Naomba ushauri wa kupata simu ya nzuri za iPhone

Mkuu chukua iPhone 7 Gb 128 ni simu nzuri sana unapata IOS updates zote hadi latest 14.5 pia ina high processing speed na 2gb Ram.
Charge inakaa kutwa nzima ukiwa online Mda wote with 4G network.

Kinging apple wana real phone specification.
Eg.
retina camera, jinsi macho yako yanvyoona kitu ndio picha ya iPhone ikionyesha

Real Ram, iPhone huwezi kuta ina stack au ku load kitu kwa muda mrefu kama android

Lakini Android huwa simu zao wana label specifications yaan unakuta simu specification kubwa lakini uwezo au uharisia zero kabisa.

Mimi natumia iPhone 7 gb 128 na jamaa yangu anatumia sumsung kubwa tu kam A10 au A20 tulizilinganisha uwezo wa processing power ya internet

Tukachukua laptop yenye Ram 8gb na processor core i3 Tuka connect WIFI kwa kutumia simu yake ya Samsung aisee pc iko slow kwenye internet Kama kobe

Then tuka disconnect na ku connect iPhone 7 yangu 4G network aisee yaani ukigusa link faster pc ina open.
Na wote tulitumia chip ya Vodacome 4G

Baada ya hapo jamaa akaamini iPhone wapo realistic kuliko android wao wana label specification lakini uwezo halisi wa simu zero.
Kwa hiyo achane kuofananisha iPhone na simu za kijinga.
A10 wala a20 sio sawa kuilinganisha kuna a71 gusa utupe hiyo iphone
 
SoC by definition ni System on Chip. Kwa technology ya simu ilivyo hii SoC ndio chip inayocontain CPU ya simu, Modem ya simu (kwaajili ya network), Image signal processor au ISP (hii ndio ina fanya process zote za kuchukua picha kutoka kwenye camera na kuprocess kuwa nzuri), Graphic processing unit au GPU (hii ni kwa ajili ya vitu vyote vinavohitaji nguvu ya kuprocess graphics zake kma games na baadhi ya apps), Artificial Intelligence processors, audio and video decorder zinawezesha kuplay audio na video za format mbali mbali na zingine zina hata RAM humo humo.

Sasa hapo umeona kuwa SoC ina kuwa na vitu vyote hvyo, ikiwa weak basi na hvyo vitu vyote hapo vitakua weak.
SoC za simu zinatoka kwenye company mbali mbali lakini zinazofahamika sana ni Qualcomm, Exynos, MediaTek, Spreadtrum, Apple A series na Hisilicon

Apple A series ndio the best of the best kwenye performance ya CPU na GPU. SoC ya Apple ya mwaka husika ukilinganisha na SoC ya Qualcomm kwenye mwaka huo mara nyingi za Apple zinakuwa na CPU na GPU performance kubwa kidogo kuliko za Qualcomm.

Kwa upande wa Android Qualcomm ndio wanatengeneza SoC nzuri kuliko wote wakifatiwa na Exynos ya Samsung and Hisilicon ya Huawei. MediaTek nao wanatengeneza SoC nzuri ila sio sana na wanajulikana kwa kuwa na SoC mbaya za bei ndogo ndio unazoziona kwenye Tecno, Infinix, itel, masimu ya kichina na simu za bei rahisi kutoka kwa Xiaomi na Samsung (kma hzo A10).

Lakini pia kila company ina category mbali mabli. Low end, midrange na high end. Hizi SoC zina majina yake. Kwa mfano ukichukua simu kma Samsung Galaxy S20 zinakuwa na SoC ya Qualcomm Snapdragon 865 or Exynos 990. Hizi ni flagship SoC zenye uwezo wa hali ya juu. Lakini simu kama Samsung Galaxy A10s ina SoC ya MediaTek Helio P22 ambayo ni ndogo na haina uwezo mzuri.

Kujua SoC ya simu yako tumia app ya DevCheck au Device Info HW na angalia kundi la Hardware or SoC utaona jina la SoC ya simu yako. Pia unaweza tafta SoC ya simu online kwa kuangalia specification zake.

Ukishajua jina la SoC basi unaweza linganisha na SoC ya simu nyingine kujua zinazidiana vipi uwezo. Kwa mfano mimi simu yangu ina Snapdragon 855 nataka nilinganishe na Samsung Galaxy A51 yenye Exynos 9611. Nitaingia Google kisha nitaandika Snapdragon 855 vs Exynos 9611 kisha utachagua website ya nanoreview.net au versus.com na kusoma tofauti zake na ipi inamzidi mwenzake.
View attachment 1776875
Big up.. mkuu
 
Mdau kakujbu hapo chini, ila kununua iphone 7 ni bora tu ununue simu ya android yenye latest android OS. Kwanza simu kama iPhone 7 haikai na charge sana pia huifaidi iOS 14 vya kutosha. Walau ununue hata iphone Xr

na vipi kuhusu 7+ ????
 
Uzi mzuri sana. Samsung simu nzuri sana sema ikipasuka kioo bahati huna na utalia bure.
Nilikua na iphone 7,google 2xl na galaxy note 10 plus.
Galaxy note 10 plus imepasuka kioo nimeambiwa ni 720 kioo, nimeamua kuiweka ndani nimeongeza iphone 8 kwenye list na kwakweli sijutii.
Camera bomba,charge inajitahidi kulinganisha na iphone 7,napata muda vizuri wa kuedit pics,kufanya kazi za office mpaka nasahau kutumia laptop wala ipad,kwa ujumla mimi ni heavy user ila iphone 8 nimeipenda.

Nashauri anunue kama ni iphone kuanzia 8 ataona kitu,seven hapana View attachment 1776648
View attachment 1776649

vipi 7 plus mkuu
 
vipi 7 plus mkuu

7+ iko Okay si unajua kuna atleast okay, okay na kuna Great kwahyo 7+ iko “okay” Maana kwa Camera ndio Potrait Nzuri inaanza kwa 7+ na kuendelea ila Charge sio sana Kama ni Heavy user kwa siku unachaji mara mbili
tip: usizimezime data ukizima data na kuwasha ndio unamaliza charge faster acha data on itakaa muda mrefu zaid
 
7+ iko Okay si unajua kuna atleast okay, okay na kuna Great kwahyo 7+ iko “okay” Maana kwa Camera ndio Potrait Nzuri inaanza kwa 7+ na kuendelea ila Charge sio sana Kama ni Heavy user kwa siku unachaji mara mbili
tip: usizimezime data ukizima data na kuwasha ndio unamaliza charge faster acha data on itakaa muda mrefu zaid
hapo nimekuelewa mkuu ngoja tutafute duka la iphone week ijayooo,,,

na kwenye swala la kujaaa CHAJI vipi si huwa hauchukuii mda au ndo ile unalaza mpaka kesho
 
hapo nimekuelewa mkuu ngoja tutafute duka la iphone week ijayooo,,,

na kwenye swala la kujaaa CHAJI vipi si huwa hauchukuii mda au ndo ile unalaza mpaka kesho

Haipo kama simu za siku hizi dkka 45 imejaa sema inajaa faster tu, kawaida
 
7+ iko Okay si unajua kuna atleast okay, okay na kuna Great kwahyo 7+ iko “okay” Maana kwa Camera ndio Potrait Nzuri inaanza kwa 7+ na kuendelea ila Charge sio sana Kama ni Heavy user kwa siku unachaji mara mbili
tip: usizimezime data ukizima data na kuwasha ndio unamaliza charge faster acha data on itakaa muda mrefu zaid
mmmh yan data on inakaa zaid

Hii ipoje?
 
Ni simu zilizorekebishwa kurudishwa katika hali ya upya. Kwa mfano zinawekewa battery mpya, kioo kipya kma kilikua kimepasuka, housing mpya kama ilikua imechubuka sana, nk. Na refurbished zina madaraja yake yenye quality tofauti.

Mfano Grade A zinakua na original parts tu kutoka kwa Apple (hizi Grade A zinafanywa na Apple wenyewe au macompany waliyoruhusu).

Grade B zinakua na parts kutoka kwa companies zinazotengeneza spares, hizi zinakua na spares za quality nzuri.

Grade C zinakua na spare za low quality, ndio zile iPhone unakuta kioo kina quality mbovu sana na camera zake sio quality nzuri.

Bongo hapa nyingi ni Grade B and C. Bora ukipata Grade B ndio zinakua ziko vizuri tu. Grade C ni majanga. Kuijua unaangalia tu quality ya kioo. Ukiona kina quality kma ya Tecno ya laki mbili kaa mbali nayo.

Umeongea kweli tupu kwa kufupi China plaza na kkoo kwa umla hapafai kuna simu vimeo sana hizi iPhone sina hamu
 
mmmh yan data on inakaa zaid

Hii ipoje?

Yaan Best ni utumie Wifi, Kama haiwezekan tumia data ila ukiwa unatumia data mara kidogo unazima then dakika 5 umewasha simu haijatulia ukazima tena mara unawasha kuna watu wanafanyaga hivyo, ukifanya hivi unadrain battery faster either zima data completely tumia wifi au acha data on zima background apps iPhone yako ita survive mda mrefu
 
Back
Top Bottom