Naomba ushauri kuhusu Mercedes benz

fazsb

Member
Aug 4, 2011
50
5
Habari!

Kuna gari nimeanza kulitumia nina mwezi sasa (mercdes benz c 220, 1995 model ) shida ipo kwenye reverse transmission.

Nikiwa kwenye muinuko kidogo linagoma kurudi nyuma, ni kama linakosa nguvu lakini nikiwa kwenye level ya kawaida linarudi ila kwa shida sana

Msaada tafadhali.
 
Chekecheke ya gearbox ni chafu kwahiyo oil ya gear box inashindwa kupenya kwenye system vizuri hivyo tafuta expert wa magari hayo aifanyie service tuu tatizo litaisha kuwa makini na funding utakayempata.
 
Nashukuru kwa ushauri wako , ila hawa mafundi wakiona ni benz na bei zinabadilika.
 
JF wangetuwekea jukwaa la Magari ingekuwa vizuri zaidi, nafikiri wadau twalihitaji sana!
 
nashukuru kwa ushauri wako , ila hawa mafundi wakiona ni benz na bei zinabadilika

Service ya gearbox sio gharama, kinachohotajika ni hydraulic ya gearbox ambayo bei zake zinajulikana, ufundi hauzidi 30000 kama akiamua kuwa ghali sana
 
Siko vizuri kwenye kutoa dirction huyo nimempatia namba ya fundi aongee nae.
 
mshana jr,
Asante Mshana, naomba kuongezea!,

  1. Gereji kuu ya kwanza ya Benzi ni DT Dobbie pale Nyerere Rd,
  2. Tatizo la DT Dobbie, hawatumii spear yoyote used, lazima ununue mpya!.
  3. Ushauri wangu, kama unaipenda benzi yako, na unajiweza kiuchumi, anzia DT Dobbie, watakupitishia kitu kinaitwa diagnostic machine, inakutolea print out ya kila ubovu wa gari lako.
  4. Baada ya hapo ndipo utapewa quotation ya DT Dobbie ujipime unaweza?!.
  5. Ukishindwa ndio sasa njoo hizi gereji za vichochoroni!.
  6. Vile vikolo kolo nenda duka la benzi pale kwenye jengo la Bilicans au used duka la Big D lindi Ste

Natumia E360, ilisumbua gear box, nikaanzia DT Dobbie, nikakuta vikolokolo kibao vibovu,

DT dobbie wakasema gear box wao hawafungui wala kutengeneza, bali wanakuagizia mpya toka Ujerumani kwa TZS. 8,000,000 na kuisafirisha TZS 1,500,000 kuifunga ni TZS.500,000 total ni 10 m!. Nikaona nyingi!,

nikashauri niende Mivinjeni kununua used, kwa TZS. 3,000,000, kuifunga TZS 200,000!. Huwezi amini, ndani ya miaka 6, nimebadili gear box mara 3, imenicost zaidi ya 10 m!, na sasa iko backyard the junk yard!.

Unaweza kusave kwenye used, ila in a long run ni maumivu makubwa zaidi!.

NB. Tusije kuanza kuitana mafisadi humu, hiyo Benzi sio gari yangu, ni gari ya wife wangu!, mimi usafiri wangu ninaomiliki ni boda boda!.

Pasco
 
Last edited by a moderator:
Mmm magari sometimes ni pasua kichwa, unaweza ukajuta hivi ni kwanini ninalimiliki.
 
Hahahahaaaa Pasco nilikuwa serious sana kusoma hii reply yako ila umenivunja mbavu hapo mwishoni

Mi siogopi kuitwa fisadi alimradi tu nilichonacho hakikugharimu roho za wengine then am OK

Kuhusu Benz sasa D.T DOBIE ni washenzi sana walishawahi kutaka kuniuzia sensor ya breezer kwenye air cleaner ambayo inahusika sana na gari kukaa silencer wakanipa quotation ya USD 1300 mwaka 2008 hiyo, nikaja kuipata sensor hiyohiyo Nairobi brand new genuine kwa USD 100

Kwa shida yake aliyoelezea naona kwa uzoefu wangu ni service tu ya kawaida ila kama itahitajika spare parts diagnosis akafanye D.T DOBIE lakini spare aende Nairobi
 
Chekecheke ya gearbox ni chafu kwahiyo oil ya gear box inashindwa kupenya kwenye system vizuri hivyo tafuta expert wa magari hayo aifanyie service tuu tatizo litaisha kuwa makini na funding utakayempata.

Chekeche likiwa chafu gear zinasumbua zote......hii mbona kama ni reverse specific!!!!??????
 
Back
Top Bottom