Naomba tafsiri ya ndoto hii

Nimerudi mara zaid ya tatu ili kukuelewa vizuri! Pamoja na kukuomba nije inbox lakin nina swali hapahapa je ninaweza kuwaomba wajtokeze na waseme wanataka nini badala ya haya kafumbo ambayo siyaelew? Hebu fikiria nisingekutana na wewe ingekuaje?
Kwanini tu yasije yakasema tunataka hivi na hiv?

Naomba nikueleze hapo niliposema wamenisujudia! Ni kweli mie ni mwanamke na nachokumbuka siku ya ndoto ni kuwa walikuja hapa kitandani nilipolala wakapiga magoti wote na mie nawaangalia halaf kila mtu akaweka kiganja chake kwenye paj la uso ishara ya utii halaf wakasujudu wote kwa pamoja halaf wakainua vichwa vyao huku wamepiga yale magot ya sujud wakiniangalia kwa huruma kama ishara ya kuniomba kitu! Hii ndiyo iliniogopesha zaid nikasema mbona kama ni kufuru? Hii siyo roho chafu?

Bahat mbaya ni kuwa nilitembea nikihadithia kila ninayemjua ili angalau anipe mwanga je mimi ni mdhambi kiasi cha kukufuru?
Lakin baadae nilipuuzia mpaka napokutana na andiko lako hapa tena ndiyo naanza kufikiria upya.
Naomba nije pm nikupe maelezo zaid Rakims
Karibu mkuu,
Elimu ya kutafsiri ndoto na maono ni kipaji na uwezo ambao mtu anapewa na Mwenyezi Mungu mwenyewe. nimewahi kushindanishwa kufasiri maono na ndoto ya mtu nikaibuka mshindi lakini sikupenda kwa maana haikuwa lengo langu ushindani nilitaka aelewe ni kiasi gani nazielewa ndoto na maana zake na kufasiri ndoto hakuna kitabu wala shule inafundisha bali ni uwezo wa mtu alionao kiroho.

Jibu la swali lako:
Unaweza kuwauliza na kuwaambia chochote na vile wapo katika hali ya kuheshimiana na wewe. jini anapopiga goti na kushika paji lake la uso au anapoinama na kutaka kukushika mguu kama wahindi ni ishara ya salamu ya heshima na upendo maana yake wewe pia ulitakiwa kufanya hivyo hivyo kwao.

Pili wao kukwambia tunataka hivi na vile hawawezi kwa maana hizo ni tabia za mashetani wakimkumba mtu huanza kumwambia tunataka utufanyie hivi na hivi ili tufanye hivi na hivi lakini hao sio mashetani ni viumbe wa kawaida ambao wenzio wanaita roho takatifu/maruhani/mizimu/masters n.k
kwa hiyo furaha ya hao ni kukusaidia na kama sio kukusaidia they mean no harm just friends.

NB:
maneno ya watu wengi na ushaur wa wengi utakupoteza tizama kwa makini ndani ya roho yako inakwambia nini kuhusu wao and that is true maana hakuna jini anaweza kubadili roho ya mtu

Rakims
 
Inasikitisha watu wengi wanaamini kila ndoto unayoota inahusu rangi na majini unatarajiwa kuwa mchawi au mganga.

Low thinkers wana matatizo sana

Rakims
 
Inasikitisha watu wengi wanaamini kila ndoto unayoota inahusu rangi na majini unatarajiwa kuwa mchawi au mganga.

Low thinkers wana matatizo sana

Rakims
Nimerudi tena kusoma hapa! Hii kitu bado inaniandama
 
4 Reactions
Reply
Back
Top Bottom