Naombeni dawa ya mapenzi tafadhali

Naombeni dawa ya mapenzi tafadhali

Juma WALEO

JF-Expert Member
Joined
Jan 16, 2014
Posts
204
Reaction score
40
Mimi sitaki kusema mengi jamani ila kila mtu anajua mapenzi yanavyoumiza, hebu tupeane njia za kuinjoy mapenzi bila stress.Labda kuna njia ya kuweza kuzuia maumivi jamani, kwa yeyote anayefahamu namna ya kujizuia na haya maumivu.
 
Mapenzi hayana formula,Ila angalau upate muda wa kua na mwenza wako karibu mchekeshane muongee yenu.
Kama una future nae na mengine mengi.
 
Usipende Kuhonga, ukishindwa hilo kunywa panado 2 na piritoni 4 mara 2 kwa siku ndani ya mwezi mmoja, Maumivu yakizidi nenda Hospitali
 
Hivi mbona huwa mnapenda kusingizia mapenzi kwenye downfalls zenu za kutendwa?
mapenzi yangelikuwa ni kansa kiasi hicho basi kusingelikuwa na neno mapenzi.
 
Mimi sitaki kusema mengi jaman ila kila mtu anajua mapenz yanavyozingua
hebu 2peane njia za kuinjoy mapenz bila stress!

Kwanza usipende kujenga fikra negative things juu ya mpenz wako,pili usipende chunguza xna mwenzako mfano kuangalia sms kwenye cmu yake kingine mfanye mtu wako kama rafiki wa kawaida mfano kutaniana au kuchekeshana vitu mbalmbali ukifanya ayo utaenjoy sana mpendwa.
 
Maumivu ya mapenzi hayatakwisha mpaka pale kila mmoja wetu atakapokuwa anajua anataka nini penzini na tukiwa na subira na uvumilivu,kila mmoja wetu yupo ambaye ameumbwa maalumu kwa ajili yake,yupo ambaye nyoyo zenu zimeunganishwa automatic na nguvu ya penzi na ukikutana nae haihitaji hata kuambiwa kwani moyo wako wenyewe utakuambia kwani ndiye hitaji lake.

Jambo la hekima ni kuwa na uvumilivu na subira kwani tamaa za kimwili ndizo ambazo hutupelekea tunaangukia sehemu ambazo zinatufanya tulie kwa kuendekeza mahitaji ya miili yetu,lazima utambue kuwa safari ya kuelekea kumpata yule atakaye ujaza moyo wako furaha na raha ni ndefu sana inayohitaji subira kwani hapo kati kati ya safari utakutana na walaghai wengi sana ambao wote wanazungumza lugha moja inayofanana hivyo kukupa wakati mgumu wa kumtambua yupi mkweli na yupi muongo.

Tusiwapime wenzi wetu kwa maneno yao matamu kwani si mara zote maneno hutoka moyoni bali matendo na ila kama unatafuta hela penzini basi maumivu ni halali yako na kama unatafuta furaha penzini,ukivuta subira na ukivumilia hatimaye utaipata furaha ya kweli,kwani muumba kamwe hajawahi kumtupa au kumjaalia kitu kibaya mja mwenye subira na mvumilivu na wakati ukifika utampata wako.
 
Japo ni gangster, baby nayajua machungu! Watu wa hip hop
 
Kwa wanahisabati,
Love(L) is complex therefore it has two parts imagenary part and real part.

ie L = ai + b

a&b ni namba tu

Kwa hiyo kokotoa hesabu yako
 
Kwanza usipende kujenga fikra negative things juu ya mpenz wako,pili usipende chunguza xna mwenzako mfano kuangalia sms kwenye cmu yake kingine mfanye mtu wako kama rafiki wa kawaida mfano kutaniana au kuchekeshana vitu mbalmbali ukifanya ayo utaenjoy sana mpendwa.

Mmmmmh yawezekana. Ila smtym kujenga negativity inasaidia kujiham. Nowerdys hakuna mapenz ya dhat, mtu anaangalia atapata fulsa gn kwa mwenzie. Mfano wakina dada ukiwatajia ndoa duuuu utawamaliza
 
Mimi sitaki kusema mengi jaman ila kila mtu anajua mapenz yanavyozingua
hebu 2peane njia za kuinjoy mapenz bila stress!

Dawa ya mapenzi inauzwa Kwa swalehe madawa na kwa Haji tumbo Zanzibar utapata wala Sio ghali...
 
Mimi sitaki kusema mengi jaman ila kila mtu anajua mapenz yanavyozingua
hebu 2peane njia za kuinjoy mapenz bila stress!

Stress, visa, mikasa, wivu na mazagzaga mengine yanayokuja na kifurushi cha LOVE ndo kuinjoi mapenzi, kama haupitii hivi vitu, kuinjoi LOVE itakuwa ngumu.
Wana wa adam sio robots.
Hivyo sahau, hamna formula.
 
Dawa usiingie huko kinga ni bora kuliko tiba

Tatizo binadamu (wazima wa afya) tumeumbwa kwa 'mabati', na mapenzi ni 'sumaku', yanatuvuta. Tuko kwenye jamii ambayo ndo mapenzi yenyewe, hivyo kutokujiingiza ktk mapenzi kwahitaji kazi ya ziada kweli kweli.
 
Back
Top Bottom