawakili
 
mnengene

JF-Expert Member
Nov 21, 2011
2,941
2,000
Kwa maoni mengi inaonekana majaji wengi ni vilaza kuliko mawakili
ila sio mawakili wa serikali,
Majaji na mawakili wa serikali ni watu ambao wana uhakika wa mshahara hata asiposhinda kesi, akiumwa na asipokwenda kazini.
kwahiyo wengi wanabweteka na hawa jibidiishi sana kwenye kujielimisha ndio maana wapo shallow sana
Ila Mawakili binafsi ambao wamejiajiri wanalipwa kadri walivyoperform hivyo mara nyingi wapo agressive kuhakikisha wanafanya vizuri.
majaji weneyewe wapo kuwaridhisha watawala (serikali) ili wapate kuteuliwa kwenye nafasi za juu mf mahakama ya rufaa au kupigiwa chepuo kwenye mahakama za kimataifa
 
mgunga pori

JF-Expert Member
Jul 23, 2016
3,265
2,000
Hii ni kwa mujibu wa katiba ya wapi bwashee? Yani hata uwe na seifiketi ya sheria tu inatosha na unaweza kuwa jaji?
Mkuu mwanasheria ni kuanzia degree
So ukiwa na certificate ya law au diploma huna uwezo wa kuwa judge au wakili
Waweza kuwa karani wa mahakama
Mpaka ukaongeze elimu
 
kidunula1

JF-Expert Member
Apr 2, 2016
6,129
2,000
1. Mwanasheria ni mtu yeyote mwenye taaluma ya sheria. Inaweza kuwa cheti, diploma, degree n.k

2. Wakili ni mwanasheria mwenye cheti/leseni inayomruhusu kumuwakilishi mtu mahakani na kuandaa document za kisheria. Kwa sasa ili uwe wakili ni lazima baada ya kupata degree ya sheria upite lawschool, yaani shule ya sheria kwa vitendo.

3. Jaji ni cheo cha kuteuliwa na raisi. Ila kuteuliwa kwake lazima awe na uzoefu wa kufanya kazi za kisheria (wakili/hakimu n.k)kuanzia miaka 10 na kuendelea.
Nimepata mwanga sana!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom