Naomba ufafanuzi kuhusu 'shoti' ya umeme

NIMEONA

JF-Expert Member
Joined
Aug 4, 2019
Posts
3,854
Reaction score
5,716
Nilipigwa na shoti ya umeme ya nguvu tu siku moja katika harakati za kurekebisha hili na lile. Ajabu ni kuwa nilisikia kama mtu kanipiga rungu la kisogoni kiasi kwamba ilinilazimu kabisa kugeuka nyuma ili nione kama kuna mtu kafanya hivyo.

Nilipowahadithia wenzangu(wale waliowahi kukumbana na kisanga kama hicho) walitoa ushuhuda unaofanana na wangu.

Wenye ujuzi/utaalamu, hili limekaaje yaani kuna uhusiano gani kati ya shoti ya umeme na hisia za kupigwa na kitu kizito kisogoni?
 
Mapigo ya moyo ni 72 kwa kila dakika moja kama sijakosea sasa Umeme huu wa majumbani una Mapigo ya 50 kwa sekunde moja kitu ambacho kikikutokea lazima wenge likuingie na Mwili wa binadamu kutoka na kuwa na majimaji basi tayari ni path yani conductor japo resistance ni kubwa ivo electrons zina hangaika kupita
 
ati ya shoti ya umeme na hisia za kupigwa na kitu kizito kisogoni?

🤣 🤣 🤣 🤣 pole aisee

inaitwa 'Brain Zap'

jua kila ukigusa kitu chochote, taarifa ya mguso inasafirishwa kwa njia ya 'neva' kama 'umeme mdogo (mild electric current)' mpaka kwenye ubongo, ubongo unatoa mwitikio kupitia muscles (effector) za eneo husika

ukigusa umeme labda wa ( 30mA ), electrons zinapita moja kwa moja ndani ya 'neva' mpaka kwenye ubongo (CNS, neva za ubongo)

iyo namba ikibadilishwa kua 'pressure/impact' , kwa kua ni kubwa, hapa ndio hisia za kama kupigwa husikika kichwani, ubongo unatuma response (feedback signal) kurudi eneo ambapo mguso/stimuli umetokea, na kumwambia effector (ambae ni flexor muscles la eneo husika) ako 'contract' , na ndipo unatoa mkono wako haraka kwenye uo waya uliogusa

mida nyingine neva za maeneo ya kiwiko (elbow , ulnar nerves ) zina react na kufanya mkono wote ufe ganzi/paralyze (kama kiwango ni kikubwa mno) , au uhisi kama umepigwa ( kama kiwango cha umeme ni cha kawaida) , same scenario inatokea ukiigonga elbow yako ukutani

Hatari sana ni pale umeme ukiwa mkubwa zaidi ( hasa nyakati za mvua )

muscles karibia zote za mwili zina contract ( ie: haziwezi relax tena ) , hii inaitwa fibrillation

muscles za moyo ( cardiac muscles ) ziki fibrillate ( 'pacemaker' ya moyo inakua 'over ridden and blown off' ), moyo unastop ku pump, unakufa ( electrocution)
 
🤣 🤣 🤣 🤣 pole aisee

inaitwa 'Brain Zap'

jua kila ukigusa kitu chochote, taarifa ya mguso inasafirishwa kwa njia ya 'neva' kama 'umeme mdogo (mild electric current)' mpaka kwenye ubongo, ubongo unatoa mwitikio kupitia muscles (effector) za eneo husika

ukigusa umeme labda wa ( 30mA ), electrons zinapita moja kwa moja ndani ya 'neva' mpaka kwenye ubongo (CNS, neva za ubongo)

iyo namba ikibadilishwa kua 'pressure/impact' , kwa kua ni kubwa, hapa ndio hisia za kama kupigwa husikika kichwani, ubongo unatuma response (feedback signal) kurudi eneo ambapo mguso/stimuli umetokea, na kumwambia effector (ambae ni flexor muscles la eneo husika) ako 'contract' , na ndipo unatoa mkono wako haraka kwenye uo waya uliogusa

mida nyingine neva za maeneo ya kiwiko (elbow , ulnar nerves ) zina react na kufanya mkono wote ufe ganzi/paralyze (kama kiwango ni kikubwa mno) , au uhisi kama umepigwa ( kama kiwango cha umeme ni cha kawaida) , same scenario inatokea ukiigonga elbow yako ukutani

Hatari sana ni pale umeme ukiwa mkubwa zaidi ( hasa nyakati za mvua )

muscles karibia zote za mwili zina contract ( ie: haziwezi relax tena ) , hii inaitwa fibrillation

muscles za moyo ( cardiac muscles ) ziki fibrillate, moyo unastop ku pump, unakufa ( electrocution)
ahsante sana kwa somo maridhawa, nimepata mwanga sasa!
 
Zingatia hili, shoti ya umeme huwa haipigi kwa maana huwa tayari hakuna mtiririko wa umeme kwenye shoti (Short) na kinachotokea hapo ni joto au moto. Isipokuwa kinachokupiga hapo ni shoku (Shock) kwa kuwa hapo umeme unatiririka kuingia mwilini na ndipo kipigo cha mbwa mchungulia watu hutokea.

Mimi niliwahi kujiuliza swali miaka ya 2001-2002 kwamba kwa nini ukishika waya mmoja wa umeme unadundwa lakini kwenye iverter hauhisi chochote? Nilichofanya hapo wakati natafiti nilichukua antena ya redio ndogo na mdenge wa baiskeli maana ndivyo vilivyokuwepo, nikashika mkono huu mdenge na mkoni huu antena, nikawasha inverter na nikachomeka extension kisha mdenge nikauchomeka kwenye tundu la kwanza na antena kwenye tundu la pili la extension, aisee sitasahau sumbwi la mgongoni nililotwishwa yaani sikujua Mike Tyson kaingia saa ngapi na kutoweka saa ngapi, nikagundua hata inverter yaweza kuuwa mtu.

Yaani nina baadhi visa ambavyo umeme umenifanyia ila sitaki kuwachosha aisee.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
hahahahahah!
shukrani, hatari sana haya mambo ya umeme....yaani ninauheshimu kweli na siruhusu hata kidogo watoto waucheee!!
 
Niliwahi kulowanisha sabuni kwa vimaji kidogo nikachukua waya wa umeme wa redio, nikauchomeka kwenye umeme huku nikiwa nimeingiza viwaya kwenye matundu ya waya yanayoingiza umeme kwenye redio, sasa hivyo viwaya nikavigusisha kwenye sabuni yenye unyevu, ile sabuni ilitoa mlio na moshi na moto ka bomu la mkorea aisee. Nikagundua kumbe sabuni ina ma-acid ya kutosha.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom