Naomba ufafanuzi kuhusu michango yangu ya PPF

NALO LITAPITA

JF-Expert Member
Aug 25, 2011
328
225
Wanabodi habari ya majukumu?

Nakuja kwenu kuomba ufafanuzi kwa mwenye kuelewa utaratibu wa Jambo hili.

Mimi ni mwàjira katika sekta binafsi. Kabla ya serikali kuunganisha mifuko ya hifadhi ya jamii nilikuwa mwanachama wa PPF. Baada ya kuunganishwa kwa mifuko tukaelezwa sisi wafanyakazi wa sekta binafsi tunapaswa kujiunga na mfuko wa NSSF. Wakati naenda kufanya usajili wa kujiunga na NSSF niliuliza kuhusu utaratibu wa michango yangu ya PPF nikaelezwa kwamba itahamishiwa NSSF punde.

Leo nimeenda kuomba statement ya michango yangu imeonekana tu ile mliyoanza kuchangia baada ya kujiunga rasmi NSSF mwaka 2019.

Nimemuuliza Dada aliyenitolea statement akasema michango niliyochangia PPF iko PSSSF. Hivyo hiyo napaswa kwenda kuiulizia huko.

Naomba mwenye kujua utaratibu wa Hatima ya michango yangu hiyo anisaidie kunifafanulia.Nini kifanyike ili michango hii iwekwe katika mfuko mmoja.
 
NALO LITAPITA

JF-Expert Member
Aug 25, 2011
328
225
Ungefanya Kwanza alivyokuelekeza huyo dada, ukikwama na huko ndio ungeanzisha Uzi.
Shukrani Mkuu, Nitafanya hivyo alafu nitaleta mrejesho. Niliona niwashirikishe wanajukwaa kwa sababu taarifa ya leo imekinzana na taarifa niliyopewa awali kipindi cha kujiunga.
 
UPOPO

JF-Expert Member
Dec 17, 2010
3,045
2,000
Mimi nimefanya hivyo na nikapwa statement yangu basi.Nilipouliza kuhusu kuunganishwa wakawa hawana jibu.So kama kuna mtu mwenye jibu atuambie jamani. Wakasema tuende NSSF.

Inaelekea kuna vitu bado havijakaa sawa. Nilipowauliza kuhusu kuchukua wakasema kila mfuko utajaza form yake. Nina mfano wa raia wa nje hapa ofisini aliyekuwa anachangia na fedha zake zikaamishwa .Amejaza form mbili, moja NSSF na nyingine PPF(PSSSF) .
 
Mkaruka

JF-Expert Member
Feb 5, 2013
18,270
2,000
Michango yako iliyoko PSSSF itabaki huko huko na wakati wa kuichukua utafuata taratibu za huko huko PSSSF kuipata.

Hivyo hivyo huku NSSF pia utafuata taratibu zao kupata haki zako. Hakuna muingiliano wowote wala kuunganishana.
 
honeybae

JF-Expert Member
Sep 3, 2016
323
500
Kila michango kwenye mifuko tofauti inajitegemea mkuu, hivyo siku ya kuchukua utaanza mmoja na utaenda kwa mwingine nadhani wameshindwa kuinganisha wameona ibaki kuwa hivyo.
 
UPOPO

JF-Expert Member
Dec 17, 2010
3,045
2,000
Michango yako iliyoko PSSSF itabaki huko huko na wakati wa kuichukua utafuata taratibu za huko huko PSSSF kuipata.

Hivyo hivyo huku NSSF pia utafuata taratibu zao kupata haki zako. Hakuna muingiliano wowote wala kuunganishana.
Je, wakati wa unastaafu .Pension wanakulipaje sasa.Utakuwa unachukua kote kuwili. PPF umechangia 10years na labda NSSF 7 years inakuwaje
 
stephot

JF-Expert Member
Mar 1, 2012
12,323
2,000
Michango yako iliyoko PSSSF itabaki huko huko na wakati wa kuichukua utafuata taratibu za huko huko PSSSF kuipata.

Hivyo huku NSSF utafuata taratibu zao kuipata. Hakuna muingiliano wowote.
Aende PSSSF kuna forms za kujaza akisha jaza atatakiwa kurudisha kwa muajiri wake,then muajiri akishapitia na kujaza sehemu yake muajiri ataipeleka tena PSSSF ili utaratibu wa kukuunganisha kutoka NSSF ufanyike na michango yako kuingizwa.
 
Mkaruka

JF-Expert Member
Feb 5, 2013
18,270
2,000
Je wakati wa unastaafu .Pension wanakulipaje sasa.Utakuwa unachukua kote kuwili.PPF umechangia 10years na labda NSSF 7 years inakuwaje
Yes, utafuatilia pesa zako zilizoko PSSSF then ukimaliza utafuatilia pesa zako zilizoko NSSF.

Kila taasisi inafanya kazi kivyake na kwa taratibu zake.
 
UPOPO

JF-Expert Member
Dec 17, 2010
3,045
2,000
Yes, utafuatilia pesa zako zilizoko PSSSF then ukimaliza utafuatilia pesa zako zilizoko NSSF.

Kila taasisi inafanya kazi kivyake na kwa taratibu zake.
Hiyo ni kama unazichukua kwa mkupuo.Kama ume qualify kwa pension ya kila mwezi inakuwaaje (yaani umestaafu sasa)
 
APEFACE

JF-Expert Member
Oct 1, 2016
3,929
2,000
Wanabodi habari ya majukumu?

Nakuja kwenu kuomba ufafanuzi kwa mwenye kuelewa utaratibu wa Jambo hili...
Kuunga michango haiwezekani, ila kama unataka kulipwa mafao yako ndo wanaijumuisha, kikubwa kitambulisho chako cha PPF uwe nacho, kwa mfano mimi nilikuwa LAPF baadae mifuko ilivounganishwa nikawa PSSSF lakini walikuja kutuambia tuanze kuchangia NSSF....sasa siku nadai madai yangu, nilienda nikachukua statement PSSSF nikaipeleka NSSF, lakini nilipoomba statement ya NSSF ile michango ilikuwa PSSF haikuonekana, but wakati wananilipa hela iliingia yote....ila huo mzunguko wake hadi nalipwa usiombe....
 
Mkaruka

JF-Expert Member
Feb 5, 2013
18,270
2,000
Hiyo ni kama unazichukua kwa mkupuo.Kama ume qualify kwa pension ya kila mwezi inakuwaaje (yaani umestaafu sasa)
Watafuata utaratibu wa kawaida wa pension ulivyo kwa mujibu wa kikokotoo chao.

Yaani kwa lugha ni kama kila mfuko haujui kama una pesa sehemu nyingine. Wao wanachojua wewe ulikuwa mchangiaji kwenye mfuko wao, na unataka chako.
 
UPOPO

JF-Expert Member
Dec 17, 2010
3,045
2,000
Watafuata utaratibu wa kawaida wa pension ulivyo kwa mujibu wa kikokotoo chao.

Yaani kwa lugha ni kama kila mfuko haujui kama una pesa sehemu nyingine. Wao wanachojua wewe ulikuwa mchangiaji kwenye mfuko wao, na unataka chako.
Kwa sheria ya pension hiyo haiwezekani .Kwani sheria ya pension inasema lazima uchangie miaka si chini ya 15 (au miezi 180) ndio unaqualify ile monthly pension na lampsum kutokana na kikokotoa.

Sasa mimi swali umeshachangia 17 years (10yrs NSSF ,7yrsa PPF) wanakulipaje ?kwa sababu ume qualify kupata pension na vigezo vingine kuzingatiwa(55years na kuendelea kumefikisha) Mimi hilo ndio swali langu
 
Mkaruka

JF-Expert Member
Feb 5, 2013
18,270
2,000
Kwa sheria ya pension hiyo haiwezekani .Kwani sheria ya pension inasema lazima uchangie miaka si chini ya 15 (au miezi 180) ndio unaqualify ile monthly pension na lampsum kutokana na kikokotoa .Sasa mimi swali umeshachangia 17 years (10yrs NSSF ,7yrsa PPF) wanakulipaje ?kwa sababu ume qualify kupata pension na vigezo vingine kuzingatiwa(55years na kuendelea kumefikisha) Mimi hilo ndio swali langu
Na kama ni hivyo, ni kwanini fao la kujitoa liliondolewa mpaka mchangiaji afikishe miaka 55.

Je, kama ulifanya kazi miaka 5 na hukuchukua michango yako mpaka ukawa na 55 of age utalipwa vipi??
 
UPOPO

JF-Expert Member
Dec 17, 2010
3,045
2,000
Kuunga michango haiwezekani, ila kama unataka kulipwa mafao yako ndo wanaijumuisha, kikubwa kitambulisho chako cha PPF uwe nacho, kwa mfano mimi nilikuwa LAPF baadae mifuko ilivounganishwa nikawa PSSSF lakini walikuja kutuambia tuanze kuchangia NSSF....sasa siku nadai madai yangu, nilienda nikachukua statement PSSSF nikaipeleka NSSF, lakini nilipoomba statement ya NSSF ile michango ilikuwa PSSF haikuonekana, but wakati wananilipa hela iliingia yote....ila huo mzunguko wake hadi nalipwa usiombe....
Wewe umelipwa one lumpsum au Lumpsum na kila mwezi unapokea kama mstaafu.Hilo ndio swali langu.Kama ni mkupuo moja hiyo inawezekana .
 
NALO LITAPITA

JF-Expert Member
Aug 25, 2011
328
225
Aende PSSSF kuna forms za kujaza akisha jaza atatakiwa kurudisha kwa muajiri wake,then muajiri akishapitia na kujaza sehemu yake muajiri ataipeleka tena PSSSF ili utaratibu wa kukuunganisha kutoka NSSF ufanyike na michango yako kuingizwa...
Mkuu nakushukuru sana,Nitaenda huko.Hakika JF idumu.
 
NALO LITAPITA

JF-Expert Member
Aug 25, 2011
328
225
Kuunga michango haiwezekani, ila kama unataka kulipwa mafao yako ndo wanaijumuisha, kikubwa kitambulisho chako cha PPF uwe nacho, kwa mfano mimi nilikuwa LAPF baadae mifuko ilivounganishwa nikawa PSSSF lakini walikuja kutuambia tuanze kuchangia NSSF....sasa siku nadai madai yangu, nilienda nikachukua statement PSSSF nikaipeleka NSSF, lakini nilipoomba statement ya NSSF ile michango ilikuwa PSSF haikuonekana, but wakati wananilipa hela iliingia yote....ila huo mzunguko wake hadi nalipwa usiombe....
Mkuu ulilipwa fao gani? ni lile la kujitoa?.
 
YEHODAYA

JF-Expert Member
Aug 9, 2015
29,555
2,000
Aende PSSSF kuna forms za kujaza akisha jaza atatakiwa kurudisha kwa muajiri wake,then muajiri akishapitia na kujaza sehemu yake muajiri ataipeleka tena PSSSF ili utaratibu wa kukuunganisha kutoka NSSF ufanyike na michango yako kuingizwa...
usumbufu wafanye wenyewe ,mwajiriwa siye aliyeunga hiyo mifuko
 
UPOPO

JF-Expert Member
Dec 17, 2010
3,045
2,000
Na kama ni hivyo, ni kwanini fao la kujitoa liliondolewa mpaka mchangiaji afikishe miaka 55.

Je, kama ulifanya kazi miaka 5 na hukuchukua michango yako mpaka ukawa na 55 of age utalipwa vipi??
Unalipwa nahisi mkupuo huwi kwenye pensionable scheme.Ila kuna kipengele waliweka kuwa ukiacha kuchangia kwa kuacha kazi ulipwi chochote ila ukiachishwa unalipwa % ya mshaharabwako kwa miezi 6 wanaita fao la kukosa ajira .So sina hakika wakishakulipa hiyo kuna cjichote utapata tena hata ufike 55
 
IROKOS

JF-Expert Member
Aug 13, 2011
10,195
2,000
Michango yako iliyoko PSSSF itabaki huko huko na wakati wa kuichukua utafuata taratibu za huko huko PSSSF kuipata.

Hivyo hivyo huku NSSF pia utafuata taratibu zao kupata haki zako. Hakuna muingiliano wowote wala kuunganishana.
Kwa mujibu wa sheria mpya iliyounda hii mifuko 2, NSSF kwa private sector na PSSSF kwa walioko serikalini ni kwamba kuna utaratibu wa kuunganisha michango ili mchangiaji wakati wa kuchukua mafao achukue kwa pamoja na aweze kunufaika zaidi.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom