Naomba tafsiri ya ndoto hii

Madalali wa ulozi
 
Madalali wa ulozi
aisee kwahiyo mleta mada ndio dalali mwenyewe au wale jamaa wanaomjia usiku?
 
Kama una sali muombe Mungu akuonyeshe inamaanisha Nini

Halafu soma Ayubu 33:14-16
 
Utaingia katika mahusiano ambayo mwanzo yatakuwa matamu na mwisho yataingiwa na giza. Suruhu: futa namba zao haraka kichwani mwako.
 
Kama mwezi mmoja au miwili nyuma niliota nipo sehem na mwenzangu ambaye nahis alikua mwanaume ambaye cjui kama namjua au simjui ila ni kama vile alikua ananiongoza yaan anataka kunionyesha kitu ambacho aliniambia mie nikambishia kuwa hicho kitu hakiwezekan.

Kwahiyo akaniambia kama unabisha twende tukafika sehem kama kulikua nankitanda hivi akainama kidogo uvunguni mwa kitanda akanyanyuka na mie nikafanya vile vile sasa ile nanyanyuka pale uvunguni natembea hatua mbili kugeuka nyuma nikaona kuna mwanaume kavaa kilemba chekundu anatufuatilia kwa nyuma japo tumemuacha mbali kidogo lakn anaonyesha juhudi za kutukimbilia nikawa naogopa huku tunaendelea kutembea tukafika sehem kuna kama uwanja na watu wengi yule akajitokeza mtu mmoja akaniambia ukitaka huyo asiwafuatulie chukua mtama huu hapa mmwagie.

Sasa nikachukua mtama ile namumwagia hiv akaukwepa japo ulimpata kidogo kwahivo tukaendelea kutembea na tukampiga chenga pale kwenye kundi la watu! Ila tumetembea mbele kidogo mara tena nikamuona huyo katokea manake katutafuta hadi katuona ndoto ikaishia hapo.

Siki ya pili yake tena nikaota mwanaume kavaa kilemba cheusi na yeye ananifuata aah sikumbuki ndoto yake ilikuaje lakin nakumbuka tu hapo kuwa alinifata.

Sasa umepita huo muda zaid ya mwezi mmoja leo tena nimeota watu wawil wale wale mmoja kavaa kilemba chekundu na mwingne cheusi eti wamekuja pembeni ya kitanda changu halafu wakanisujudia kkaa wananiomba kitu hivi

Naombeni anayejua tafsir ya ndoto hii yenye muendelezo anisaidie maana hata sielew ni kina nan hao wanaonifuata?

Na kwanini wamefunga vilemba? Sioni sura zao vizuro lakin najua ni wanaume weusi na vilemba wamevifunga vizuri tu.

Msaada wenu tafadhali maana naogopa sana!
Kuna mambo yenu ya asili yanayo kuandama wewe utaweza kuwa mganga wa asili siku za mbele. Hebu jaribu mababu zako kama wapo hai wataweza kukwambia kitu chakufanya. Au kama kuna mganga katika familia yenu amesha kufa akiwani babu au bibi basi ujijuwe utamrithi kwa dalili ya hiyo ndoto yako.
 
Aseee! Miaka 30 plus jaman kwel uganga unisogelee?
 
Kama mwezi mmoja au miwili nyuma niliota nipo sehem na mwenzangu ambaye nahis alikua mwanaume ambaye cjui kama namjua au simjui ila ni kama vile alikua ananiongoza yaan anataka kunionyesha kitu ambacho aliniambia mie nikambishia kuwa hicho kitu hakiwezekan.

Kwahiyo akaniambia kama unabisha twende tukafika sehem kama kulikua nankitanda hivi akainama kidogo uvunguni mwa kitanda akanyanyuka na mie nikafanya vile vile sasa ile nanyanyuka pale uvunguni natembea hatua mbili kugeuka nyuma nikaona kuna mwanaume kavaa kilemba chekundu anatufuatilia kwa nyuma japo tumemuacha mbali kidogo lakn anaonyesha juhudi za kutukimbilia nikawa naogopa huku tunaendelea kutembea tukafika sehem kuna kama uwanja na watu wengi yule akajitokeza mtu mmoja akaniambia ukitaka huyo asiwafuatulie chukua mtama huu hapa mmwagie.

Sasa nikachukua mtama ile namumwagia hiv akaukwepa japo ulimpata kidogo kwahivo tukaendelea kutembea na tukampiga chenga pale kwenye kundi la watu! Ila tumetembea mbele kidogo mara tena nikamuona huyo katokea manake katutafuta hadi katuona ndoto ikaishia hapo.

Siki ya pili yake tena nikaota mwanaume kavaa kilemba cheusi na yeye ananifuata aah sikumbuki ndoto yake ilikuaje lakin nakumbuka tu hapo kuwa alinifata.

Sasa umepita huo muda zaid ya mwezi mmoja leo tena nimeota watu wawil wale wale mmoja kavaa kilemba chekundu na mwingne cheusi eti wamekuja pembeni ya kitanda changu halafu wakanisujudia kkaa wananiomba kitu hivi

Naombeni anayejua tafsir ya ndoto hii yenye muendelezo anisaidie maana hata sielew ni kina nan hao wanaonifuata?

Na kwanini wamefunga vilemba? Sioni sura zao vizuro lakin najua ni wanaume weusi na vilemba wamevifunga vizuri tu.

Msaada wenu tafadhali maana naogopa sana!
Habari! kwanza hongera na pole moja kati ya hizo itategemea na imani yako!

1: Sehemu ya kwanza:
Kuota mtu ambaye humjui lakini ndotoni unakuwa unajuana nae ni ishara ya kuwa na rafiki wa kiroho au adui wa kiroho kama anakufanyia wema ni rafiki lakini kama anakufanyia uovu ni adui,
Kwa mujibu wa ndoto yako huyo ni jini ambaye upo nae muda mrefu japo hivi karibuni kaanza kujidhirisha na kama umeanza kuona hivi karibuni basi alikuwa kajifunga na umefika muda wa yeye kujidhihirisha sasa mada ambayo mlikuwa mnaongea nae ni ya kuthibitisha nguvu ya miujiza uliyonayo ya kuweza kuwasiliana nae na wewe ukawa unakataa kuwa hilo haliwezekani ndio akajaribu kukudhihirishia kwa kukuonyesha kama unabisha tizama hili linavyowezekana

2: Sehemu ya pili:
Kuota mtu kavaa kitambaa au kilemba chekundu ni ishara ya kuwa na jini jamii ya Masultan au Ufalme lakini kwa kumuota hali ya kuwa ni Mweusi basi ni ishara ya kuwa mtemi au kiongozi wa asili lakini pia kuota mtu na kitambaa chekundu kichwani ni ishara ya kuwa na jini ambaye ni Subiyani(Abdulat e sabyaan) jini ambaye sio mzuri sana na huwa na asili ya ukorofi kwa maana ni jamii ya Ifriit katika majini.
Sasa kwa mujibu wa ndoto yako ni kuwa huyu ndio mwenye kuingilia mambo yako ambayo wewe unataka kuarchieve nae anakuwa anafanya kama kikwazo sasa kwa kuelekezwa dawa ya mtama ni dawa asili ya dawa za kimizimu (majini wa asili) au mzimu wa kwenu ndio unakuelekeza ili huyu asikusumbue mmwagie mtama yaani ufanyiwe tiba ambayo itahusishwa na kumwagiwa mtama ili kumuweka sawa ndio maana baada ya kumwagia mtama akakufuata tena yaani hana ubaya.

3: Sehemu ya tatu:
Kumuona mwingine kavaa kilemba cheusi pia ni ishara ya jini wa asili ya kimizimu nae kukufuatilia ni ishara yupo na wewe katika mambo yako na yupo radhi kukutumikia kwa mambo yako utakayo hitaji kama kukupa baadhi ya siri kama upo interest nayo
Vile vile kuwaota wote wawili wanakusujudia
(HAPANA) kuota unasujudiwa ni ndoto ya kisharifu na kuna watu wachache sana ambao huota ndoto hii na pia masharifu ni wanaume unless nimekosea jinsia yako na vile vile ulivyoona wamekusujudia sio sana wameinama kama kwamba wanaomba kitu ni ishara ya kutii amri zijazo kutoka kwako na hii ni baada ya kuwafanyia shughuli zao za mtama. na kukuinamia hivyo kwa kukutii ni kama kukuachia ufanye chaguo lako je unawataka au la?

Note:
Kwa details zako zaidi ukitoa naweza kukupa muendelezo na nini cha kufanya baada ya hapo.

MAJIBU RAHISI:
Una majini wawili na mmoja anatumia mavazi meusi na mwingine anatumia mavazi mekundu ni wako mwenyewe na wapo muda mrefu japo wanajidhihirisha sasa hivi baada ya kukuona kidogo akili imekomaa hivyo unaweza kuwatumia kwa faida au unaweza kuwapuuza kwa hasara.

HITIMISHO:
Una nguvu ya miujiza ambayo ni Mediumship uwezo wa kuongea na roho zingine soma zaidi hapa kwenye blog yangu:

Kuwa msiri katika baadhi ya mambo yako hususani mambo kama haya ukiyaweka hadharani kila mtu atasema kwa akili zake anazojua mwenyewe

La kukushauri kama ni mtu wa dini basi jaribu kuzungumza na kiongozi wako wa dini ambaye anaelimu pana kuhusu mambo ya kiroho atakwambia ni nini hicho na awe na hofu ya Mungu na asiwe ni mtu wenye tamaa au Jealously au mropokaji maana utapata hasara pia katika watu wanaokuzunguka usimshirikishe mtu yoyote wa karibu yako kwa maana dunia haina siri, vile vile Sio kila ndoto ni ya kuhadithia wengi waliohadithia ndoto zao waliishia kuzipoteza.
Watu wanajua kabisa kwamba wewe unaweza kupata au kuwa nani hivyo jilinde na ushauri wao.

Rakims
 
Maana ya ndoto yako:
1.kuna roho za kichawi/ ugaga zinakusaka yaani unatakiwa kutumikia hizo kazi.
2. Walipokusujudia inamaana wewe ktk ulimwengu was roho utakuwa boss wao yaani utakuwa mkuu wao na wewe utakuwa unawapa order.
 
Nimerudi mara zaid ya tatu ili kukuelewa vizuri! Pamoja na kukuomba nije inbox lakin nina swali hapahapa je ninaweza kuwaomba wajtokeze na waseme wanataka nini badala ya haya kafumbo ambayo siyaelew? Hebu fikiria nisingekutana na wewe ingekuaje?
Kwanini tu yasije yakasema tunataka hivi na hiv?

Naomba nikueleze hapo niliposema wamenisujudia! Ni kweli mie ni mwanamke na nachokumbuka siku ya ndoto ni kuwa walikuja hapa kitandani nilipolala wakapiga magoti wote na mie nawaangalia halaf kila mtu akaweka kiganja chake kwenye paj la uso ishara ya utii halaf wakasujudu wote kwa pamoja halaf wakainua vichwa vyao huku wamepiga yale magot ya sujud wakiniangalia kwa huruma kama ishara ya kuniomba kitu! Hii ndiyo iliniogopesha zaid nikasema mbona kama ni kufuru? Hii siyo roho chafu?

Bahat mbaya ni kuwa nilitembea nikihadithia kila ninayemjua ili angalau anipe mwanga je mimi ni mdhambi kiasi cha kukufuru?
Lakin baadae nilipuuzia mpaka napokutana na andiko lako hapa tena ndiyo naanza kufikiria upya.
Naomba nije pm nikupe maelezo zaid Rakims
 
Maana ya ndoto yako:
1.kuna roho za kichawi/ ugaga zinakusaka yaani unatakiwa kutumikia hizo kazi.
2. Walipokusujudia inamaana wewe ktk ulimwengu was roho utakuwa boss wao yaani utakuwa mkuu wao na wewe utakuwa unawapa order.
Yaan ukisikia miujiza ndiyo hii sasa mwaka huu walah khaaa
 
Kubali ili upate kuwasaidia watu na wewe ufanikiwe mambo yako. Utatajirika kwa uganga
Hapana! Kwanza sijui kama utakua uganga kweli au uzushi tu! Pili nina mambo yangu ya kumtukuza mungu sitaki kuingiza vitu vingine! Halafu nachukia yanavyokuja kwa mafumbo kwanini yasije tu yakasema yanachotaka moja kwa moja mbona yanaanza na kunitsha?
 
Back
Top Bottom