Naomba ushauri

Naomba ushauri

G

guest-1792649409

Guest
Mimi ni mwanafunzi wa udakitari mwaka 3(MD3) katika chuo kikuu cha Afya Bugando.
Kuna malumbano hapa mnaweza kutusaidia kutatua hii changamoto au kutushauri kama viongozi watarajiwa katika jamii zetu baada ya kumaliza chuo.
Tunautaratibu wa kusaidiana kuchangiana kiasi chochote cha pesa ili kumfariji na kumpa mkono wa pole mwanafunzi yeyote aliyepata matatizo eg kufiwa na wazazi ,kupata ajali au kuumwa.
Je mwanafunzi ambae hatoi ushirikiano wa kuguswa na matatizo ya wenzake, siku akipata matatizo ya kufiwa na mzazi wake afu tukagoma kumchangia rambirambi tutakuwa tumekosea? , Naomba ushauri wenu.Ahsante
 
Tenda wema pasina kungoja shukran yawezekana akawa anahitaji kuchangia ila pia hana je mtaendelea kumtenga

Waafrika huu utaratibu wa rambi rambi tumeufanya kua wa lazima kwa kila mtu hapana rambi rambi haimrejeshi aliyeondoka
 
Mwanafunzi upo mwaka wa tatu, unasoma sayansi....ishu ndogo kama hii unaileta hapa ? Ushauriwe nini sasa ?

Nyie ndio mkija kuajiriwa mnafanya matibabu viseversa.....kichwa unapasua goti....na goti unapasua kichwa ... uelewa mdogo
 
Tulikuwa na mtu wa aina hiyo ofisini, kila kitu ni kupinga tu na hakuwahi kumchangia mtu. Alipopatwa na tatizo tukakubaliana tushiriki kikamilifu kwa hali na mali. Tulijitoa mpaka familia yake ikashangaa. Baada ya hapo alibadilika na kuwa na ushirikiano na wenzake.
 
Mimi ni mwanafunzi wa udakitari mwaka 3(MD3) katika chuo kikuu cha Afya Bugando.
Kuna malumbano hapa mnaweza kutusaidia kutatua hii changamoto au kutushauri kama viongozi watarajiwa katika jamii zetu baada ya kumaliza chuo.
Tunautaratibu wa kusaidiana kuchangiana kiasi chochote cha pesa ili kumfariji na kumpa mkono wa pole mwanafunzi yeyote aliyepata matatizo eg kufiwa na wazazi ,kupata ajali au kuumwa.
Je mwanafunzi ambae hatoi ushirikiano wa kuguswa na matatizo ya wenzake, siku akipata matatizo ya kufiwa na mzazi wake afu tukagoma kumchangia rambirambi tutakuwa tumekosea? , Naomba ushauri wenu.Ahsante
Naona dogo umeanzisha kamradi upige pesa za wenzio? we soma acha kupoteza muda na michango mpuuzi wewe kazi kukopi assignment za watu!
 
Eti kiongozi wa kesho kwenye jamii! Jamii hiyo which? jamii hiyo who? Kwa akili hizo uwe kiongozi wa nani? Kwa jamaa kwa harakaharaka anatamaa kabisa, ndio vijana wanaoweza kununulika kwa vipande vya fedha km kina gilishoni
 
Mimi ni mwanafunzi wa udakitari mwaka 3(MD3) katika chuo kikuu cha Afya Bugando.
Kuna malumbano hapa mnaweza kutusaidia kutatua hii changamoto au kutushauri kama viongozi watarajiwa katika jamii zetu baada ya kumaliza chuo.
Tunautaratibu wa kusaidiana kuchangiana kiasi chochote cha pesa ili kumfariji na kumpa mkono wa pole mwanafunzi yeyote aliyepata matatizo eg kufiwa na wazazi ,kupata ajali au kuumwa.
Je mwanafunzi ambae hatoi ushirikiano wa kuguswa na matatizo ya wenzake, siku akipata matatizo ya kufiwa na mzazi wake afu tukagoma kumchangia rambirambi tutakuwa tumekosea? , Naomba ushauri wenu.Ahsante
Zingatia hekima hii ya yesu aliye zungumza kwenye biblia.

Alisema

Unayo taka ufanyiwe na watu na wewe wafanyie hayohayo

Huyo akikutwa na changamoto ( msimsaidie hapo ndipo atakapo jua maana ya kusaidiana katika matatizo.

Ukimsaidia utaniongezea ubinafsi.

Asante.
 
Mwanafunzi upo mwaka wa tatu, unasoma sayansi....ishu ndogo kama hii unaileta hapa ? Ushauriwe nini sasa ?

Nyie ndio mkija kuajiriwa mnafanya matibabu viseversa.....kichwa unapasua goti....na goti unapasua kichwa ... uelewa mdogo
Hiki kitu kinahitaji uelewa mkuu.!!!?. Haya ni mambo ya kijamii busara inahitajika kushauri.
 
Hata uelewa pia ni muhimu mkuu .... si kila jambo tu unalipeleka kwa watu unataka ushauri !!! Ishu kama ya mleta mada haihitaji hata elimu ya darasa la pili.... hapo ni uelewa tu wa kuchanganua mambo ya kijamii
 
Mimi ni mwanafunzi wa udakitari mwaka 3(MD3) katika chuo kikuu cha Afya Bugando.
Kuna malumbano hapa mnaweza kutusaidia kutatua hii changamoto au kutushauri kama viongozi watarajiwa katika jamii zetu baada ya kumaliza chuo.
Tunautaratibu wa kusaidiana kuchangiana kiasi chochote cha pesa ili kumfariji na kumpa mkono wa pole mwanafunzi yeyote aliyepata matatizo eg kufiwa na wazazi ,kupata ajali au kuumwa.
Kwa utaratibu wenu; kuchangiana "kiasi chochote cha pesa ili kumfariji.." inamaanisha nini?? Dkt. mtarajiwa, unaonaje mwenzenu akija kumshika mkono na kumtamkia "Pole rafiki yangu; Mungu akupe afya na nguvu ya kuvumilia kipindi hiki kigumu kwako kisha akaketi pembeni yake na kuongea(Mazungumzoya kumfariji)" na akaondoka bila kutoa hata senti moja. Je, atakuwa hajachangia chochote? Tumieni Busara na Hekima zenu.
Je mwanafunzi ambae hatoi ushirikiano wa kuguswa na matatizo ya wenzake, siku akipata matatizo ya kufiwa na mzazi wake afu tukagoma kumchangia rambirambi tutakuwa tumekosea? , Naomba ushauri wenu.Ahsante
Kama Utaratibu mliojiwekea unasema hivyo, na mkiamua kusimamia hapo na kutimiza ilivyoandikwa; mtakuwa hamjakosea ila msiache kwenda kuzungumza naye na kumfariji, halafu mliweke wazi kwamba mtu binafsi anaweza kutoa chochote alichonacho i.e. Msiwagomeshe na wale wenye roho ya kutoa bila kuzingatia Utaratibu wa Andiko lenu.
Ni hayo tu.
 
Tulikuwa na mtu wa aina hiyo ofisini, kila kitu ni kupinga tu na hakuwahi kumchangia mtu. Alipopatwa na tatizo tukakubaliana tushiriki kikamilifu kwa hali na mali. Tulijitoa mpaka familia yake ikashangaa. Baada ya hapo alibadilika na kuwa na ushirikiano na wenzake.
Ushauri mzuri kwa mfano.
Wakati mwingine matendo mema hubadirisha mtazamo na misimamo ya wanaopinga.

Huwa napenda sana ule mstari wa biblia (sijui ni Mathayo au Yohana....au nani vile).

"Hubirini kwa matendo yenu"
 
Safi kabisa. Tusiende kwa kauli ya Jino kwa jino au Tit for Tat.
 
Back
Top Bottom