Naomba ushauri mke wangu ananisema kwenye What's App

Waterloo

JF-Expert Member
Nov 30, 2010
25,356
38,908
Wadau

Mke wangu ananiwekea message kwenye profile yake kunisema.nikimuuliza kuna tatizo gani ananiambia hakuna tatizo.

Yani nashindwa kumuelewa message za vijembe kama analalamika vile eti simpendi.na mi sina mwanamke nje.

Nifanyeje?
 
Last edited by a moderator:
Yani nashindwa kumuelewa message za vijembe kama analalamika vile eti simpendi.na mi sina mwanamke nje
Inawezekana kweli huna mtu nje lakini Inawezekana hauna mahusiano naye mazuri tena kama ilivyokuwa mwanzoni. Japo hajatumia njia nzuri kufikisha malalamiko yake, ujumbe umeupata so kaa naye chini mzungumze nini ni tatizo.
 
Nawewe Kama Vipi Nenda Kamseme FACEBOOK, TWITTER Au GOOGLE+ Nadhani Ndio Itakua Dawa Yake.
 
Ukiona anakusema, jirekebishe. Pua ushukuru kua anakusema kuliko kukaa nalo moyoni
 
Labda unajistukia. Kama vijembe unavielewa vitendee kazi. Toka nae mkabarizi mahali, muambie unampenda na umsifie kama anapendeza. Kama huoni anapendeza basi mnunulie nguo uzipendazo afu umsifie nazo.

Hongera kwa sababu mkeo bado anakupenda. Akifika mahali hakupendi hutomsikia akiuliza wala kulalamika, utaona happy status hadi ushangae furaha yake inatoka wapi.
 
Back
Top Bottom