Naomba tafsiri ya ndoto hii

Maana yake siku za hivi karibuni utaolewa na mganga wa kienyeji. Kwa hyo jipange mama. Ni mwendo wa kula kuku na mbuzi wa kafara kwa mrija.
 
Unadalili ya kua mganga
 
Acha utani kie nauliza kweli ujue
Mambo ya ndoto mda mwingine huwa ni fikra tu na mawazo yako. Ila binafsi hua ninaota usiku kama kuna jambo baya litatokea kesho yake. Mfano kuna siku niliota nimesimama pembeni ya kaburi na watu wengi wamenizunguka wanalia. Ile naamka tu kesho yake asubuhi mjomba wangu akanipigia simu ananiambia rudi nyumbani kuna tatizo nilikua chuo alafu kesho yake kulikua na test. Nikamwambia mjomba siwez nina test kesho. Akaniambia nenda ni muhimu akakata simu. Mda huo huo bro nae akanipgia simu ananiambia rudi nyumban mzee amefariki. So kua makin nenda kanisan mueleze mchungaj uombewe.
 
Kuna baadhi ya ndoto unaota ukiwa hujashiba sawasawa, nyingine ukiwa umeshiba na kupitiliza, nyingine ukiwa na njaa na nyingine ukiwa na madeni lukuki...

Hizi ndoto lazima uwe mwangalifu sana.
 
Inabidi uwe makini na watu ambao utakuwa nao kimahusiano.. Usimkubalie mtu usiyemjua kiundani zaid utakubali mapepo...

Sina mengi ila ni hayo tuu nyota yako iko vyema watu wanataka kuitumia sasa njia ya kukupata ni kwa mahusiano
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…