Naombeni kazi wakuu hali ni mbaya

msouth23

Member
Oct 31, 2015
73
59
Habari zenu wakuu,

Hope ni wazima otherwise Allah awafanyie wepesi.

Lengo la uzi huu ni kuomba kazi, kibarua au shughuli yoyote halali itayoniingizia kipato.

Nina umri wa miaka 27, nina elimu ya Diploma ya Information Technology ila sijabahatika kupata hata kazi ya kujitolea (mimi ni kati ya wale watu ambao hatuna watu wa connection). Nipo DSM naishi maeneo ya Tegeta nipo tayari kufanya kazi yoyote halali hata ukiniambia nije kufanya usafi sehemu niko tayari.

Nina ujuzi wa computer kuitumia na kurekebisha matatizo mbalimbali, nimeshawahi kufanya kazi ya boda boda, nimeshawahi kuwa shop keeper, hayo yote nimefanya nikiwa mkoani kwa hapa Dar ni mgeni nimetoka mkoani baada ya mama yangu kufariki.

Nina imani nitapata wa kunishika mkono humu na ukihitaji kunipa kazi au connection yoyote basi mawasiliano yangu 0674633302.

Asanteni sana.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom