Naomba ushauri | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Naomba ushauri

Discussion in 'JF Doctor' started by KIZAKINENE, Dec 31, 2011.

 1. K

  KIZAKINENE Member

  #1
  Dec 31, 2011
  Joined: Dec 21, 2011
  Messages: 8
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ndugu zangu wanafamilia wa JF nayotoa yangu matatizo kwenu ni hivi.
  Kwa kipindi cha karibu miaka kumi sasa nimekuwa nikisumbuliwa na matatizo ya ya tumbo, mwanzo nilikuwa sijui ni tatizo gani kwani lilikuwa linauma na kujaa gesi, wakati mwingine naumwa mwili mzinma nakuw na dalili zote kama mtu wenye malaria-ninapopima nakutwa sina. Mwaka 2002 nikapiga X-ray ya tumbo nikaambiwa Duodenum cup is ulcerated, nikapewa daya inaitwa Helligo-kit (samahani kama nimekosea jina la dawa hiyo) nikatumia mwezi mzima, sikupata nafuu, nikendelea kutumia madawa mengi tu ya anti-acid mpaka mwaka 2004 nikaenda hospitali nyingine nikafanyiwa Endoscopy-Yule daktari akaniambia hajaona vidonda ila wamechukua saple kutoka tumboni kwangu wataipima-Baada ya wiki mbili majibu hayakuonyesha infection yoyote tumboni, ila akasema tumboni kwangu kuna Inflamation akanipa dawa sikupata nafuu. sasa nikawa nachangnya madawa ya tiba mbadala na hospitali kwa nyakati tofauti kila hali inapokuwa mbaya. Mwaka 2010 nikaenda tena hospitali nyingine wakanifanyia endoscopy. Daktari aksema kweli ameona vidonda na ni fresh, ila pale kwenye duodenum akasema vimepona ('Healed) nikatumia dawa za gharama sana, lakini sikupata ahueni.
  Nikaenda kwa Dada RAHABU wa pale Ilala na vipmo vyangu niaktumia dawa zake kama alivyonielekeza, kwa kweli nilichofanikiwa ni kuondoa ile milendamilenda ili ilyokuwa inatoka pamoja na choo, lakini maumivu yatumbo , tumbo kujaa gesi na ninapumua sana kupitia haja kubwa ambapo baada ya tendo hilo hwa napata ahueni ya muda. nimepewa masharti mengi tu ya chakula ninajitahdi
  kuyafuata.

  Naombeni ushauri wa kuapa dawa hii ya vidonda vya tumbo, au inawezekana nina tatizo lingine katika tumbo langu lia madaktari hawajapata ufunuo kuelewa nini kaikinanisumbua
   
 2. Kennedy

  Kennedy JF-Expert Member

  #2
  Jan 1, 2012
  Joined: Dec 28, 2011
  Messages: 11,233
  Likes Received: 2,915
  Trophy Points: 280
  Mkuu pole,dokta atakupa ushauri ila ni vema uwe close na jukwaa hili.
   
 3. D

  Dotowangu JF-Expert Member

  #3
  Jan 1, 2012
  Joined: Nov 14, 2011
  Messages: 242
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  jaribu hii dawa ina saidia sana matatizo ya tumbo... Chukua vitunguu saumu vitano vizima sio punje vya kienyeji chambua na usage au ubrend.. Kisha changanya na asali mbichi nusu lita.. Kula vijiko vitatu vikubwa kutwa mara tatu kwa muda wa wiki mbili.. Kwa uwezo wake Allah utapata nafuu.. Dawa hii inatibu magonjwa ya tumbo kujaa gesi na kunguruma na mengine mengi ya tumbo..
   
 4. Gosbertgoodluck

  Gosbertgoodluck JF-Expert Member

  #4
  Jan 1, 2012
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 2,866
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 0
  Pole sana ndugu yangu. Nami nimepitia mateso hayo japo kwa sasa naendelea vizuri sana baada ya kutumia dawa ya kienyeji niliyoipata kwa mzee mmoja pale Jijini Mwanza. Wewe kwa sasa upo wapi?
   
 5. NusuMutu

  NusuMutu JF-Expert Member

  #5
  Jan 1, 2012
  Joined: Sep 26, 2011
  Messages: 423
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  pole sana mkuu, Mungu atakusaidia
   
 6. n

  ngwana ongwa doi Member

  #6
  Jan 2, 2012
  Joined: Dec 26, 2011
  Messages: 75
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  ukitumia antacid(omeprazole)na antibiotic(clarythromyzine) kwa pamoja yaweza kukusaidia.Pia jaribu kula chakula kiasi baada ya muda kisha unakula tena kuliko kula chakula kingi sana kwa wakati mmoja,jitahidi kula vyakula vya majimaji na upunguze vyakula vya mafuta mengi nk.hii itakupunguzia usumbufu na baada ya mlo jitahidi kufanya kazi kuliko kukaa tu kwani ukikaa digestion inakwenda polepole sana.
   
 7. K

  KIZAKINENE Member

  #7
  Jan 2, 2012
  Joined: Dec 21, 2011
  Messages: 8
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  aSANTE SANA NDUGU YANGU, KWA SASA NIPO HAPA DSM. NAOMBA UNIELEKEZE HUO MWANZA NITAFIKA TU
   
 8. K

  KIZAKINENE Member

  #8
  Jan 2, 2012
  Joined: Dec 21, 2011
  Messages: 8
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Huo mseto wa dawa ulizo shauri nimetumia sana na sikupata ahueni, ila ushauri wa kula kidogokidogo ni mzuri pamoja na kufanya mazoezi, nitauzingatia. Asante
   
 9. Angel Msoffe

  Angel Msoffe JF-Expert Member

  #9
  Jan 2, 2012
  Joined: Jun 21, 2011
  Messages: 6,797
  Likes Received: 74
  Trophy Points: 145
  WALAH AKILA VITUNGUU SAUMU NA ANAVIDONDA VYA TUMBO ATAUMIA SN,mimi juzi nilikula vitunguu saumu na asali kwa lengo la kuponya kichwa niliumwa na tumbo vibaya sana, angekua hana vidonga dawa ya vitunguu ingemfaa sana.
   
 10. K

  KIZAKINENE Member

  #10
  Jan 3, 2012
  Joined: Dec 21, 2011
  Messages: 8
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  hapo sasa umnichanganya.
   
 11. e

  ejogo JF-Expert Member

  #11
  Jan 3, 2012
  Joined: Dec 19, 2009
  Messages: 994
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Kuna jamaa aliweka uzi wake humu akisema alikunywa mkojo wake mwenyewe kwa siku sana, ule wa asubuhi na maajabu yakatendeka tumboni mwake, alijisikia kupona kabisa vidonda vyake vya tumbo
   
 12. doctorz

  doctorz JF-Expert Member

  #12
  Jan 3, 2012
  Joined: Aug 10, 2010
  Messages: 907
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Pole sana. Kwanza yapasa ujue kwamba pamoja na dawa ni lazima uchunge diet yako. Kwa vile majibu ya endoscopy yanathibitisha tatizo lako basi unatakiwa upate milo midogo midogo ambayo haina pili pili wala mafuta kwa wingi mara kwa mara. Kama unavuta sigara na kunywa pombe inakubidi kuacha kabisa. Na uanze kutumia PPI Kama vile Omiprazole ua Pantoprazole kidonge kimoja mara mbili kwa siku. Usitumie machungwa, Mananasi, Ndimu na Malimau. Fanya mazoezi mepesi kila siku kufanya mzunguko mzuri wa damu na lala mapema. Usijihusishe na mambo yatakayo kufanya uwe na fikra. Iliobaki ni juhudi yako kufwata masharti ya daktari. Kidonda cha tumo kama kisiposhughulikiwa na matibabu yaweza kugeuka Cancer. Nakutakia kila la kheri
   
 13. middo

  middo JF-Expert Member

  #13
  Jan 4, 2012
  Joined: Mar 21, 2011
  Messages: 204
  Likes Received: 20
  Trophy Points: 35
  Pole sana, 0717392103 ni namba ya doctor Scola jaribu kuwasiliana nae atakusaidia. Mtafude mida ya jioni ndo huwa mara nyingi yupo free. Ugua pole
   
Loading...