Naomba ushauri kuhusu mahusiano yangu

sam green

Senior Member
Joined
Feb 21, 2020
Posts
191
Reaction score
297
Habari wanaJF,

Naombeni ushauri nipo na mpenzi wangu tumedumu kwenye mahusiano kwa miaka miwili na miezi kadhaa mpaka leo hii

Shida iko hapa tulikuwa tunaaminiana sana mimi na mpenzi wangu kumbe yeye sio mwaminifu kwangu nilihisi anatembea na mtu fulani nikamuulza alibisha mimi nikaendelea na uchunguzi wangu mpaka nikaamua kumpangia chumba sehemu ili taaratibu maandalizi yaendelee ili baadaye nimuoe, na hakuna kitu amewahi kosa kwangu kula, kuvaa, kila kitu kama kumpelekea moto nimepeleka saana.

Kisa kinaanzia hapa siku ya jana huyo jamaaa niliyekuwa nahisi kuwa anatembea naye alinifuata kanieleza kila kitu... akanionesha na picha walizopiga pamoja.

Akanipa ushauri kuwa huyu mwanamke ukija kuoa umepotea maana ana mambo ya ajabu sana na mimi nishamuacha baada ya kuona hasomeki.

Mimi nilipatwa na hasira sana jana usiku nikamfuata anakoishi nikamuuliza lakini alibisha tena kuwa hajawahi kuwa na mahusiano na huyo mwanaume.

Nikatoa ushahidi wa picha akanambia alimuomba tu wapige picha lakini hakuna mahusinao baina yao na picha wamekaa mikao mibaya sana.

Basi nikamshushia kipigo cha mbwa mwizi halafu nikampola laini aliyokuwa anahifadhia hela zake.

Kwa sasa kinachoendelea anaomba nimpe laini yake atoe hela halafu aondoke na mimi nataka nitoe hela yangu ambayo nilitoa kodi pale maana yeye ndio aliomba nimpangie nikalipa na kodi sasa hivi nataka nikatoe hela yangu zitakazobaki nimpe maana amesemea anataka kuondoka.

Naombeni ushauri maana hata wazazi wake wanajua kuwa nipo nae japo nilikuwa bado sijajitambulisha.
 
Mngekaa mkayamaliza mkuu maana unaonekana bado unampenda
 
Pole mkuu katika akili yangu nakushaur kaa muongee naye mwite kwa upole muulize kwa upole then usikie anasemaje kama haonyeshi kujutia kosa lake achana naye
 


JIONGEZE BRO

Mimi nilijua ulionyeshwa picha za kuthibitsha mahusiano au msg

Fanya uchunguzi wako ujiridhishe pasishaka Usijekuta mtu kakataliwa sababu yako sasa anaharibu mkose wote

Pole pia kwa hako kastress
 
Kila binadamu ana makosa, kosa la kuto kuwa mwaminifu kwenye urafiki wenu ni ishara mbaya. Shukuru Mungu wako umejua mapema yangekukuta mabaya zaidi. Chukua hizo fedha katoe sadaka
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…