Mambo vp Wana JF,nahitaji ushauri wenu kwenye hili............!!
Ni mwaka sasa umepita toka nianze mahusiano na huyu msichana.Wakati tunaanza mahusiano alikua akiishi hostel za chuo chao but after miezi mitatu akaniambia anahamia kwake kwani mama yake kamkubalia kumpangishia nyumba.Baada ya kuhamia kwake kama mwezi ukapita nikaenda kumtembelea kwake palinishtua kidogo alikua amepanga zaidi ya chumba kimoja kama nilivyofikiri nyumba ilikua na Sebule,jiko,chumba cha kulala na pia alikua na vitu vya ndani vyote ikiwa mziki mkubwa,tv-flat,masofa,kabati n.kIlinishtusha kwamba mama yake ampangie ghafla hivyo na vitu vyote vya gharama hivyo but alinihakikishia ni mama yake na kunihakikishia zaidi mama yake alikua akija kumtembelea ananitumia mpaka picha.Wakati huo wote mimi pia nlikua nikiishi kwangu tho pia nlikua nasoma chuo.Alifanya sherehe ya kuhamia kwake na alialika marafiki zangu na marafiki zake wachache pia but marafiki zangu walishtuka baada ya kupaona kwake but niliwaambia ni mama yake na huwa anakuja mara kwa mara so wakaamini hivyo kwa shingo upande.
Ki ukweli ananipenda sana kiasi kwamba kwenye watsup dp yake ananiwekaga mimi tu mda wote na instagram full kuweka picha zangu na ujumbe wa mapenzi kuonesha ulimwengu ananipenda sana.Nikajiaminisha napendwa sana.Kwa sababu kwangu nipadogo(chumba kimoja) aka ning'ang'aniza ni hamie kwake.Nika hamia tho niliamia na rasket tu vitu vingine vilibaki kwangu na niliendelea kulipa kwangu kodi tho nimehamia kwa demu tyr.
But juzi akaamua kuniapasualia ukweli wote tukiwa kitandani.Kuwa kwao maisha ni ya chini sana tofauti na ninavyomuona na jamii inavyomchukulia pia kwao hawawezi ata kumlipia ada ya shule na matumizi tofauti na nlivyokuwa nafikiria kabla. Baada ya miezi miwili ya kuaanza mahusiano yetu alifukuzwa chuo kwa kukosa ada baada ya ndugu aliyekua anamsaidia kutofautiana nae na baada ya hapo alikutana na mbaba flani ambae alimuonea huruma na kuamua kumlipia ada na hela ya matumizi kama mwanae.Lakini eti baada ya miezi mitatu yule mbaba akampeleka nje kidogo na jiji na kulala nae mchana kwa hoteli na wamesha lala mara nne toka wakutane sasa ikiwa ni karibu mwaka na vitu vyote vya ndani,ada na hela tunazokula sio za mama yake ni za huyo mbaba.Na ananiambia hayo yote coz ananipenda sana na anataka kuachana na huyo mzee coz karibu anamaliza chuo na ameshamlipia ada tayari.Ndugu nilihisi naota ndoto kumbe ilikua ni kweli nilishindwa kumjibu mpaka leo na jibu sina.Ni kamuuliza mbona mama yako alikua anakuja kwako akaniambia mama yake anajua pale ni kwangu na nilikua nimesafiri .
Wana JF naomba ushauri nimkimbie,nimvumilie tho sina hela zakumpa akiachana na huyo mtu wake,ama nifanye nn.........????
add: Tumeshapima afya zetu wote tupo wazima.Na bibie anaforce kumwambia huyo mzee waachane sasa nafikiria wakiachana nani atampa hela ya matumiza kila siku mimi sina hizo hela???