Naomba tafsiri ya ndoto hii

Kama mwezi mmoja au miwili nyuma niliota nipo sehem na mwenzangu ambaye nahis alikua mwanaume ambaye cjui kama namjua au simjui ila ni kama vile alikua ananiongoza yaan anataka kunionyesha kitu ambacho aliniambia mie nikambishia kuwa hicho kitu hakiwezekan.

Kwahiyo akaniambia kama unabisha twende tukafika sehem kama kulikua nankitanda hivi akainama kidogo uvunguni mwa kitanda akanyanyuka na mie nikafanya vile vile sasa ile nanyanyuka pale uvunguni natembea hatua mbili kugeuka nyuma nikaona kuna mwanaume kavaa kilemba chekundu anatufuatilia kwa nyuma japo tumemuacha mbali kidogo lakn anaonyesha juhudi za kutukimbilia nikawa naogopa huku tunaendelea kutembea tukafika sehem kuna kama uwanja na watu wengi yule akajitokeza mtu mmoja akaniambia ukitaka huyo asiwafuatulie chukua mtama huu hapa mmwagie..

sasa nikachukua mtama ile namumwagia hiv akaukwepa japo ulimpata kidogo kwahivo tukaendelea kutembea na tukampiga chenga pale kwenye kundi la watu! Ila tumetembea mbele kidogo mara tena nikamuona huyo katokea manake katutafuta hadi katuona ndoto ikaishia hapo.

Siki ya pili yake tena nikaota mwanaume kavaa kilemba cheusi na yeye ananifuata aah sikumbuki ndoto yake ilikuaje lakin nakumbuka tu hapo kuwa alinifata.

Sasa umepita huo muda zaid ya mwezi mmoja leo tena nimeota watu wawil wale wale mmoja kavaa kilemba chekundu na mwingne cheusi eti wamekuja pembeni ya kitanda changu halafu wakanisujudia kkaa wananiomba kitu hivi...

Naombeni anayejua tafsir ya ndoto hii yenye muendelezo anisaidie maana hata sielew ni kina nan hao wanaonifuata?

Na kwanini wamefunga vilemba? Sioni sura zao vizuro lakin najua ni wanaume weusi na vilemba wamevifunga vizuri tu.

Msaada wenu tafadhali maana naogopa sana!
Ndoto nzuri sana hii
 
Mizimu aka Roho za kiukoo za mababu zina nguvu pia - zinapenda kuabudiwa kwanza kabla ya kukusafishia njia ya mafanikio.
Sahihi kabisa, ndio hao wanaomfuata na bila shaka ama yupo katika mitihani au itafuata.
 
Nimesoma lakin sijaelwa
 
Mizimu aka Roho za kiukoo za mababu zina nguvu pia - zinapenda kuabudiwa kwanza kabla ya kukusafishia njia ya mafanikio.
Sasa zinifuate mie kwa mpango upi? Jaman kwanini znisujudie?
 
Sasa na utu uzima huu itoke wap?
Kwenye ukoo wenu na ina miaka mingi kuliko utu uzima wako, kwa sisi Waafrika hivi vitu si vya kujiuliza vimetokea wapi maana ndiyo asili yetu kabla hawajakuja waarabu na wazungu kuleta dini.
Pamoja na hayo bado asili haipotei.
 
Kwenye ukoo wenu na ina miaka mingi kuliko utu uzima wako, kwa sisi Waafrika hivi vitu si vya kujiuliza vimetokea wapi maana ndiyo asili yetu kabla hawajakuja waarabu na wazungu kuleta dini.
Pamoja na hayo bado asili haipotei.
Aiseee sasa sijui nianzie wapi kujua hiyo mizimu inataka nini na nifanyaje?
 
Ni lazima tuote hilo halikwepeki lakini si kila ndoto ina tafsiri yenye maana ..nyingine ni vague memories tu, kushiba sana ama kulala vibaya nk
Huwa naelewa hiyo na ndiyo maana sinaga mazoea ya ndoto sasa hii ya kuwa na muendelezo halaf watu wazima wananisujudia ndiyo nimeona ni tatizo
 
Huwa naelewa hiyo na ndiyo maana sinaga mazoea ya ndoto sasa hii ya kuwa na muendelezo halaf watu wazima wananisujudia ndiyo nimeona ni tatizo
Ifuatilie mpaka mwisho kuna kitu kinajaribu kujifunua kwako kupitia ndoto
 
Back
Top Bottom