Naomba nichukue nafasi hii kumpongeza Museveni

Zero Hours

JF-Expert Member
Apr 1, 2011
12,943
18,665
Naomba nichukue nafasi hii kumpongeza Raisi Yoweri Kaguta museveni wa Uganda kwa wema aliowafanyia wahanga wa tetemeko wa nchini kwake.



Tarehe 4/10/ 2016 Museveni alifanya ziara ya kushitukiza katika wilaya ya Rakai kwa helcopter. Alitumia helicopter kwanza kuzunguka maeneo ya kijiji hicho na kujionea kwa macho yake jinsi watu wa Rakai walivyo athirika na Tetemeko. Baada ya hapo alipata muda wa kuongea na watu wa Rakai.
Hawa watu walikuwa wakilala kwenye migomba kwa hofu ya kulala kwenye nyumba zilizokuwa na nyufa au kubomoka baada ya tetemeko.

Museveni alijitahidi sana kuwatumia misahada watu wa Rakai kama vile Chakula (6.4 tan za unga, 3.2tan za maharage), mablanketi na matundubali kabla yakufika eneo la tukio. Hata ivyo wahanga wa tetemeko wa Rakai walikataa misaada ya chakula na kupokea mablanketi na tundubali pekee huku wakidai kuwa serikali iwasaidie kujenga nyumba zao sababu tetemeko halikuaffect mashamba bali ni nyumba zao. Watu wa uganda walilalamika sana ni kwanini museveni alitoa msaada Tanzania wa million 600 tsh huku akiwaacha wahanga wa Rakai wakilala kwenye migomba na miti ( plantations).



Baada ya museveni kufika Rakai na kujionea mwenyewe alitoa ahadi ya kuwapa misaada ya kujenga nyumba. Alihaidi kuwapa mabati 13 kila nyumba pamoja na nondo na siment. Hsta hivyo mpaka sasa mchakato wa kufikisha huu msaada haujakamilika. Inasemekana ni zaidi ya nyumba 500 zimebomoka huku kama 400 zilikuwa na nyufa.

Nachompongeza museveni ni kuwa kajitahidi kuwasaidia wahanga wa tetemeko nchini kwake ingawa hakupokea misaada toka nje wala kuwachangisha wananchi wake. Na zaidi ya hapo walitoa million 600 kusaidia wahanga wa kagera. Chakula, matundubali na mablanket unaweza kuzaraulika kuwa si msaada wa maana lakini angalau kafanya kitu kuliko kutosaidia kabisa.

Hata ahadi aliyotoa kuwasaidia watu wake mpaka sasa ina 60% kufanikiwa maana mchakato wa kuandikisha nyumba zilizobomoka na kupata nyufa ndyo umeisha. Muda si mrefu watu wa Rakai watapata misaada walioaidiwa.
 
cf9e079f677694c971fc137ea9a73820.jpg
 
Huyu wenu na PhD yake hajuhi hata maana ya social security na humanity. Na angepewa kuongoza shirika la The hamnesty int. basi wahanga wangejinyonga hapa duniani ..a such useless figure reveals how poor Africans are blessed.
 
Huyu wenu na PhD yake hajuhi hata maana ya social security na humanity. Na angepewa kuongoza shirika la The hamnesty int. basi wahanga wangejinyonga hapa duniani ..a such useless figure reveals how poor Africans are blessed.
Watzi wameokota apple chini ya mlimao.
 
Back
Top Bottom