NAOMBA MSAADA: WhatsApp Cloud API (Access Token, Phone Number ID na App Secret)

NAOMBA MSAADA: WhatsApp Cloud API (Access Token, Phone Number ID na App Secret)

Millifire69

Senior Member
Joined
Jul 8, 2021
Posts
146
Reaction score
151
Habari wakuu,

Naomba msaada kwa mtu mwenye uzoefu wa WhatsApp Cloud API na Meta Developers.

Nimejaribu mara nyingi ku-set up WhatsApp Cloud API kwa matumizi yangu binafsi, lakini nimekwama kupata Access Token, Phone Number ID na App Secret kwa sababu Meta ime-restrict account yangu.

Niliomba review tangu wiki iliyopita, lakini mpaka sasa sijapata majibu yoyote. Nimejaribu njia mbalimbali, lakini bado sijafanikiwa, hivyo kwa sasa nipo njia panda.

Kama kuna mtu mwenye uzoefu ambaye anaweza kunisaidia kufanya setup upya kwa utaratibu sahihi, kunielekeza hatua kwa hatua, au kunisaidia kutatua restriction iliyopo, nitashukuru sana.

Pia, naomba ushauri kwa yeyote aliyewahi kukutana na changamoto kama hii: Je, ni bora kuendelea kusubiri review ya Meta au kuna njia nyingine sahihi ya kutatua tatizo hili?

Mwenye ujuzi naomba aniandikie PM. Niko tayari kujadiliana kuhusu malipo ya huduma ikiwa itahitajika.

Asanteni sana.
 
Back
Top Bottom