Naomba Ushauri, nataka kurudi shule nikasome Master's

May 8, 2018
95
125
Wadau ninaomba mchango wenu wamawazo. Nimekua mtumishii wa serikali kwa miaka minne Sasa, katika idara ya elimu(Mimi ni mwalimu) umri miaka 28.

Nafundisha masomo ya physics na chemistry, na ninayo elimu ya bachelor yenye GPA nzuri tu.

Nimeamua kutaka kurudi kupiga kitabu Tena, nafikiri nikasome master hasa ya physics. Ila mpaka saiz bado cjajua field ipi nikachukue

Nimekuja kwenu kupata msaada wa mawazo ili niweze kufanikisha ndoto angu.

Afu pia, Kuna swali najiuliza vipi Kuna manufaa yeyote ninaweza pata baada ya kumaliza master au mifumo ya sikuhizi imekaaje wadau.

Nawakaribisha mchangie kwa chochote.

KARIBUNI.
 
DLS

JF-Expert Member
Feb 18, 2015
240
250
ngoja wazoefu waje wakushauri in details ila with no doubt kwenda kusoma ni muhimu wala usiangalie manufaa ya sasahivi, utumishi wa umma elimu itakubeba, lakini pia hata kwako binafsi usiridhike na degree moja ni sawa na kuwa na mtoto mmoja akifa ndo basi.
Kila la kheri.
 
financial services

JF-Expert Member
May 17, 2017
10,562
2,000
Hongera kwa kupata hamasa ya kwenda kusoma mkuu,ngoja wakuu waje ila je umejaribu kucheki fields zilizopo zenye hiyo physics? Umevutiwa na ipi?
Manufaa kwanza ni kwako mwenyewe utakua educated kiasi cha masters👍pia naona salary haitakua the same namwenye degree bana. All the best
 
The imp

JF-Expert Member
Jul 6, 2012
12,238
2,000
Hongera kwa kupata hamasa ya kwenda kusoma mkuu,ngoja wakuu waje ila je umejaribu kucheki fields zilizopo zenye hiyo physics? Umevutiwa na ipi?
Manufaa kwanza ni kwako mwenyewe utakua educated kiasi cha masterspia naona salary haitakua the same namwenye degree bana. All the best
Labda alambe cheo

Ila serikalinii hakuna mshahara wa masters boss .

Labda kwenye vyuo vikuu .

Otherwise Ni waste of time and money

Pesa ya master afungulie biashara .

Ila kama anae Godfather pale tamisemi au wizara ya elimu sawa Go ahead.
 
black hawk87

JF-Expert Member
Jan 25, 2020
673
1,000
Kusoma Kama unataka kwenda kusoma nenda master's Ni kupoteza muda na pesa fikiria nje ya elimu na kuajiriwa

Umepata nafas ya kupata mkopo kiurahis wekeza tengeneza mifumo Kwanza ya pesa isimame vizuri serikalini hakuna mshahara wa master's Zaid cheo kitakufanya kuwa mtumwa Zaid

Siku hiz ukiwa na degree inatosha kabisa Ni kuwekeza TU hakuna sifa utakayopata kwa ajili ya elimu yako hata familia yako Bali pesa tu ndio itakayo kupa tabasamu na afya njema na heshima popote utakapo simama

Sent from my TECNO B1 using JamiiForums mobile app
 
FineForever

JF-Expert Member
Apr 12, 2017
1,722
2,000
Wadau ninaomba mchango wenu wamawazo. Nimekua mtumishii wa serikali kwa miaka minne Sasa, katika idara ya elimu(Mimi ni mwalimu).

Nafundisha masomo ya physics na chemistry, na ninayo elimu ya bachelor yenye GPA nzuri tu.

Nimeamua kutaka kurudi kupiga kitabu Tena, nafikiri nikasome master hasa ya physics. Ila mpaka saiz bado cjajua field ipi nikachukue

Nimekuja kwenu kupata msaada wa mawazo ili niweze kufanikisha ndoto angu.

Afu pia, Kuna swali najiuliza vipi Kuna manufaa yeyote ninaweza pata baada ya kumaliza master au mifumo ya sikuhizi imekaaje wadau.

Nawakaribisha mchangie kwa chochote.

KARIBUNI.
Kasome "bachelor degree in material science" Mandela University - Arusha... Hutojuta...
 
Heavy Metal

JF-Expert Member
Feb 7, 2017
287

Nelson Mandela hawatoi Bachelor Degree; wanatoa Master's & PhD, Materials Science and Engineering ataikuta; specialization kwenye Structural Materials & Energy Materials;
 
FineForever

JF-Expert Member
Apr 12, 2017
1,722
2,000
Nelson Mandela hawatoi Bachelor Degree; wanatoa Master's & PhD, Materials Science and Engineering ataikuta; specialization kwenye Structural Materials & Energy Materials;
Very true.... Ahsante mwamba kwa info zaidi kwa jamaa yetu ...
 
Heavy Metal

JF-Expert Member
Feb 7, 2017
287
1,000
Wadau ninaomba mchango wenu wamawazo. Nimekua mtumishii wa serikali kwa miaka minne Sasa, katika idara ya elimu(Mimi ni mwalimu).

Nafundisha masomo ya physics na chemistry, na ninayo elimu ya bachelor yenye GPA nzuri tu.

Nimeamua kutaka kurudi kupiga kitabu Tena, nafikiri nikasome master hasa ya physics. Ila mpaka saiz bado cjajua field ipi nikachukue

Nimekuja kwenu kupata msaada wa mawazo ili niweze kufanikisha ndoto angu.

Afu pia, Kuna swali najiuliza vipi Kuna manufaa yeyote ninaweza pata baada ya kumaliza master au mifumo ya sikuhizi imekaaje wadau.

Nawakaribisha mchangie kwa chochote.

KARIBUNI.
Kama GPA yako ni nzuri I mean iko 3.8 and above tafuta nafasi vyuo vikuu then omba kuhamia km Tutorial Assistant; then utaenda kufanya Master's ukishafika huko maana ni lazima
Lakini pia kwa masomo yako kuna taasisi nyingi tu na mashirika ya umma unaweza kufanya kazi; omba kuhamia sehemu km TBS; TAEC; TIRDO; COSTECH (Hii ukiwa na Master's au PhD)
All in all ingia mitandaoni utafute scholarship ziko nyingi tu hata Mandela zipo na za nje ya nchi zipo km ICCR- India, China, DAAD- Germany....., All the best
 
mazojms

JF-Expert Member
Sep 22, 2017
1,499
2,000
Ila mpaka saiz bado SIJAJUA field ipi nikachukue

Nimekuja kwenu kupata msaada wa mawazo ili niweze kufanikisha NDOTO ANGU.

Afu pia, Kuna swali najiuliza vipi Kuna MANUFAA YEYOTE ninaweza pata baada ya kumaliza master.
_ Mkuu upo serious kabisa?
_ Ndoto yako ni nini? maana ndoto unayo lakini field unayoplan kusoma na manufaa ya kusoma huyafaham.
 
May 8, 2018
95
125
Kama GPA yako ni nzuri I mean iko 3.8 and above tafuta nafasi vyuo vikuu then omba kuhamia km Tutorial Assistant; then utaenda kufanya Master's ukishafika huko maana ni lazima
Lakini pia kwa masomo yako kuna taasisi nyingi tu na mashirika ya umma unaweza kufanya kazi; omba kuhamia sehemu km TBS; TAEC; TIRDO; COSTECH (Hii ukiwa na Master's au PhD)
All in all ingia mitandaoni utafute scholarship ziko nyingi tu hata Mandela zipo na za nje ya nchi zipo km ICCR- India, China, DAAD- Germany....., All the best
Asante mkuu
 
Mr Director

Senior Member
May 10, 2015
130
500
All in all usitoke nje ya ulichosomea 1st degree, kasome Master of education...
Faida yake ni rahisi kupata kazi vyuo vya kati na vyuo vikuu...
Kama sasa hivi una GPA nzuri kuanzia 3.8 omba kuwa TA ktk vyuo vikuu within a year utakua umepata...
Kama GPA ipo chini ya 3.8 omba vyuo kati...
BAHATI MBAYA ktk ualimu wa secondary au primary hata usome uwe na phd mshahara wako utafuata scale zilezile kama ulikua D basi utangoja zamu ifike uingie E
 
clecla

JF-Expert Member
Dec 13, 2016
779
1,000
Wadau ninaomba mchango wenu wamawazo. Nimekua mtumishii wa serikali kwa miaka minne Sasa, katika idara ya elimu(Mimi ni mwalimu) umri miaka 28.

Nafundisha masomo ya physics na chemistry, na ninayo elimu ya bachelor yenye GPA nzuri tu.

Nimeamua kutaka kurudi kupiga kitabu Tena, nafikiri nikasome master hasa ya physics. Ila mpaka saiz bado cjajua field ipi nikachukue

Nimekuja kwenu kupata msaada wa mawazo ili niweze kufanikisha ndoto angu.

Afu pia, Kuna swali najiuliza vipi Kuna manufaa yeyote ninaweza pata baada ya kumaliza master au mifumo ya sikuhizi imekaaje wadau.

Nawakaribisha mchangie kwa chochote.

KARIBUNI.
Hakuna manufaa isipokua utaongezewa ngazi mbili za mshahara,, mf Kama uko TGTS D2 utapelekwa TGTS D4,,,,,,zaidi Maningu yataongezeka Sana Kazini,,,nimegraduate MA.ED 2018 najua ninachokiandika
 
clecla

JF-Expert Member
Dec 13, 2016
779
1,000
Labda alambe cheo

Ila serikalinii hakuna mshahara wa masters boss .

Labda kwenye vyuo vikuu .

Otherwise Ni waste of time and money

Pesa ya master afungulie biashara .

Ila kama anae Godfather pale tamisemi au wizara ya elimu sawa Go ahead.
Sure mkuu nime-graduate Master's 2018.....mpka sasa nimeongeza Majungu kazini na uadui na H/M
 
evonik

JF-Expert Member
Jun 12, 2015
2,979
2,000
ngoja wazoefu waje wakushauri in details ila with no doubt kwenda kusoma ni muhimu wala usiangalie manufaa ya sasahivi, utumishi wa umma elimu itakubeba, lakini pia hata kwako binafsi usiridhike na degree moja ni sawa na kuwa na mtoto mmoja akifa ndo basi.
Kila la kheri.
Kwa hiyo degree inakufa?
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom