koba lee
JF-Expert Member
- Sep 29, 2016
- 964
- 1,552
Natumaini mu wazima tukiwa tunaendelea na ujenzi wa taifa letu pendwa.
Nijikite moja kwa moja katika mada, mimi ni muajiriwa katika sekta binafsi katika kampuni flani maarufu sintopenda kuitaja jina. Nimefanya kazi hapo sasa ni mwaka wa tisa nautafuta wa kumi, nikiangalia maendeleo niliyonayo katika kipindi chote hayaendani kabisa maana yake nimeona nshapoteza muda na sitaki kupoteza muda tena maana na umri unasogea.
Nikipiga mahesabu ya kiasi gani ntapata kama nikifanya hapo kazi kwa miaka kumi mingine haifiki hata milioni 30, sasa huu si upimbi wakuu?
Kwahiyo wakuu ninachofikiria kukifanya ni hiki, nikishakamilisha miaka 10 kamili naandika barua ya kustaafu kwa hiari, pesa ntakayolipwa nshapiga mahesabu haitopungua milioni kumi.
Kiasi hiki naamini nikitulia kinaweza kunisogeza mbele kimaendeleo kwa kuinvest katika biashara yoyote, kuliko kupoteza muda kutumikishwa mpaka tone la mwisho likauke.
Haya ndio mawazo yangu wakuu naombeni ushauri wenu najua humu kuna watu washapitia haya na wenye uzoefu katika hili.
Asanteni na wasilisha.