Serikali: Hameni mabondeni kabla ya El Nino, hakuna fidia kwa waathirika

ChoiceVariable

JF-Expert Member
May 23, 2017
43,114
49,840
Tahadhari hiyo imetolewa wakati Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) ikitabiri kuwapo kwa mvua kubwa za El Nino zinazotarajiwa kuanza hivi karibuni.

Mkurugenzi Msaidizi Ofisi ya Waziri Mkuu, anayesimamia Kituo cha Operesheni na Mawasiliano ya Dharura, Prudence Constantine, akizungumza katika maadhimisho ya kimataifa ya kupunguza madhara ya maafa, alisema serikali haina fungu la kulipa fidia wananchi.

Alisema hakuna mtu mwenye uhalali wa kukaa maeneo hatarishi, hivyo hata kama wamekaa muda mrefu, wanatakiwa kuondoka kabla ya mvua hizo kuanza.

“Wanaoishi mabondeni au maeneo yote hatarishi, serikali haina fidia ya kuwapa. Tuendelee kuwaelimisha ili waondoke,” aliomba.

Constantine aliwataka wakazi hao wasing'ang'anie kusema wana vibali vya kuishi maeneo hayo na wasisubiri kupewa fidia, hivyo ni vizuri waondoke.

Alisema katika idara hiyo ya maafa, hamna fidia ya maisha ya binadamu na yakitokea maafa, kamati elekezi za mikoa, zitaainisha maeneo yaliyoathirika na siyo fidia, bali ni kifuta jasho.

“Ni vizuri wahame mapema kwa kuwa hakuna cha kupewa kiwanja ndiyo wahame, hii tunawapa elimu ya bure na mtu asichukulie poa,” alisisitiza.

Alisema katika kukabiliana na maafa ya mvua hizo, timu ya wataalamu kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu, iko katika mikoa 14, ambayo imetambuliwa na TMA kutoe elimu ya kujikinga na majanga hayo.

Aliitaja mikoa hiyo kuwa ni, Kagera, Geita, Mwanza, Shinyanga, Simiyu, Kigoma, Dar es Salaam, Tanga, Pwani, Morogoro, Unguja Kusaini, Manyara, Pemba na Unguja Kaskazini.

Katika maadhimisho hayo, Mkuu wa Kitengo cha Majanga Asili ya Jiolojia kutoka Taasisi ya Jiolojia ya Utafiti wa Madini Tanzania, Gabriel Mbogoni, alisema athari zinaweza kusababishwa na majanga ya asili ni sunami, vimbunga na tetemeko la ardhi.

Alisema lengo la kuadhimisha siku ya kimataifa ya kupunguza madhara ya maafa kufanyika Oktoba 13 ili kutoa kupunguza majanga ya asili.

Mbogoni alisema wananchi wanaoishi karibu na miinuko waepuke kujenga kwenye miinuko na waendelee kuchukua tahadhali.

Mvua hizo ambazo zimekuwa zikinyesha kila baada ya miaka miwili, kwa mara ya mwisho nchini zilinyesha mwaka 2016 na kusababisha madhara yakiwamo mafuriko.

Nipashe
 
Write your reply...nimepanda mahindi kwakutegemea elnino.mahindi yangu yamekwamia kwnye udongo mm na wenzangu.tulipokuwa tunapanda baadh ya watu walikuwa wanatucheka kwakuamini kuna elnino
 
Back
Top Bottom