Nunua vitu vya mwezi mzima, kama huna fridge nunu chakula cha mwezi mzima ila mboga nunua kila week, then usikae na hela mfukoni. Kama hujiamini mpe mtu akuwekee kadi ya bank
Huyo wa kwanza kukupa ushauri ndo alimaliza kila kitu...
Mimi mwenyewe hiyo hali ninayo (nilikuwa nayo) lakini tangu nioe naona kidogo kwa mbali imeanza kupotea potea
Yaani ilikuwa hata niandike bajeti yangu vizuri namna gani aisee PAYE ikitoka tu wiki yangu ni moja tayari sina kitu
Huwa napata taabu sana maana naumiza akili hata sielewi nakwama wapi wakati ukicheki silewi (sio mlevi), sihongi (sio mzinzi), sibeti (sichezi kamari) wala sifanyi jambo lolote la kijinga la kunimalizia pesa yet pesa haikai wala haitoshi
Hatahivyo, kwako hiyo hali naona itachukua muda zaidi yangu kwasababu umesema wewe ni wa kike... nitakwambia kwanini
Inaonesha hela zako una maamuzi nazo wewe mwenyewe na mumeo anashughulikia maswala yote ya hapo ndani kwa kipato chake mwenyewe
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.