Naomba ufafanuzi kuhusu michango yangu ya PPF

Je, wakati wa unastaafu .Pension wanakulipaje sasa.Utakuwa unachukua kote kuwili. PPF umechangia 10years na labda NSSF 7 years inakuwaje
Itachanganywa ili mtu apate mafao mazuri, nimeulizia nikaambiwa hivyo. Wakati wa kustaafu wataangalia kule ambako umemalizia ndiyo wstahamushia huko.
 
Kwa sheria ya pension hiyo haiwezekani .Kwani sheria ya pension inasema lazima uchangie miaka si chini ya 15 (au miezi 180) ndio unaqualify ile monthly pension na lampsum kutokana na kikokotoa.

Sasa mimi swali umeshachangia 17 years (10yrs NSSF ,7yrsa PPF) wanakulipaje ?kwa sababu ume qualify kupata pension na vigezo vingine kuzingatiwa(55years na kuendelea kumefikisha) Mimi hilo ndio swali langu
Ndiyo maana nakuambia wataiunganisha michango yako from both ili uwe umequlify kulipwa pensheni
 
Kwa mujibu wa sheria mpya iliyounda hii mifuko 2, NSSF kwa private sector na PSSSF kwa walioko serikalini ni kwamba kuna utaratibu wa kuunganisha michango ili mchangiaji wakati wa kuchukua mafao achukue kwa pamoja na aweze kunufaika zaidi.
Mpaka sasa hakuna michango iliyounganishwa.
 
Michango yako iliyoko PSSSF itabaki huko huko na wakati wa kuichukua utafuata taratibu za huko huko PSSSF kuipata.

Hivyo hivyo huku NSSF pia utafuata taratibu zao kupata haki zako. Hakuna muingiliano wowote wala kuunganishana.
Hili Ni tatizo Sasa.

Sababu michango yako ikifikia miezi 180 (miaka 15) unakua qualified kupata monthly pensions apart from Gratuity.

Sasa Kama NSSF iko miezi 100 na PSSSF iko miezi 80 si utajikuta inanyimwa kote kote?
 
Wanabodi habari ya majukumu?

Nakuja kwenu kuomba ufafanuzi kwa mwenye kuelewa utaratibu wa Jambo hili.

Mimi ni mwàjira katika sekta binafsi. Kabla ya serikali kuunganisha mifuko ya hifadhi ya jamii nilikuwa mwanachama wa PPF. Baada ya kuunganishwa kwa mifuko tukaelezwa sisi wafanyakazi wa sekta binafsi tunapaswa kujiunga na mfuko wa NSSF. Wakati naenda kufanya usajili wa kujiunga na NSSF niliuliza kuhusu utaratibu wa michango yangu ya PPF nikaelezwa kwamba itahamishiwa NSSF punde.

Leo nimeenda kuomba statement ya michango yangu imeonekana tu ile mliyoanza kuchangia baada ya kujiunga rasmi NSSF mwaka 2019.

Nimemuuliza Dada aliyenitolea statement akasema michango niliyochangia PPF iko PSSSF. Hivyo hiyo napaswa kwenda kuiulizia huko.

Naomba mwenye kujua utaratibu wa Hatima ya michango yangu hiyo anisaidie kunifafanulia.Nini kifanyike ili michango hii iwekwe katika mfuko mmoja.
Mkuu @NALO LITAPITA
kwema, Nilikuwa na swali kama hili. Je kwako ulifikia wapi baada ya kufuatilia ukiunganisha na maelezo ya wadau?
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom