Naomba niwaage

Ingekuwa vizuri ukaweka wazi uliponaje mkuu,maana sio Ushimen pekee anaeishi kwa hofu tuko wengi humu ndani...

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu usikate tamaa fanya hivi

Anza dosi ya mchanganyiko wa kuchemsha Wa limao ,tangawizi ,kitunguu swahum na chumvi kila wakati wakati huo pata dawa za kupunguza maumivu,weka antibiotic Kali ka ma azithromycin,na kama homa Kali piga na mseto inaweza kua malaria kama shida kupumu chukua salbutamol inhal.Tuliza kichwa punguza mawazo na kwa maelezo hayo ni matumain utaludi hapa janvin kwa kicheko
 

Boss naomba tips kidogo. Kusema kweli sijisikii vizuri.
 
Hahaha,pole,,wiki iliyopita nilipata homa kali nusra nitoke mbio kwenda hospital,maana kila nikilala naona joto linapanda kasi Kama niive,,halafu ndani Niko home alone

Kifua nacho kinabana kimtindo,,Mara mbili nakurupuka kitandani na kupepesuka kulifuata getting nitoke nje angalau Basi nifie nje,nisije kuozea ndani watu hawajui nimedead.

Nikajikaza kurudi ndani,nikanywa dawa ya kushusha homa,,wapi,,,nikajikongonja famasi,nikanunua metakeflin,nikarudi nikanywa na kutulia kitandani nikisema Sasa if I die,I die,

Kufikia jioni home imeshuka,

Nikawa Sasa naisikia kea mbali na hii SI kawaida,maana nikimeza dawa Mimi haichukui mda kupona,
Ila Sasa nimetimiza wiki na ushee,

Kifua bado Kama hakiko sawa,lakini ndo hivyo. Wanadai,ukipitisha wiki na zaidi haujawa kuzidiwa kuna uwezekano mkubwa wa kurecover maana mwili unakuwa umeshaanza kumjua adui na kupambana nae vilivyo.

As for me,sijui Kama Ni corona au ilikuwa maralia tu,maana sikuwa na chembe ya kikoozi ama mafua
 
Mkuu kama ni muumini wa biblia pitia mstari huu:
Mithali - 18:21
Mauti na uzima huwa katika uwezo wa ulimi; Na wao waupendao watakula matunda yake.

Haijalishi upo kwenye hali gani, pambania uhai wako huku ukiukiri uhai. Pindi unapopoteza tumaini na kuikiri mauti haina budi kuja.

Watu wengi wanaofanikiwa kuwa karibu na marehemu katika saa zake za mwisho utawasikia wakisema yamkini marehemu alijua ya kuwa anakaribia kufa, ila ukweli ni kuwa huwa mtu anaikiri mauti mwenyewe.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…