Naomba ushauri wa kupata simu ya nzuri za iPhone

KAGAMEE

JF-Expert Member
Dec 20, 2013
1,290
2,000
Habari zenu wakuu,

Naomba msaada wa kujua aina gani ya Iphone ni nzuri ambayo bei yake ni kati ya laki 5 mpka laki 6? Simu ambayo ina storage kubwa (64GB above) na camera yake ni nzuri. Itapendeza zaidi nikipewa chimbo zuri la kuipata Dar.

Asanteni.
 
Nafaka

JF-Expert Member
Feb 17, 2015
5,861
2,000
Habari zenu wakuu.Naomba msaada wa kujua aina gani ya Iphone ni nzuri ambayo bei yake ni kati ya laki 5 mpka laki 6?.Simu ambayo ina storage kubwa (64GB above)na camera yake ni nzuri.Itapendeza zaidi nikipewa chimbo zuri la kuipata dar.

Asanteni.
Mdau kakujbu hapo chini, ila kununua iphone 7 ni bora tu ununue simu ya android yenye latest android OS. Kwanza simu kama iPhone 7 haikai na charge sana pia huifaidi iOS 14 vya kutosha. Walau ununue hata iphone Xr
 
Champagnee

JF-Expert Member
Jan 12, 2019
5,659
2,000
Ukiataka brand new kwa sasa utapata kuanzia iphone xr, iphone11, na 12 series zingine ni refurb tu
 
KAGAMEE

JF-Expert Member
Dec 20, 2013
1,290
2,000
iPhone 7 plain Refurbished unapata kwa hiyo (hakuna iPhone 7 mpya kutoka kwa Apple sshv). Maduka kibao tu kule Sinza yanauza. Jua tu ni refurbished
Asante.But nieleweshe unaposema refurbished una maana gan?
 
The Knowledge Seeker

JF-Expert Member
Apr 13, 2019
1,091
2,000
Mdau kakujbu hapo chini, ila kununua iphone 7 ni bora tu ununue simu ya android yenye latest android OS. Kwanza simu kama iPhone 7 haikai na charge sana pia huifaidi iOS 14 vya kutosha. Walau ununue hata iphone Xr
Kama hana mambo mengi joh ni sim poa sanaa, ila kama anajijua n mtu mwenye mambo mengi tafuta android yako yenye specifications nzuri ui enjoyed maisha
 
Kennedy

JF-Expert Member
Dec 28, 2011
28,259
2,000
Asante.But nieleweshe unaposema refurbished una maana gan?
Ni Simu Iliyotumika Huko Ughaibuni Kwanza Halafu Ndiyo Inaletwa Hapa Tanzania Ikiwa Wakati Mwingine Na Kila Kitu Chake!!!

Sasa Inategemea Unaweza Kuipata Ikiwa Na Hali Nzuri Kila Idara Ama Kinyume Chake.
Chukua Ushauri Wa Wataalam Wa Hapo Juu
 
racka98

JF-Expert Member
Jul 7, 2020
981
1,000
Asante.But nieleweshe unaposema refurbished una maana gan?
Ni simu zilizorekebishwa kurudishwa katika hali ya upya. Kwa mfano zinawekewa battery mpya, kioo kipya kma kilikua kimepasuka, housing mpya kama ilikua imechubuka sana, nk. Na refurbished zina madaraja yake yenye quality tofauti.

Mfano Grade A zinakua na original parts tu kutoka kwa Apple (hizi Grade A zinafanywa na Apple wenyewe au macompany waliyoruhusu).

Grade B zinakua na parts kutoka kwa companies zinazotengeneza spares, hizi zinakua na spares za quality nzuri.

Grade C zinakua na spare za low quality, ndio zile iPhone unakuta kioo kina quality mbovu sana na camera zake sio quality nzuri.

Bongo hapa nyingi ni Grade B and C. Bora ukipata Grade B ndio zinakua ziko vizuri tu. Grade C ni majanga. Kuijua unaangalia tu quality ya kioo. Ukiona kina quality kma ya Tecno ya laki mbili kaa mbali nayo.
 
Extrovert

JF-Expert Member
Feb 29, 2016
36,660
2,000
Mdau kakujbu hapo chini, ila kununua iphone 7 ni bora tu ununue simu ya android yenye latest android OS. Kwanza simu kama iPhone 7 haikai na charge sana pia huifaidi iOS 14 vya kutosha. Walau ununue hata iphone Xr
Hahaha unampotosha mie niliamua kujaribu Iphone almost nina week ya 3 ni iphone 6S!

Niliagizisha ya soko la Canada! Iko freshi sana yani na ukizingatia nilikuwa natumia li Itel jamani tofauti yake na Iphone ni kama usiku na mchana! Kwanza iOS iko smooth kuliko android interms of loading apps! Natumia 1xbet kwenye android it was taking a lot of time kusubirie iload ila kwa iOS nikugusa tu kitu mwaaah! Mbali na yote natumia iOS 14 ambayo unasema hataipata na juzi wamentumia iOS 14.5 update ya GB1 sema sijaidownload bado!

Kwa support ya software pia naona iPhone wako vizuri sababu simu ya mwaka 2016 kupata support kwa miaka mitano mfululizo sio jambo dogo! Hamna android ya 2016 inayopata update ya OS current, labda utumbukize Rom za kudownload uchochoroni!

Kitu cha kiboya kuhusu Iphone ni power management tu! Aisee hii simu kabla sijatoka lazma nihakikishe iko na 100% kwanza walau ndio naweza survive nayo ila bila hivyo itazima kabla sijarudi home!

Nikiwa nafanya full matumizi naweza kuchaji mara 3 kwa siku kitu ambacho kwenye android phones kimetatuliwaga muda mrefu tu! Hawa jamaa sijajua kwenye yale ma Iphone kuanzia X na kuendelea ila haya matoleo kuanzia iPhone 8 plus kuja chini ni uongo! Battery health inasoma 100% ila simu haikai na chaji inaboa sana hasa kwa sie ambao simu hazibandukagi mikononi!
 
mkorinto

JF-Expert Member
Jun 11, 2014
22,535

uko sawa kabisa,lakini kuichallenge ios kwa kutumia android ya kwenye itel,ni kosa kubwa tena unatakiwa ukamatwe ufunguliwe kesi ya uhaini.

iphone ni simu nzuri sana,lakini kuna vitu utavikosa kama utatafuta hizo zetu za miaka hiyo.kwa sasa ili uepuke kero hiyo ya charge angalau unatakiwa uwe na iphone x max kwenda juu,napo bado huwezi linganisha na majini ya A series ya samsung,ambayo anaweza pata kwa nusu bei na akasahau kabisa stress za tanesco.

simshauri kununua iphone 7,8,wala 6s plus kwa sasa,hatafurahia simu yake.maana atanyanyaswa mpaka na watumiaji wa infinix kwa charge.kama amefikisha huyo 500k hawezi kosa 1mln.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom