Naomba ushauri mke wangu ananisema kwenye What's App

Naomba ushauri mke wangu ananisema kwenye What's App

Labda unajistukia. Kama vijembe unavielewa vitendee kazi. Toka nae mkabarizi mahali, muambie unampenda na umsifie kama anapendeza. Kama huoni anapendeza basi mnunulie nguo uzipendazo afu umsifie nazo.

Hongera kwa sababu mkeo bado anakupenda. Akifika mahali hakupendi hutomsikia akiuliza wala kulalamika, utaona happy status hadi ushangae furaha yake inatoka wapi.
Nashukuru kwa ushauri
 
Wasap status update... Msg sent and delivered kazi kwako sasa!!
 
Ukiona anakusema, jirekebishe. Pua ushukuru kua anakusema kuliko kukaa nalo moyoni
Sasa si bora aniseme kwa kitu nilichofanya kiongozi? Nikimuliza anasema hakuna shida sasa nifanyeje hapo?
 
Kivipi mkuu
Acha kumuogopa na m confront. Majibu yote anayo mkeo. Hakikisha mwisho wa mazungumzo anaelewa wewe sio shabiki wa taarabu za WhatsApp. Ni muhimu mkeo kujua misimamo yako la sivyo kila siku itakuwa shida hapo.
 
Futa namba yake alafu muite selemara akubandikie notice board nje getini uwe unamsema nawe mpaka akome.
 
Back
Top Bottom