Naomba ushauri kuhusu flat TV

scientificall

JF-Expert Member
Jun 4, 2015
454
314
Naomba ushauri kabla sijaingizwa mjini mimi sio mzoefu wa hizi falt TV.

Ipo hivi kuna mfanyakazi mwenzangu hapa ni mzanzibari anafanya kazi bara. Nilimwambia nahitaji kununua tv ya bei ndogo ila nimwagize tokea zanzibar kwani huko bei afadhari akanambia hata yeye alichukulia huko kwao.

Akanishauri kama tv nichukue mtumba kwani hata yeye ndo aliyonayo na ni nch 43 kampuni ya toshiba. Basi nkamwambia aniuzie ya kwake akaanzia 500k tukavutana mpaka 400k nkamlipa nusu na nkaomba nikaione kwake. Baada ya kuiona nilishangaa kidogo kuona ipo tofauti kidogo na hizi nyingine za mchina.

kwani niliona kama ina nyama kubwa ya plastic yaan kioo kinaonekana kidogo ila likaver la juu yaan plastic inaonekana imechukua nafas kubwa sana. Sikuweza kumuuliza maana alikuwa tayari kashaisifia sana kuwa haichemshi wala nn inaweza piga mzigo siku mbili mfululizo.

sasa wadau naomba mnishauri kwa hili vipi hii tv inafaa kwa matumizi ya nyumbani au imekaa kilocal sana. Na je kwa bei yake hio nimepigwa au kanifanyia fair.

kwa wajuzi naomba mnisaidie ubaya na uzuri wa hizi tv flat za mtumba hasa kampuni ya TOSHIBA.

Nawasilisha.
 
Inaitwa Bezell hio plastic ya pembeni, kama mdau hapo juu alivyokwambia inaweza kuwa ni plasma na sio led. Plasma zinakuwa mamia ya watts Sometime hadi 300W,

Cha muhimu mkuu weka model hapa, piga picha ama inakili. Kupitia model tutajua kama ni nzuri ama la.
 
Inaitwa Bezell hio plastic ya pembeni, kama mdau hapo juu alivyokwambia inaweza kuwa ni plasma na sio led. Plasma zinakuwa mamia ya watts Sometime hadi 300W,

Cha muhimu mkuu weka model hapa, piga picha ama inakili. Kupitia model tutajua kama ni nzuri ama la.
sawa lkn hapa akili ya kwenda kuchukua advance yang ishaanza kunijia
 
Back
Top Bottom