Naomba ushauri kunirejeshea hamu ya kuishi

Naomba ushauri kunirejeshea hamu ya kuishi

Dunia Tabu

Member
Joined
Jun 25, 2014
Posts
53
Reaction score
16
Habar Wana JF

Ndugu zangu niko hapa kuomba ushauri utaonipa mwanga wa maisha yangu. Baada ya kuhangaika hatimaye nilibahatika kuajiriwa mamlaka ya bandari.

Nilipata barua yangu ya ajira na kuanza kazi mtwara. Ikapita miezi minne bila kuanza kupata mshahara huku nilioanza nao wakianza kupata. ktk kufuatilia kwangu nikafika hazina ambako janga limenikuta.

Nikaelezwa cheti changu cha frm 4 kimetumika na mtu kaajiriwa yupo ktk system hivyo wao wametuma barua mamlaka husika kusitisha ajira yangu.

Ndugu zangu sijawahi kutoa cheti changu kumpa mtu yeyte na wala huyo simfaham.

Historia yangu nimehitim frm4 2005, Advance 2008, Bachelor UDsm 2011, diploma ya sheria chuo cha uongozi wa mahakama lushoto 2013.

Nikafanya usaili mara 6, ya saba nikapata kazi, leo ndugu zangu naambiwa hivi?

Vyet vyote ninavyo, sina ndugu kusema alitumia, wala sijakitoa kwa yeyote.

Hiv ni kweli ajira nakosa?

Ina maana elimu yangu yote ni bure?

Naomba ushauri nipate hamu ya kuishi.
 
Pole na matatizo kaka cha mm nilikua naomba ungefuatilia kwa makini huko hazina au nenda utumishi wa umma wakupe details kamili za huyo mtu anayetumia cheti chako cha four pia itabidi uende necta kaka ukaelezee hiyo situation yote ili uweze kujua nani anakula jasho lako kaka kirahisi hivyo wakati vyeti unavyo inakuaje hapo itakua necta ndo mchezo ulikochezwa kama kweli haujawah kumpa mtu hicho cheti
 
Kwa nini wasisitishe ajira ya huyo mwingine? Kuna kitu hapo, cha msingi fuatilia vizuri ikishindikana hata mahakamani. Haki ya mtu haipotei, inaweza kucheleweshwa tuu.
 
pole sna fuatilia pale utumishi wana kitengo cha ubora wanadili sana na mambo ya vyet,pamoja na necta yanawezekana kuna mtu aliiba details za akampa mtu mwengine anazitumia.
 
Kama uliyoandika hapa ni kweli tupu, fanya yafuatayo:

1. Andika barua kwa mwajiri wako kuhusu kutokupata mshahara
2. Majibu watakayokupa kama mwajiri atasema ni suala la hazina, andika barua kwa Katibu Mkuu wizara ya Fedha kupitia kwa mwajiri wako.
3. Majibu ya hazina yakisema cheti ni feki, nenda necta kupata uthibitisho wa cheti kisha majibu peleka hazina.

Katika hatua zote hizo hakikisha unapata majibu kwa maandishi. Baada ya hapo ndipo waweza kwenda Utumishi kuthibitisha kwamba unavyo vyeti halali, wao watakushauri hatua ipi ya kuchukuwa.

Ni mlolongo mrefu kidogo lkn njia ya haki siku zote siyo fupi. Pole
 
diploma ya sheria chuo cha uongoz wa mahakama lushoto 2013 hope ni IJA kwa kuwa umesoma na unaijua sheria ni vizuri ungefatilia ukapata haki yako kweli inauma, yani usome miaka na kulipa ada leo hii mtu kiurahisi tu aje kupata ajira kupitia cheti chako inauma sana kwa kweli.
 
Habar Wana JF

Ndugu zangu niko hapa kuomba ushauri utaonipa mwanga wa maisha yangu. Baada ya kuhangaika hatimaye nilibahatika kuajiriwa mamlaka ya bandari.

Nilipata barua yangu ya ajira na kuanza kazi mtwara. Ikapita miezi minne bila kuanza kupata mshahara huku nilioanza nao wakianza kupata. ktk kufuatilia kwangu nikafika hazina ambako janga limenikuta.

Nikaelezwa cheti changu cha frm 4 kimetumika na mtu kaajiriwa yupo ktk system hivyo wao wametuma barua mamlaka husika kusitisha ajira yangu.

Ndugu zangu sijawahi kutoa cheti changu kumpa mtu yeyte na wala huyo simfaham.

Historia yangu nimehitim frm4 2005, Advance 2008, Bachelor UDsm 2011, diploma ya sheria chuo cha uongozi wa mahakama lushoto 2013.

Nikafanya usaili mara 6, ya saba nikapata kazi, leo ndugu zangu naambiwa hivi?

Vyet vyote ninavyo, sina ndugu kusema alitumia, wala sijakitoa kwa yeyote.

Hiv ni kweli ajira nakosa?

Ina maana elimu yangu yote ni bure?

Naomba ushauri nipate hamu ya kuishi.

Tafuta Dawa Ya Kuulia Panya Kisha Ichanganye Na Kloroquine Na Ichujie Na Mwarobaini NA HAPO UTAPATA KHERI, FURAHA na MIAKA MINGI YA KUENDELEA Kuishi Hapa Duniani. Huo MSETO Wa Hizo Dawa au Kemikali Zitakusaidia Mno Na Ukishazitumia Utanisalimia Akina Kanumba Na Mangwea Huko Utakapokutana Nao.😛oa😛oa
 
mahakama ndio jibu hapa wakikufanyia termination!kwa sasa cheza na utumishi na hazina,
urelax kazi ni yako,wanakutisha hao!
 
Tafuta Dawa Ya Kuulia Panya Kisha Ichanganye Na Kloroquine Na Ichujie Na Mwarobaini NA HAPO UTAPATA KHERI, FURAHA na MIAKA MINGI YA KUENDELEA Kuishi Hapa Duniani. Huo MSETO Wa Hizo Dawa au Kemikali Zitakusaidia Mno Na Ukishazitumia Utanisalimia Akina Kanumba Na Mangwea Huko Utakapokutana Nao.😛oa😛oa

mkuu acha kujitia utemi!!
 
pambana mwanzo mwisho! niliwai pata deiwaka - kufundisha shule - hz mnaita international, nikakuta kuna mwl ana majina km yangu, nilifuatilia kwa undani nikagundua jamaa ana copy za vyeti vyangu vya O-level na A-level, jamaa kumbe anajuana na mwenye shule, wakaniita "tuka mezani", nikajionea mauzauza, nikasepa!
 
Tafuta Dawa Ya Kuulia Panya Kisha Ichanganye Na Kloroquine Na Ichujie Na Mwarobaini NA HAPO UTAPATA KHERI, FURAHA na MIAKA MINGI YA KUENDELEA Kuishi Hapa Duniani. Huo MSETO Wa Hizo Dawa au Kemikali Zitakusaidia Mno Na Ukishazitumia Utanisalimia Akina Kanumba Na Mangwea Huko Utakapokutana Nao.😛oa😛oa

shindwa kwa jina la yesu
 
Pole sana ndugu ndio maisha misukosuko lazima....ila hilo suala unatakiwa usizembee fuatilia sehemu husika kwa uwezo wa mungu utafanikiwa
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Ahsanteni ndugu zangu nitajitahidi kuufanyia kazi ushaur wenu. linaniumiza sana hili suala lkn no way out nikuyafanyia kaz yale mazur mlonishaur, naamini kama ni rizik yangu bas mungu atanifanyia wepesi.
 
Chukua vyeti vyako vyote nenda baraza la mitihan. Wafatilie hcho chet huyo mtu mwngne kakipataje na nimwaka gan, je uliwezaja kufanya applcatn za vyuo kama chet kinashida. ? TCU hawakuliona hlo?mpaka mwsho ukapata chet cha undergraduate? Utajua kila kitu brother
 
Tafuta Dawa Ya Kuulia Panya Kisha Ichanganye Na Kloroquine Na Ichujie Na Mwarobaini NA HAPO UTAPATA KHERI, FURAHA na MIAKA MINGI YA KUENDELEA Kuishi Hapa Duniani. Huo MSETO Wa Hizo Dawa au Kemikali Zitakusaidia Mno Na Ukishazitumia Utanisalimia Akina Kanumba Na Mangwea Huko Utakapokutana Nao.😛oa😛oa

Mkuu sijapenda maneno yako, hii ishu iko serious mtu hadi kuja huku kwenye jukwaa anajua kuna intelligence people ambao watampa ushauri mzuri wsa kisomi, sa we unavyomwambia hvyo una maana gani?? Sio vizuri hvyo bhana..kama unatania bac ungeenda jukwaa la utani sio humu watu wako serious na wana matatizo kweli..kwahiyo akifa ndo utafurahi au? Au we ndio mwizi wake..mmh
 
Hiyo ni kitu ndogo sana bwana mdogo! acha kupanic fuata utaratibu husika na hakikisha una leaving certificate ya o'level then waambie wakusearchie huyo kupe anaetumia cheti chako.
Unless ukizubaa wanakuchinja kikwelikweli wanatikisa kiberiti tu hakuna termination laini kiasi hicho.
 
Back
Top Bottom