Naomba ushauri wa kisheria kuhusu wito wa ustawi wa jamii

Kwatu

New Member
Oct 14, 2019
2
2
Ndugu zangu katika jukwaa la sharia, Salaam.
Naomba nitumie ukurasa huu kuomba ushauri wenu wa kisheria, mimi ni kijana (mwanaume) mwenye umri wa miaka 34, nina mke mmoja na watoto wa tatu (wakike 2, na kiume 1).

Lililonileta hapa ni kuhusu mmoja kati ya wanangu (wakike) ambaye nilizaa nje ya ndoa mwaka 2006, mimi na mama yake tulikutana Mbeya, mahusiano yakaanza kwa upendo mkubwa japo kiumri tulikuwa bado wadogo mimi nikiwa mwanafunzi lakini yeye kwa bahati mbaya hakuwa anasoma, tukajikuta tumeshiriki tendo la ndoa mara moja kabla ya yeye kuhama Mbeya na kuelekea Arusha kwao (Mbeya alikuwa anaisha kwa shangazi yake).
Kitu ambacho sikujua ni kama aliondoka na ujauzito wangu, uzingatia simu zilikuwepo kwa wachache wakati ule, maisha yaliendelea bira ya mawasiliano yoyote baina yetu, na mimi nikiendelea na masomo. Mwaka 2012 nikamaliza chuo kikuu, na mwaka huo huo nikabahatika kupata kazi kwenye shirika.
Kuna mdogo wangu aliyenifuata akawa amejiunga chuo cha afya KCMC 2013, akiwa katika masomo yake kwa vitendo wodini alikutana na huyu mama wa mtoto wangu, kwa kuwa walikuwa wanafahamiana na mdogo wangu alikuwa anajua kuwa nilikuwa na mahusiano naye basi wakapeana namba za simu, na hatimaye nami nikapata namba ya mzazi mwenzangu.

Nakumbuka ilikuwa jioni ya saa kumi na moja baada ya kazi nikapiga simu na kumsalimia, lakini baada ya kusikia ni mimi akaanza kulia sana, nikamuuliza chanzo cha kulia, akaniambia kuwa alivyotoka Mbeya alitoka na ujauzito wangu na mtoto alikuwa akimsumbua sana akitaka kuniona baba yake. Kwa sababu nilimpenda sana na kipindi cha nyuma nilimuani sana sikuwa na shaka na huyo mtoto, akanipatia mtoto nizungumze naye, kwa kweri nilifurahi sana, ukizingatia sikuamini kama nitakuwa na mtoto mkubwa kwa wakati huo.

Nikamuhakikishia kuwa nitamuhudumia mtoto kwa chochote atacho shuleni hata nyumbani, JAPO YEYE ALIKUWA TAYARI KWENYE NDOA, nilijitahidi ninatuma hela kwa mtoto natuma ya kutosha watoto wengine 2 ambao alizaa na huyo baba mwengine.
Mtoto akaanza kuniambia kuwa anataka kuwafahamu ndugu zangu (Baba na Mama) yaani babu na bibi yake, nikamuahidi kuwa nitakuja kumpeleka. Mwaka 2014 nikamweleza mama yangu na baadhi ya ndugu zangu kuwa nina mtoto, wazazi wakifurahi japo walinisihi kumwambia mke wangu kwani mwaka huo January nilikuwa nimeingia kwenye ndoa.

Nikamweleza mke wangu pia, yeye akaniuliza mtoto anaumri gani, nilivyomjibu akalinganisha na umri wa mahusiano yetu akakubari, na akasema kama nitahitaji kumchukua yeye yupo tayari kumlea, na alipenda siku tukija pata watoto wengine basi wasitofautiane.

NIFUPISHE KIDOGO:

Mwaka 2016 nikiwa kikazi Ruvuma, mama yake alinipigia simu kuwa mume wake baada ya kusikia kuwa mtoto baba yake amejulikana na anamuhudimia mtoto wake alisema hataki kumuona mwanangu kwake (Kulingana na maelezo ya mama), nikamwambia sawa ila nipo safari nikirudi nitafanya utaratibu wa kumuhamisha, mama akakata na kusema jumamosi inayofuata mtoto atampandisha kwenye basi kuja nilipo ikizingatia kabla ya huo mwaka mtoto alishawahi kuja kwangu mara mbili peke yake.

Nikakubaliana naye, na mimi nikahairisha field work na kurudi mkoani kwangu kumsubiri mtoto, nilirudi ijumaa jumamosi jioni nikawa stand kumsubiri mtoto. Gari za Arusha zote zikaingia bira ya kumuona mtoto, nikampigia simu kama kuna gari jingine kampandisha, jibu alilonipa liliNIpa hasira sana na kujiuliza maswali mengi sana, alisema “UMESIKIA WAPI MTOTO ANASAFIRISHWA KAMA NJUGU”.

Nikamuuliza kama kuna jambo lolote anataka ambalo sijafanya angepende nifanye, akaniambia anahitaji hela ya mtaji ili naye awe na maisha yake, nilituma pesa ambayo alihitaji, lakini bado mtoto hakuja. Baada ya hapo vituko kutoka kwa mama vikaanza, mara mtoto nyumbani hana chakula, japo nilikuwa natuma pesa ya matumizi kila mwezi, lakini ilikuwa kama kawaida kila mwisho wa mwezi mtoto alikuwa anaumwana na bill ilikuwa inakuja kuanzia laki mbili, baadae nikaona bora nimkatie TOTO AFYA CARD, nikafanye hivyo, cha kushangaza baada ya kupatikana hiyo card, mtoto sikuwahi sikia akiumwa tena.

Mungu mkubwa mtoto akamaliza darasa la saba na kufaulu vizuri kwa wastani wa B, japo shule aliyochaguliwa ilikuwa shule ya kutwa ingawa wazazi wa kata hiyo walichanga pesa na wakajenga hostel kwa watoto wakike, kulikuwa na michango na ada kidogo ya kuingia kwenye hostel hizo, nikaona ni busara mwanangu kwenda kuishi hostel ili asome vizuri.

Kidato cha kwanza kikaanza nayeye masomo yakaanza kwa kasi sana, nami nikawaza wakati huo ndio ulikuwa wakati sahihi wa mimi kufanya mpango wa kumhamisha ili tuwe karibu Zaidi, bahati ikawa nzuri kwangu, walipofunga midterm mtoto aliomba nimuhamishe kwani alitaka asome shule nzuri Zaidi, nikazungumza na mama yake naye akakubari, mchakato wa kumhamisha shule ukaanza, na nikapata shule moja ya wasichana tupu, nikampa taarifa mtoto na mama yake, wote wakafurahi kesho yake nikamwambia kuwa nitatuma form za uhamisho kwa ajiri ya kupitishwa shule anayosoma, akakubari.
Form zilitumwa kwa mama lakini nilishangazwa na sms aliyotuma baada ya kupokea form hizo, iliandikwa hivi “BABA (JINA LA MTOTO) NITAZIDI KUKUHESHIMU NA KUKUESHIMU NA NINASHUKURU SANA KUMSAIDIA MWANAO TOKA MWANZO NA MPAKA SASA ILA NAOMBA SASAIVI NIKUSAIDIE NA MM”. nikamwambia sawa nikaamini kuwa jambo zuri kusaidiana, siku ya jumatatu nikamuuliza kama amepeleka form shule akanijibu “KWANI SMS YANGU HUKUIPATA AU HAUJAIELEWA?” nikamuuliza anamaanisha nini, akanijibu “NAMAANISHA KUWA SITAKI MTOTO AHAME NA KUANZIA LEO SITAKI UMUHUDUMIE MWANANGU, ENDELEA NA MAISHA YAKO NA FAMILIA YAKO
Basi uhamisho ukaishia hapo japo nilimsihi sana aligoma.

Ushauri ninao hitaji ni kutokana na wito wa ofisi ya ustawi wa jamii ukinataka kwenda ofisini kwao kwa kutokutoa huduma kwa mtoto. Nilikataa kutoa matumizi tena.
NAOMBA USHAURI WENU.
ASANTE.
 
Mtoto ana zaidi ya miaka 7, Mama yake kaolewa na familia nyengine, uwezo wa kumhudumia at the best level of the chilid interest hana, familia ya mkeo na mumewe wake wanakuletea figisu na kukugeuza mtaji, HUYO MTOTO UNASUBIRI NINI KUMCHUKUA?

Itika wito na nenda na vielelezo, lkn mchukue mwanao!
 
Mtoto ana zaidi ya miaka 7, Mama yake kaolewa na familia nyengine, uwezo wa kumhudumia at the best level of the chilid interest hana, familia ya mkeo na mumewe wake wanakuletea figisu na kukugeuza mtaji, HUYO MTOTO UNASUBIRI NINI KUMCHUKUA?

Itika wito na nenda na vielelezo, lkn mchukue mwanao!
Asante kwa ushauri, nitaitika wito,
 
skia yaan hata unapoenda kuitika wito tambua kwamba lile dawat huwa lipo kuwatetea wanawake kwa hyo kuwa makn usijichanganye kwny maelezo

cha pili na muhmu nenda na zle message za mpesa ambazo ulikuwa ukimtumia pesa hyo itakuwa kama ushahidi
 
kesi ya nyani anaenda kuendesha ngedere na wewe mwenzangu nguchiro, ukipata haki hapo niambie najitoa JF.

Wewe komaa umchukue mwanao, ni gia yao ya kutaka ukamuliwe pesa kila leo kisa mtoto.

mwisho; ulisikia wapi kuwa ustawi wa jamii ni mahakama? lile ni dawati la usuluhishi na kuwatetea wamama. usipoenda mara kadhaa watakimbilia kumshauri mzazi mwenzio aende mahakamani tu, hawana meno wale.
 
kesi ya nyani anaenda kuendesha ngedere na wewe mwenzangu nguchiro, ukipata haki hapo niambie najitoa JF.

Wewe komaa umchukue mwanao, ni gia yao ya kutaka ukamuliwe pesa kila leo kisa mtoto.

mwisho; ulisikia wapi kuwa ustawi wa jamii ni mahakama? lile ni dawati la usuluhishi na kuwatetea wamama. usipoenda mara kadhaa watakimbilia kumshauri mzazi mwenzio aende mahakamani tu, hawana meno wale.
ur right
 
Back
Top Bottom