mkuu yani ndo nilikua naandika hapa nikijua HR 666 kama weweNilihisi HR 666 kumbe HR huyo
Habari wadau,
Ni wiki ya tatu tu tangu nipate kazi katika moja ya mashirika binafsi hapa nchini. Ni jambo la heri ukizingatia ndio kwanza nimemaliza chuo mwaka jana novemba.
Nilikuwa mwenye furaha sana kama mnavyo jua ( nilikuwa kama ndama aliyetoka zizini kwa mara ya kwanza). Ghafla faraja na furaha niliyokuwa nayo inapotea baada ya afisa muajiri (human resource) kuanza kunisumbua ananitaka kimapenzi (si vibaya), tatizo ni mtu mzima anayekaribia kustaafu (50+) yrs, ameolewa na mume wake ni boss mkubwa tu. Ni kama bibi yangu vile!
Hivi sasa amefikia pabaya, analeta figisu figisu hata kazi zangu haziendi. Ananiambia atahakikisha naiaga ofisi. Kazi naipenda haswa ila afya yangu naipenda zaidi . Nashindwa nifanye nini kwa sasa? Ushauri wenu ni wa msingi sana.
Hali hii inanifanya nashindwa kufikiri sawa sawa.
Mkubalie halafu panga sehemu ya kukutana.
ila kabla ya kukutana mrekodi sauti kama mara kadhaa kisha ihifadhi sehemu salama ili isije kutokea.
panga kukutana nae sehemu ambayo siyo ya wazi sana ili nafasi ya kumrekodi ipatikane.
andaa gues/hotel/au sehemu ya kukutania kufanya vile vitu,hakikisha unapatafuta mwenyewe
fanya mpango wa kutega camera ndani na nje weka mtu atakae kurekodi kwa siri sana mkiingia eneo hilo.
muache awe wa kwanza kuvua nguo baada ya hapo mwambie kila kitu kuwa umeweka watu wamewafuatilia na amerekodiwa hivyo utaenda takukuru na kuwaonyesha video zote na kama atakusumbua au kukutisha mwambie video hizo utasambaza kazini,kwa familia yake na mpaka mitandaoni ili liwalo na liwe.
Umenikumbusha mbali sanaMwambie una ukimwi
Huu Ushauri sio mzuri hata kidogo. Yaani kabla hajapiga hatua sita huyo mama atakuwa kaisha ambiwaPole sana kwa majaribu, nakushauri mpuuze, fanya kilichokupeleka.
Mambo yakizidi, basi unaweza kuwasiliana na viongozi wa chama cha wafanyakazi kinachokuwakilisha, utawaeleza changamoto hiyo na vitisho unavyovipata huku ukiwa na ushahidi hata wa meseji.
Hao viongozi watajua mbinu za kuwasiliana na uongozi wa shirika unalofanyia kazi. Lakini pia itaweka tahadhari juu ya mpango wa kukuharibia kazi kwa mambo binafsi na kukufanya kuwa salama zaidi.
Tahadhari: usithubutu kutembea na huyo mama na kama umeanza naye, acha.
Kila la heri.