Naomba ufafanuzi kuhusu mshahara katika Kiwanda cha chokaa cha Nelkanth Tanga

bokilo

JF-Expert Member
Nov 30, 2015
498
968
Wakuu kwema?

Naomba kujua mishahara wanalipaje kwenye hiki kiwanda cha kneelkanth cha chokaa maana kuna jamaa wa Facebook ananiitia kazi kule sasa kila nikimwomba taarifa zaidi hanipi.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwani kwa sasa una ajira? kama huna ni vizuri tu ukajitosa mazima kuliko kukaa kupiga mark time,kama unayo pia ni vyema kwenda kusikiliza maslahi yao with confidence kuwa unaweza kuwapa salary expectation yako pamoja na benefits zingine.

wakifika bei you are in. kuna utofauti mkubwa wa utafutaji kazi kati ya asiye na ajira kabisa na mwenye ajira anayetafuta maslahi zaidi
 
kwani kwa sasa una ajira?kama huna ni vizuri tu ukajitosa mazima kuliko kukaa kupiga mark time,kama unayo pia ni vyema kwenda kusikiliza maslahi yao with confidence kuwa unaweza kuwapa salary expectation yako pamoja na benefits zingine,wakifika bei you are in.kuna utofauti mkubwa wa utafutaji kazi kati ya asiye na ajira kabisa na mwenye ajira anayetafuta maslahi zaidi
Nimejiajiri mkuu sema nilitaka nimwachie mtu kibanda changu nikapambane zaidi

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wakuu kwema?

Naomba kujua mishahara wanalipaje kwenye hiki kiwanda cha kneelkanth cha chokaa maana kuna jamaa wa Facebook ananiitia kazi kule sasa kila nikimwomba taarifa zaidi hanipi.

Sent using Jamii Forums mobile app
Kama wewe upo legelege usiende huko maana hutaweza ! Pale watu wanalipwa kwa wiki kila Jmosi watu wanachukua mpunga na malipo inategemea na kitengo chako ila range ni kuanzia 45,000 -100,000/ kazi nyingi pale inategemea sana juhudi yako.
n.b Pale ndio nilipojifunzia kuvaa Barakoa maana vumbi lake sio la nnchi hii.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
tafadhali naomba unijibu yafuatayo;
i/ Huyo aliekupa taarifa za uwepo wa hiyo Kazi kwenye hicho Kiwanda ni nani yako?
ii/ Nafasi iliyopo ni kwa ajili ya Kazi gani?
iii/ Ushawahi kutuma Maombi ya Kazi kwenye hicho Kiwanda?
Mtu aliyeniita ni kwenye group Facebook sasa nikimtumia mesej hajibu tena
 
Back
Top Bottom