Naomba TMA watuambie kama Dodoma kuna hatari ya kukumbwa na tetemeko kabla serikali haijahamia huko

Information is power. Wataalamu wa hali ya hewa, TMA watuambie mapema kama mji wa Dodoma ni ukanda unaofahamika kuwa na tabia nchi yenye matetemeko ya ardhi ya mara kwa mara ili wananchi washauriwe mapema aina ya majengo yanayopaswa kujengwa Dodoma.

Hii ni muhimu sana ili kuepuka kuja kunyoosheana vidole vya lawama kati ya wanasiasa, wachumi na wataalamu wa hali ya hewa kama maafa na hasara nyingine zitakujakutokea kwa kusababishwa na matetemeko ya ardhi.

Ni nyumba zenye urefu gani zijengwe Dodoma? Sehemu gani zijengwe nini au zisijengwe nini? Je, TMA mnasemaje nanyi kuhusu serikali kwenda Dodoma?
Mamlaka ya hali ya hewa haihusiki na mambo ya matetemeko.ni sawa na kumuuliza messi akuandikie dawa ya gono.
 
Je tetemeko lina uhusiano na hali ya hewa? Au TMA wana uhusiano na matetemeko ya ardhi?
TEtemoko ni moja kati mabadiliko ya tabia nchi, matetemeko ya ardhi yanaweza kuadhiri hali ya hewa ya sehemu fulani. Nani ana wajibu wa kutabiri uwezekano wa kutokea tetemeko la ardhi? Doctor wa macho na dokta wangozi ni tofauti lakini wote ni madaktari
 
Hili litiliwe maanani badala ya kukurupuka tu na kuhamia Dodoma. Kanda ya ziwa ilikuwa ikipata matetemeko madogo ambayo hayakuwa na madhara makubwa hali kadhalika Dodoma. Hili tetemeko la ardhi la juzi lililo na ukubwa wa 5.9 ni la kwanza ambalo limeacha maafa makubwa. Hivyo siku za usoni si ajabu Dodoma nayo ikakumbwa na tetemeko kubwa kama hili na kuleta maafa kama ya Kagera au hata zaidi hili lililotokea July 13, 2016 lilikuwa na ukubwa wa 5.1. Serikali isikurupuke tu na kuhamia Dodoma kwa sababu tu mungu wa Ikulu anataka iwe hivyo.

*~*~*~*~*~*~*~*~*~*~*~*~*~*~*~*~*~*~*~*~*~*~*~*
Asubuhi ya July 13 2016 nilianza kuona naandikiwa msg na wengine kuniandikia kwenye mitandao ya kijamii kwamba kumetokea tetemeko la ardhi kwenye mkoa wa Dodoma na mpaka wengine wakaelezea walivyopata na hofu.

Sasa ili kujua kama kuna madhara yoyote yaliyotokea kwenye maeneo mbalimbali ya Dodoma lilikopita tetemeko hilo, millardayo.com imempata Kamishna msaidizi wa Polisi Lazaro Benedict.

Amesema ‘ni Kweli tetemeko limetokea asubuhi hii lakini hakuna madhara yoyote yaliyoripotiwa sehemu yoyote, ilikuwa ni majira kati ya saa kumi na mbili asubuhi kuelekea saa moja kamili asubuhi’

Dodoma pia ni prone area to earthquakes coz lipo kwenye ukanda wa bonde la ufa
 
Acheni ujinga kweni walioko dodoma sasa hivi wana miili ya chuma hawaogopi matetemeko.? Dodoma tutaenda kama ni matetemeko tutapambana nayo huko mbele kwa mbele
 
Kwani kwa mfano; makao makuu ya kahamia huku sumbawanga au njombe au mbeya kutakuwa na shida... kuna mchawi mmoja alisema baada ya miaka milioni 2 dodoma itazama chini ya ardhi na kutokea ziwa kubwa kama sio bahari...

Ngoja niishie hapo nisije chochea
 
Hivi mamlaka ya Geology na Meteorology zna zina uhusiano?
hili suala nimesikia tena watu wamejikanganya hi ni issue ya Geology and Survey in Tanzania
 
DOM kwa matetemeko ndio kwao, hata majengo marefu hayashauriwi kujengwa Dom.
 
Ofisi kuu (Headquarter) za GST zipo Dodoma. Let's hope wanashirikishwa ipasavyo katika suala hili la kuhamia Dom
 
Nionavyo mimi kabla ya kuhamia Dodoma wangeitwa kwanza wataalamu kutoka nje wafanye utafiti kwanza ufanyike utafiti wasije ujaza magorofa mwisho ikatokea handaki la karne itakapo tokea tetemeko na uelemewa wa ardhi. Sijasomea mambo hayo ni maono tu wajameni.

Wazungu walishapima na kuona karne nyingi huko nyuma. Kujua Dodoma ni eneo linaloweza kuathirika kwa tetemeko la ardhi ni jambo moja lakini kujua namna ya kuishi katika eneo la namna hii ni jambo lingine.
 
Ofisi kuu (Headquarter) za GST zipo Dodoma. Let's hope wanashirikishwa ipasavyo katika suala hili la kuhamia Dom
Ofisi kuu (Headquarter) za GST zipo Dodoma. Let's hope wanashirikishwa ipasavyo katika suala hili la kuhamia Dom
Ofisi kuu (Headquarter) za GST zipo Dodoma. Let's hope wanashirikishwa ipasavyo katika suala hili la kuhamia Dom
Ofisi kuu (Headquarter) za GST zipo Dodoma. Let's hope wanashirikishwa ipasavyo katika suala hili la kuhamia Dom
Ofisi kuu (Headquarter) za GST zipo Dodoma. Let's hope wanashirikishwa ipasavyo katika suala hili la kuhamia Dom
Ofisi kuu (Headquarter) za GST zipo Dodoma. Let's hope wanashirikishwa ipasavyo katika suala hili la kuhamia Dom
Africa hakuna uhusiano kati ya siasa na sayansi na tafiti. Africa inategemea kuendelea kwa kutumia siasa badala ya sayansi na tafiti. Kabla ya kufanya jambo kubwa kama hili la kuanzisha mji mkuu mpya ni vema wanasiasa wangekaa na wanasayansi, watafiti, wachumi, wanasheria na wadau wote muhimu kufanya upembuzi wa kina kwenye hili jambo ambalo bila shaka litahitaji kuwekeza pesa nyingi za wananchi na kuwakusanya watu wengi sana na mali zao nyingi na vitu vyao vingi sana kwenye eneo moja. Bila shaka eneo hilo nyeti namna hii ni lazima lithibitishwe kuwa liko salama na linafaa kwa vigezo vingi badala ya kigezo kimoja tu cha eneo hili kuwa katikati ya nchi. bila kujali ni TMA au ni GST hiyo sio hoja kuu ya uzi huu, hoja ni je wanasayansi, watafiti, wachumi wameshilikishwa vipi katika kulichagua eneo la kujenga makao makuu mapya ya serikali? Haitoshi kusema tu kuwa ni katikati ya nchi. Watu wengi sana na vitu/magengo mengi vikisongamana pamoja ni hatari sana nyakati za disasters kama vile tetemeko, floods, terrorism, fire, etc. Kila jambo linapangwa na Mungu lakini Sayansi nayo inatoka kwa Mungu pia wakawezezwa wanadamu ili kuwahudumia wanadamu wenzao.

Tunafahamu ni kawaida kwa wanasiasa tangu zama za kale kukataa ushauri wa kisayanzi, wanasayansi wengi wa kale duniani kote walipoteza maisha yao mikononi mwa wanasiasa walipokuwa wanapinga kukosolewa na wanataaluma.
 
Nenda kajifunze kwa nn dodoma hakujengwi majengo marefu na hata yakijengwa hayazid ghorofa 6 au yakizidi kuna style /shape ya kujenga .. Au jiulize kwa nn majengo yote ya udom yamejengwa nyuma/pemben ya milima
 
Uko kuna tetemeko la ukawa tu
Wewe nawee, kwako kila kitu unawaza vyama vingi tu. kana kama hujiamini vile!! uchaguzi umeshapita na washindi wameshafahamika na wako kazini. Hapa tunajadili kuhusu taifa letu. Tetemeko linapotokea haliangalii Ukawa wala rangi ya sare ya chama. Usiogope kutoa maoni yako huru kwa kuhofia ukawa na uccm sisi ni watanzania mazuri na mabaya kitokea ni yetu wote
 
Back
Top Bottom