Naomba msaada wa kisheria. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Naomba msaada wa kisheria.

Discussion in 'Jukwaa la Sheria (The Law Forum)' started by tpaul, Jun 2, 2010.

 1. tpaul

  tpaul JF-Expert Member

  #1
  Jun 2, 2010
  Joined: Feb 3, 2008
  Messages: 13,092
  Likes Received: 3,586
  Trophy Points: 280
  Wakuu heshima zenu,
  Wandugu kuna rafiki yangu mmoja ameachishwa kazi kinyume cha sheria, naomba msaada wenu wa kisheria jinsi anavyoweza kupata haki zake.

  Huyu bwana alikuwa akifanya kazi kwenye kiwanda kimoja cha kutengeneza nondo jijini Dar. Kwa bahati mbaya, akiwa kazini, alikatwa kiganja cha mkono wake wa kulia na mashine za kiwandani. Juhudi za madaktari kuurudishia mkono wake ziligonga ukuta. Alitibiwa jeraha la mkono uliopatwa na ajali na baada ya kupona alirejea kazini. Kwa kuwa hakuweza kufanya kazi zake kwa ufanisi kama ilivyokuwa mwanzo, mabosi wake walimhamishia kwenye kitengo kingine ndani ya kiwanda kwa muda. Lakini cha ajabu ni kwamba alipewa muda wa miezi mitatu kuomba kazi nyingine ndani ya kiwanda(endapo zitatangazwa) au nje ya kiwanda na endapo asingeweza kupata kazi yoyote basi angekuwa terminated from employment.

  Baada ya kuisha miezi mitatu hakuna kazi yoyote aliyoipata ndani au nje ya kiwanda. Ikabidi atimuliwe bila huruma na bila kulipwa chochote zaidi ya kugharamiwa mkatibabu ya mkono wake.

  Je, hii ni halali kisheria? Je, ni utaratibu gani wa kisheria ambao ulikiukwa hapa? Sheria za nchi zinasemaje kuhusu mtu aliyepata ulemavu kazini kama huyu ndugu yetu? Wadau naomba msaada wa kisheria katika hili na jinsi tunavyoweza kumsaidia huyu jamaa apate haki zake za kimsingi na kisheria.

  Asante sana.
   
 2. Mapondela

  Mapondela JF-Expert Member

  #2
  Jun 4, 2010
  Joined: Mar 31, 2009
  Messages: 457
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Pole sana.

  Bwana kwenye hilo itabidi ajaribu aende katika kituo cha msaada wa sheria. Kwani kuna mambo mengi katika dai hili yanatakiwa kuzingatiwa kwa mfano:- Mkataba wake wa kazi unasemaje, Je kampuni in Work Man's compensation scheme? Je alikuwa ana contributions za NSSF kwani siku hizi liability nyingi zimetolewa kwa muajiri na mwajiri anachangia kwenye hizo pension scheme ikiwa na matibabu ikiwa mfanyakazi ameumia. Hivyo aende huko na vigezo vya kuthibitisha kama kweli aliajiriwa nao na terms zikoje halafu watamsaidia.

  Pia sheria mpya ya kazi ambayo imeainisha sababu za muajiri kumuachisha kazi mfanyakazi ni pamoja na kama hawezi tena kutumika anaweza kuachishwa kazi, E.D zikizidi siku 126 kwa mwaka pia unaweza kufukuzwa kazi, kama huna ujuzi na ofisi imebadilisha miundo mbinu ambayo wewe mfanyakazi huwezi kuitumia wanaweza kukuachisha kazi.
   
 3. tpaul

  tpaul JF-Expert Member

  #3
  Feb 8, 2014
  Joined: Feb 3, 2008
  Messages: 13,092
  Likes Received: 3,586
  Trophy Points: 280
  Hizo zote ni changamoto zinazosababishwa na wawekezaji uchwara wanaobebwa na serikali dhalimu ya CCM. Wakati mwingine dawa rahisi ya matatizo kama haya ni kuwang'olea mbali magamba wanaokaribisha na kuwapa bichwa wawekezaji mpaka kufikia hatua ya kuwaonea na kuwadhulumu wananchi kiasi hiki! Haya yote yana mwisho wake. Tuombe Mungu 2015 wananchi wafunguke akili wawapige chini hawa manyang'au wenye njaa!!!!!!
   
Loading...