Naomba ushauri, wazazi wangu hawataki nisome ujuzi mwingine zaidi ya taaluma niliyosoma

Mama pretty

JF-Expert Member
May 1, 2020
1,832
3,479
Wakuu habari,

Kama kichwa cha uzi kinavyosema hapo. Mtanisamehe mimi sio mwandishi mzuri ila nitajitahidi nieleweke.

Mimi nimebahatika kusoma systematically kama ilivyo mfumo wa elimu wa Tanzania, yani kuanzia std7, f4, f6 mwisho chuo kikuu.

Sasa kipindi nimemaliza f4 wakati nasubiri matokeo niliwaomba kuwa nikasome hotel management kwa sababu shule niliosoma tulikuwa tukisoma cookery ambayo naipenda na kwenye kupika mash'Allah si haba, nikaona vyema niende kupata ujuzi zaidi lakini nilipopeleka hili wazo nyumbani walinikatalia kwa kunipiga chenga mpaka muda ukaisha and mind you, kipindi hicho nipo tu nyumbani sina issue na ukiomba pesa hupewi.

Japokuwa nilikua najiwekea akiba zangu yani mfano nikipewa elfu 3 ya shule nlikua natoa buku yani hiyo buku ni nauli pamoja na kula shule then elf 2 ndo akiba yangu kwa hiyo kwa wiki nlikua natunza sh. elf 10 ambayo ilikua inanisaidia matumizi yangu. Nikiri kusema kuwa material things mbalimbali nilikua najinunulia mwenyewe .. sijawahi kuomba nyumbani pesa yoyote ya matumizi yangu ya kike zaidi wazazi wangu walikua wanajua kulipa tu ada pamoja matumizi ya shule!

Najaribu tu kufupisha, baadae nikawaomba niende nkasome certificate& diploma ndipo niende chuo kikuu walinikatalia tena wazi sio kwamba nilikua sijitambui lakini nature ya familia yangu ina tabia ya kudharau mawazo ya mtu bila kuyapima ..nkasema anyway kwa kuwa bado nipo chini yao na ninawategemea wacha tu niwaskilize, kwa hiyo nikaenda boarding school!

Nikafaulu tena kujiunga na chuo kimoja hapa Tanzania, niliomba mkopo ila sikupata kwa hiyo ada nikawa nategemea wazazi wangu pamoja na matumizi, wakati wote huo hakuna anaejali kuwa mimi ni mtotonwa kike nina mahitaji mengi.. nkasema fresh...

Nikaanza semester ya kwanza maisha magum, nikachekecha akili nilikua nna dada ambae tumesoma wote A level alikua anakaa nje ya hostel za chuo..
Nikamuomba niwe napikia jiko lake na gesi ikiisha mimi nitagharamia kuijaza akakubali..
Kwa hiyo nikawa natangaza menu ya chakula watu wanaweka oda mida ya kuanzia saa 9 mchana napika kwa ajili ya hizo oda maana nilifanya kwa jioni tu ili ratiba yangu ya darasani isiharibike kwa hiyo nikaanza taratibu kujitegemea completely..

Baada ya muda fulani nkatafuta chimbo la viatu nkapata nikawa nachukua viatu nazungusha hostel za chuo na nje ya chuo nikiwa na rafiki yangu wakati mwingine tunafanya biashara mseto yani hatujastick kwenye biashara moja.

At least maisha yakawa yanaenda, baadae tulitakiwa kuishi nje ya hostel za chuo, nikafanikiwa kununua godoro pamoja na kitanda, nikapata na chumba ambacho kipo affordable nkapanga.

Tukaanza semester nyingine, baba alikua akinipa ada nusu semester na kama kuna michango mingine atatoa yote. Basi hiyo semester nikatoa kiasi kidogo cha ada nikannua vitu muhim vya ndani nkawa napambana kuirudisha hivyo hivyo as usual mpaka nkamaliza chuo ndo yakiwa maisha yangu ya kujitafutia.

Sasa mwishoni nakaribia kumaliza, nilikua nmepanga kuwa nitimize baadhi ya malengo yangu ya kusoma ujuzi tofauti kidogo.
Kuna ndugu yetu yupo mkoa jirani na nilipokua tulikua tukiwasiliana aliposikia npo hapo jirani, kuna kipindi alinisaidia PC yake ya kazini baada ya kuibiwa ya kwangu ambapo pia sasa nimemaliza matumizi yake inabidi niirudishe. Kwa hiyo nilimuomba anisaidie nikienda nipate mafunzo ya udereva akakubali, nikawataarifu nyumbani kuhusu hilo jambo wakakubali pia.. lakini ajabu ilipokaribia kuondoka wakanizuia kuwa hakuna kwenda huko tena! Nikiwauliza sababu wanajiumauma! Nawajua vizuri! Niliumia ila sikua na jinsi zaidi ya kuwasikiliza.

Huyo ndugu yetu yupo kwenye system ambapo niliongea nae pia akaniahidi kuweza kupata sehem ya kujishikiza kulingana na taaluma yangu ya chuo, kwa hiyo hilo pia likayeyuka!

Yote kwa yote wazazi wangu hawafaham changamoto ninayopitia kwan nimekua mtu mkimya nisieongea nayopitia kutokana na kunionesha kutoguswa/kujali hivyo ni tabia yangu kunyamaza tangu nikiwa mdogo. Na nina siri nyingi sana sina mtu wa kumueleza.

Wakati mwingine nawashangaa watu wanasema wanapenda wazazi/mama zao au wapo nao karibu kiasi wanaweza kuwaambia kila kitu ila kwangu ni tofauti😥 sijui kama kuna upendo wa namna hiyo kwangu😫 kwa hiyo vutu vingi napitia kimya kimya mpaka natatua changamoto zangu peke yangu.

Anyway nisiwachoshe , ushauri naoomba ni huu.

Kwa sasa nina akiba kiasi ninayoweza kujisomesha udereva je niende? Maana nimerudi nyumbani sina nachofanya zaidi ya kusengenywa na wazazi wangu😪

Kingine kwa sababu ninavyo vitu vya kuanzia maisha na ramabi at least ninayo, je niondoke nyumbani nikapange niendelee kujitafutia? Maana nipo in the middle of 20's.. naona nyumbani pameanza kunilemaza kiaina.

Nawaheshimu wazazi wangu ila kwa baadhi ya maamuzi yangu watanisamehe. Nishaurini hapo. Nina mengi sana labda nitapata kuyasema wakati mwingine nipunguze uchungu wangu.
 
Wakuu habari,
Kama kichwa cha uzi kinavyosema hapo. Mtanisamehe mimi sio mwandishi mzuri ila nitajitahidi nieleweke.

Mimi nimebahatika kusoma systematically kama ilivyo mfumo wa elimu wa Tanzania, yani kuanzia std7, f4, f6 mwisho chuo kikuu.

Sasa kipindi nimemaliza f4 wakati nasubiri matokeo niliwaomba kuwa nikasome hotel management kwa sababu shule niliosoma tulikuwa tukisoma cookery ambayo naipenda na kwenye kupika mash'Allah si haba, nikaona vyema niende kupata ujuzi zaidi lakini nilipopeleka hili wazo nyumbani
Unakumbuka hii wakati unamjibu Smart911 :

Nmetaka kupata maarifa tu.. mbona nipo nae jamani😂
Ref: Uhalali wa cheti kutoka Marriage Conciliation Board ni upi?
 
The fate of your life is in your hands. Use your mind well do what you want while respecting your parents and also try to educate them with metaphors for example using your friend's example etc.

You could say he studied something and stayed at home for 2 years but when he went to study something he got a job or became self-employed. etc
 
The fate of your life is in your hands. Use your mind well do what you want while respecting your parents and also try to educate them with metaphors for example using your friend's example etc.

You could say he studied something and stayed at home for 2 years but when he went to study something he got a job or became self-employed. etc
Nashkuru sana.
 
. Na nina siri nyingi sana sina mtu wa kumueleza.
Mimi nipo unaweza niambia... kidding..!
Hapo nilichoona Mimi wewe kuwa mtoto wa kike wazazi wako wanaangaika usalama wako kwanza ila pia inaonesha uchumi wa home ni wakawaida nikushauri tu.. km unataka kutoka hapo ni wazo nzuri unaweza kuwaambia kumepata part-time job mkoa x ukaondoka zako hapo kwa amani na wakakupa baraka zao ni muhimu Sana..

Ila ukitoka hapo ukatulie huko upambane kweli.
 
Mimi nipo unaweza niambia... kidding..!
Hapo nilichoona Mimi wewe kuwa mtoto wa kike wazazi wako wanaangaika usalama wako kwanza ila pia inaonesha uchumi wa home ni wakawaida nikushauri tu.. km unataka kutoka hapo ni wazo nzuri unaweza kuwaambia kumepata part-time job mkoa x ukaondoka zako hapo kwa amani na wakakupa baraka zao ni muhimu Sana..

Ila ukitoka hapo ukatulie huko upambane kweli.
Kwa akili za hao wazazi lazma watataka mkoa anaoenda kuwe na ndugu kama hamna watamgomea asiende kabisa😅
 
Hivi udereva si unaweza tu kwenda asubuhi ukarudi mchana ukiwa hapo hapo nyumbani? Kama unalipia mwenyewe sasa kwanini uombe? Uko mkoa gani? Mimi nakushauri kama una hoby bado ya kupika nenda kasome hiyo taaluma halafu anza hiyo biashara, wazazi watakuja kuku support baadae. Wewe ndio mwenye maono ya maisha yako, wao ilikuwa ni kukusomesha tu, baada ya hapo ni wewe, akili na nguvu zako. Support watakupa wakiona juhudi na mafanikio yako.
 
Mimi nipo unaweza niambia... kidding..!
Hapo nilichoona Mimi wewe kuwa mtoto wa kike wazazi wako wanaangaika usalama wako kwanza ila pia inaonesha uchumi wa home ni wakawaida nikushauri tu.. km unataka kutoka hapo ni wazo nzuri unaweza kuwaambia kumepata part-time job mkoa x ukaondoka zako hapo kwa amani na wakakupa baraka zao ni muhimu Sana..

Ila ukitoka hapo ukatulie huko upambane kweli.
Nashkuru mkuu, ila kama wangekua wanajali usalama wangu wangekua wananipatia majitaji yangu muhim and mind you miaka takribani 6 sipo nao mkoa mmoja, kwa hiyo ningeamua kufanya ushenzi ningefanya tu ila najiheshimu.

Kuhusu kuondoka home, siwezi kuondoka kienyeji lazima niongee nao kwanza nawaheshimu tu.
 
hivi udewreva si unaweza tu kwenda asubuhi ukarudi mchana ukiwa hapo hapo nyumbani? Kama unalipia mwenyewe sasa kwanini uombe? Uko mkoa gani? Mimi nakushauri kama una hoby bado ya kupika nenda kasome hiyo taaluma halafu anza hiyo biashara, wazazi watakuja kuku support baadae. Wewe ndio mwenye maono ya maisha yako, wao ilikuwa ni kukusomesha tu, baada ya hapo ni wewe, akili na nguvu zako. Support watakupoa wakiona juhudi na mafanikio yako.
Asante kwa ushauri ndugu
 
Back
Top Bottom