Naomba ushauri kutokana na changamoto ya umeme kwisha haraka na kupiga shoti mwilini

Udochi

JF-Expert Member
Jul 25, 2015
761
1,006
Waheshimiwa,

Ninapoishi kuna changamoto mbili za umeme;
1) Umeme unaisha haraka sana tofauti na kawaida.
Kwenye nyumba niliyokuwa naishi awali nilikuwa natumia umeme wa 15,000/- tu kwa mwezi,
Wakati ninapoishi sasa, umeme huo nautumia kwa siku 10 tu hali ya kuwa vifaa vyangu ni vilevile na matumizi ni yaleyale

Na sishei umeme na mtu mwingine.

2) Changamoto ya pili, umeme unaonekana kuwa mkali sana kiasi cha kupiga shoti mwilini

  • Unapoigusa charger ya simu ikiwa kwenye socket hata kama socket imezimwa.
  • Unapocharge PC ukiigusa baadhi ya sehemu.
  • Ukiunganisha pasi kwenye socket, ukiigusa tu shoti yake mwilini ni hatari.
  • Na kifaa chochote kipitishacho umeme kikiunganishwa na socket tu, ukikigusa mwili hupigwa shoti.

Ningeomba kujuzwa ufumbuzi wa changamoto hizi wakuu.
 
Mimi siyo mtaalamu wa Umeme ila tatizo la kupigwa shoti Hovyo linatokana na Earth wire..

Tafuteni fundi akague Connection ya Earth wire..kuna shida mahali...

Kama nimekosea Mafundi watanisahihisha
 
Umemjibu sahihi kabisa.
Na jibu la changamoto ya pili ni inawezekana sababu ikawa nyumba ya kwanza umeme ulikua umeunganishwa kwa lile punguzo maalum ambalo kwa mwezi hua haizidi kiwango flani (REA). Nyumba aliyo hamia mara ya pili iliunganishwa umeme kwa meter za kawaida ambazo hazina punguzo ndio maana umeme unatumika mwingi kwa muda mfupi.
 
Mimi ndo maana ninakaa chumba hakina umeme. Munakua kimya km muko jela.
 
Waheshimiwa,
Ninapoishi kuna changamoto mbili za umeme;
1) Umeme unaisha haraka sana tofauti na kawaida.
Kwenye nyumba niliyokuwa naishi awali nilikuwa natumia umeme wa 15,000/- tu kwa mwezi,
Wakati ninapoishi sasa, umeme huo nautumia kwa siku 10 tu hali ya kuwa vifaa vyangu ni vilevile na matumizi ni yaleyale-
Na sishei umeme na mtu mwingine.

2) Changamoto ya pili, umeme unaonekana kuwa mkali sana kiasi cha kupiga shoti mwilini

  • Unapoigusa charger ya simu ikiwa kwenye socket hata kama socket imezimwa.
  • Unapocharge PC ukiigusa baadhi ya sehemu.
  • Ukiunganisha pasi kwenye socket, ukiigusa tu shoti yake mwilini ni hatari.
  • Na kifaa chochote kipitishacho umeme kikiunganishwa na socket tu, ukikigusa mwili hupigwa shoti.

Ningeomba kujuzwa ufumbuzi wa changamoto hizi wakuu.
.
Ripoti Tanesco haraka..
Unacheza na hatari..
Au tafuta fundi mzuri apime voltage ikoje ..na apime Earth kama ina umeme...fanya haraka Sana .....

Kama earth ina umeme ni lazima umeme uende haraka Sana ina maana kuna leakage ...utafute fundi mzuri akague leakage iko wapi...hadi earth iwe ina umeme...pia kagua earth wire na earth rod...kama viko sawa..mtafute fundi mzuri atazame hivyo kama tatizo ni la Tanesco uripoti Kwa haraka
 
Mimi ndo maana ninakaa chumba hakina umeme. Munakua kimya km muko jela.
Vijana wa daslam watakuita mshamba...🤣 lakini mimi nimegundua wewe ndio mjanja...😜
Hongera sana kwa kujiongeza ili uwakomoe wenye umeme wao...😝
 
Back
Top Bottom