Naomba ushauri, wazazi wangu hawataki nisome ujuzi mwingine zaidi ya taaluma niliyosoma

The best solution kwake ni either akomae na upishi au arudi Law school IMO
 
Natafuta sehemu uliyoongelea mahusiano sioni, huo umri wa kufait njoo tulianzishe pamoja ili usine tena fika muda ukaanza harakat za kusaka mwenza!
Njoo tuhusiane kiuchumi, kiroho, kifuture, kimalengo na kimikakati
 
Natafuta sehemu uliyoongelea mahusiano sioni, huo umri wa kufait njoo tulianzishe pamoja ili usine tena fika muda ukaanza harakat za kusaka mwenza!
Njoo tuhusiane kiuchumi, kiroho, kifuture, kimalengo na kimikakati
Asante, unaweza kutafuta kwingine
 
Mkuu do what your heart tells you. Lakini make sure hata kama wazazi hawatakubaliana na maamuzi yako, utakuwa na amani na kile unachoenda kufanya. Ni vizuri kuwa na taaluma zaidi ya moja, hasa kwa maisha ya sasa. Vilevile hakikisha unachoenda kukifanya basi kitakusaidia kupata kipato kitakachoweza kuendesha maisha yako. All the best.

Mama pretty
 
Hivi jamani hata kwenda driving school napo inabidi wazazi wako ndio wakupe ruhusa??

We labda unategemea ada kutoka kwao ila kama unajilipia unatakiwa kuwapa taarifa tu kuwa unasomea driving, na ratiba yako itakuaje umemaliza.
 
Sikia dogo wkt mwingine wazazi wanarogwa. mie kwa mfano nilisepa kivyangu kwa kozi nayoitaka kufika kulechuo bana nikawa mpiga picha mzuri tu!....rovin' photographer! basi nikasoma weeeeee!! bila salamu kuwapa!!

nKamaliza nkafanya kazi nkamaliza nikaenda tena chuo kikuuu!! ndo wakajua kwa mbaaali hilo toto liko UDSM, wakalewa mpaka leo!
 
wangekua wananipatia majitaji yangu muhim and mind you miaka takribani 6 sipo nao mkoa mmoja, kwa hiyo ningeamua kufanya ushenzi ningefanya tu ila najiheshimu.
Hapo ndo huwaga nachokaga kabisaaa!!........wao km wao! wakikupa karo ya shule ni kitu kikubwa saaaana!! mengineyo ni wewe mwenyewe!! ..kuwafanyia ushenzi unajikomoa weye mwenyewe kabisaaa bila chenga!

ukitenda mazuri ni weye mwenyewe kabisaaa bila chenga!! huwakomoi wao utapo kuwa unazunguka na Dunia mpaka unalia poo!,....wao hawapo hapo ungewakumbuka mpaka ulie pooo!! kwa akili hizi za kuwakomesha sizo kabisa!..tena ushukuru mara kumi ziliondoka na zaka utoe!

Hao ukipata kazi wape wale/wanywe mpaka wasaze!! na kila wakikuhitaji uwe na kimberembere km chote yaani wa kwanza kufika utoe zaidi ya walivyo toa.......... mengine yooote fanya kufuta ...uone maajabu ya Dunia

utakavyo iweka mkononi mwako mpaka ushangae hata ukipita majani hayo hayoo!! yanakupa shikamooo Mama pretty!...njia rahisi ya kusahahu mabaya yao ni kuwa wewe mama pretty Jifanye km walikuwa wana kufundisha kujitegemea!
 
Du…kisa cha kushangaza hiki.
Lakini kama wewe ni dada, wa kulaumiwa sana ni mama yako.
Hana ukaribu na wewe.
Yote unayojifanyia ni ya kawaida kabisa kwa binti, ila unakosa ule ukaribu wa kusikilizwa.

Wazazi wengi wanawapoteza watoto wao kwa hali kama hii, huyu dogo akipata mshawishi atakayemghilibu akili, hata ruhusa hataomba.
Utasikia tu binti katoweka nyumbani.
Muhimu binti uongee na mama yako kwa undani na umweleze hisia zako.
Asipokusikiliza bado, waambie wazazi uwaombe baraka zao na uendelee na maisha yako.
 
Ndio hivyoo
 
Nimeshajifunza.. asante 🙏🙏
 
Nlipata wakati wa kuzungumza nao tena.. wakanielewa.. kwa sasa naishi kivyangu na nlivyokuwa natamani nimeshaanza kutimiza... 🙏🙏
 
umeshaswma kwao ni familia flani ya kawaida na kama unavyojua familia zetu za kiswahili hizi zilivyo,

ukiwaambia umepata kazi huwa wanategemea makubwa sana , sasa huoni kama bado itakuwa ngumu kwake?

sababu akiondoka tu nyumbani baada ya mwezi utaskia tunaomba pesa ya luku , mara oooh mwezi ujao jitahid basi utununulie madirisha mawili tumalizie chumba flan kumbe we uko ulipo huna kazi wala nini unaunga unga tu maisha
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…